Uchaguzi 2020 Wananchi wa Kawe mnafahamu jambo hili?

Huu ukurasa wa kwanza umenitisha, ukiacha Mr. Zero said, wengine wote ni ID mpya/ngeni, inawezekana vipi mtu mmoja akafungua ID nyingi hivi? Nawaza tu, sina ushabiki na wanasiasa kwakuwa wana DNA moja
 
Basi haina maana ya sisi wananchi kuchagua wabunge tuwaachie tu serikali ifanye majukumu yake yenyewe ili tusiwe na lawama kwa watu wasiohusika.
Wabunge ni wawakilishi tu wa wananchi kwasababu hatuwezi kukusanyika pamoja nchi nzima mzee. Hivyo anatupelekea maoni yetu kwa serikali
 
Sijui kama ulimuelewa Magufuli kule Mbeya aliposema wamchagulie mbunge wa CCM ili awaletee maji. Pale alikuwa anajaribu kuwatoa usingizini kuwa inayoleta maji au barabara ni serikali kupitia hela zetu sie watz kama kodi. Wabunge kazi yao kutusemea serikalini na pia kuhoji matumizi ya pesa zetu za kodi hali kadhalika kupitisha bajeti inayoletwa na executive. Na jukumu lingine ni kupitisha sheria ambazo zinaletwa bungeni kama miswada au maekebisho yake na kisha kusainiwa na raisi na kuwa sheria kamili. Kuhusu hoja ya kuwaachia tu serikali ifanye majukumu yake ni kweli hili limefanyika siku nyingi sana maana bunge tulilonalo na kama picha ya kuchora tu maana inapitisha mambo ambayo hata kwa mwendawazimu hawezi kupitisha. Ukitaka mfano naweza kuordhesha hapo mambo lukuki. Na kwanini bunge letu liko hivyo? kuna sababu nzito tu nyuma ya pazia
 
Wana jamvi,

Kitabu chenye title TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA JIMBO LA KAWE 2015-2020, kitabu hiki kimejaa kona nyingi sana na giza nyingi kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake. Kuna utekelezaji hewa, fedha zilizoelekezwa hazihakisi kabisa uhalisia wa kile kilichofanyika pamoja na miradi ya kusadikika.

Mzalendo wa Kweli
Kawe-Mikoroshini
Mkuu kudamademede , don't add an insult to an injury, Wana Kawe tuko kwenye maandalizi ya send off, ya Halima, kitendo cha kuitumikia Kawe kwa kipindi cha miaka 10,anastahili send off ya heshima na sio kubezwa!.

Uchaguzi 2020 - Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

P
 
Anko hivi kwa kauli zile za Magu ,kuwa mkichagua upinzani maendeleo haleti, bado mnalaumu wabunge wa upinzani ?
 
Hata Kama Hana hio nguvu lakini kwa sababu ametamka Mara nyingi na anaonyesha chuki dhahir kwa waislamu na uislam akipata ubunge atakua anatusimanga Sana
Hoja yako imekosa mashiko kwenye kuhusisha ubunge na hilo la kufanya misikiti kuwa Sunday schools,sasa hayo ya masimango hata asiye mbunge aweza kufanya hivyo.
 
Wabunge ni wawakilishi tu wa wananchi kwasababu hatuwezi kukusanyika pamoja nchi nzima mzee. Hivyo anatupelekea maoni yetu kwa serikali
Sasa watu wanapo walaumu hawa wawakilishi wetu kwa kushindwa kutekeleza vyema majukumu yao ya kutuwakilishia matatizo yetu basi inaonekana tunawalaumu watu wasiohusika,ndio maana nikasema bora ibaki tu serikali.
 
Sijui kama ulimuelewa Magufuli kule Mbeya aliposema wamchagulie mbunge wa CCM ili awaletee maji. Pale alikuwa anajaribu kuwatoa usingizini kuwa inayoleta maji au barabara ni serikali kupitia hela zetu sie watz kama kodi. Wabunge kazi yao kutusemea serikalini na pia kuhoji matumizi ya pesa zetu za kodi hali kadhalika kupitisha bajeti inayoletwa na executive. Na jukumu lingine ni kupitisha sheria ambazo zinaletwa bungeni kama miswada au maekebisho yake na kisha kusainiwa na raisi na kuwa sheria kamili. Kuhusu hoja ya kuwaachia tu serikali ifanye majukumu yake ni kweli hili limefanyika siku nyingi sana maana bunge tulilonalo na kama picha ya kuchora tu maana inapitisha mambo ambayo hata kwa mwendawazimu hawezi kupitisha. Ukitaka mfano naweza kuordhesha hapo mambo lukuki. Na kwanini bunge letu liko hivyo? kuna sababu nzito tu nyuma ya pazia
Kwa hayo maelezo yako kwahiyo utakuwa unakubaliana na mimi kuwa hawa wabunge hawana faida na hivyo ni kupoteza muda tu kuwachagua?
 
Barabara za makongo juu zote ni vumbi tupu ametekeleza nini hapo zaidi ya kuandika uongo na unafki tu?
Akajipange tena maana safari hii hatutamchagua tena
Kwa upande wangu, ni vizuri kutofautisha kati ya majukumu ya 1) serikali ya kutoa huduma za kijamii nchini kutokana na wananchi kulipa kodi ili wananchi wapate maendeleo na 2) majukumu ya mbunge - kama mwakilishi wa wananchi katika chombo cha kutunga sheria (bunge) - kuishauri na kuisimamia serikali katika kutekeleza majukumu yake hayo. Serikali haiwezi kukasimisha majukumu yake kwa mbuge na wala mbunge hawezi kuinyanyang'anya serikali majukumu yake. Majukumu haya yote yameanishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na ni vizuri wakati tunajadili majukumu haya tuwe na uelewa mzuri na tujue nani ana wajibu upi kwa wananchi. Mfano, mbunge akijenga hospitali, barabara, madaraja, shule nk, serikali katika hilo jimbo itafanya nini kitakacholingana na ukusanyaji wake wa kodi kutoka kwa wananchi? Au je, mwenye jukumu la kukusanya kodi ni mbunge? Sijui hiyo taarifa ya mbunge inasema nini, lakini nimetaka tu kusema inabidi tujue kwanza majukumu ya serikali na ya mbunge kabla ya kuchangia hoja kama hii ili tuweze kutoa michango yetu ya maoni katika suala hili vizuri zaidi.
 
Hoja yako imekosa mashiko kwenye kuhusisha ubunge na hilo la kufanya misikiti kuwa Sunday schools,sasa hayo ya masimango hata asiye mbunge aweza kufanya hivyo.
Whatever
Lakini kwa sababu ameonyesha chuki dhahir kwa waislamu na uislam hata kama gwajima angegombea na mbwa sisi waislamu wa Kawe tungempigia kura mbwa
 
Miaka yote inajulikana kuwa kuna malalamiko ya waislamu kuhusu kuwepo mfumo kristo hapa nchini katika hii serikali ya ccm,ila pamoja na hayo yote bado kuna waislamu wanaipigia kura ccm na kama hilo halitoshi serikali hii hii ya ccm imewashikilia masheik wa uamsho na hawataki hata kuwapeleka mahakamani na ni suala linalopigiwa kelele ila bado waislamu wanaipigia kura ccm.

Sasa wewe hayo ya Gwajima ndio umeona issue kiasi kwamba et waislamu wasimpigie kura? Kama ni hivyo basi hata Lowassa asingepata kura za waislamu.
 
Sijui unatokea kata ipi lakini ungejua namna ambavyo misikiti imepata maji kutoka kwa Gwajima wala usingeshirikisha waislamu wenzio kwenye hili. Waislamu wako tayari kumchagua kiongozi aliyewaletea maji na msaada hata kabla ya kuwa mbunge
 
Gwajima mnafiki eti kachimba visima kule mbagala
Hata Kama angejenga ghorofa ya dhahabu bila kutoa maelezo ya kauli zake waislamu bado hatumtaki
Labda waislamu wanafiki atawapikia ubwabwa watamuelewa
Kwa nini anajipendekeza kwetu
Kwa nini anaficha makucha
Mbona Trump anasema wazi wazi anatuchukia na anahinda uchaguzi
Mimi Namshauri Gwajima asijifiche kwenye kimvuli chake
Sasa hivi tupo kwenye mchakato wa kutengeneza USB nyingi za kashfa zake kwa waislamu halafu tutagawa nyumba hadi nyumba
Hata akishinda lakini waislamu tuondokane na dhima ya kuchagua kafiri
 
Haya hicho kitabu mumekisoma, na sasa kamsomeni kigogo Twitter, aliyoyasem Gwajiboy kayatenda , Duh ni Balaa
 
Miaka yote inajulikana kuwa kuna malalamiko ya waislamu kuhusu kuwepo mfumo kristo hapa nchini katika hii serikali ya ccm,ila pamoja na hayo yote bado kuna waislamu wanaipigia kura ccm na kama hilo halitoshi serikali hii hii ya ccm imewashikilia masheik wa uamsho na hawataki hata kuwapeleka mahakamani na ni suala linalopigiwa kelele ila bado waislamu wanaipigia kura ccm.

Sasa wewe hayo ya Gwajima ndio umeona issue kiasi kwamba et waislamu wasimpigie kura? Kama ni hivyo basi hata Lowassa asingepata kura za waislamu.
Sio masheikh wa uamsho tu
Kuna masheikh mamia kwa mamia wapo jela kwa miaka mi5 hii
Nimeshangaa kusikia kwa miaka mi4 ya magufuli serikali hii inashikilia watu wengi nchini kwa tuhuma za ugaidi kuliko Afghanistan na Iraqi!!
Anyway waislamu tunaangushwa na wanafiki mashekh ubwabwa hata mtu kafiri kama Gwajima akiwapikia ubwabwa amewapata
 
Wana jamvi, nawasalimu mchana huu na hongera kwa majukumu ya kulijenga Taifa letu pendwa.

Nimefanikiwa kusoma kitabu cha Halima Mdee mbunge aliyemaliza muda wake wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kitabu chenye title TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA JIMBO LA KAWE 2015-2020, kitabu hiki kimejaa kona nyingi sana na giza nyingi kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake. Kuna utekelezaji hewa, fedha zilizoelekezwa hazihakisi kabisa uhalisia wa kile kilichofanyika pamoja na miradi ya kusadikika.

Nina uhakika kabisa mtu aliyemshauri Halima Mdee kuandaa kitabu hicho alijua kuwa hajafanya chochote na ndio njia ya kumuonesha kwa wananchi wamjue tunapoelekea kwenye uchaguzi; asante sana muandaaji na mshauri kwa kutuokoa na kirusi hiki tulichoishi nacho kwa miaka 10.

Kelele nyingi zinazopigwa na Wabunge wa upinzani zinaonekana kuwa za kweli lakini kama utekelezaji ni wa namna hii, basi huenda wapinzani wakawa ni hatari sana kuliko mtu yeyote yule.

Namalizia summary ya kitabu hiki na nitaileta kwenu moja kwa moja

Mzalendo wa Kweli
Kawe-Mikoroshini
Sasa unakosoa vp kabla hujamaliza ? Lakini unaelewa kazi ya mbunge? Tena hasa wa upinzani
 
Hayo uyasemayo n ya kweli Kabsa nilipitia baadhi ya nyaraka hakuna alichokamilisha kila kitu n kinaendelea for 10yrs ameshindwa kutatua matatizo ya kawe halima hafai kabsa kuendelea kushikilia kawe

Sasa atatue matatizo ya kawe yy ndio serekali? Au yy anasimami serekali au unadhani kawe ni nchi na yy ndio rais? Au hujui kazi za ubunge?
 
Kwa hayo maelezo yako kwahiyo utakuwa unakubaliana na mimi kuwa hawa wabunge hawana faida na hivyo ni kupoteza muda tu kuwachagua?
Yes kwa katiba tuliyonayo ni kweli raisi ni dikteta mbaya kuliko hata Idi Amini.
 
Sasa watu wanapo walaumu hawa wawakilishi wetu kwa kushindwa kutekeleza vyema majukumu yao ya kutuwakilishia matatizo yetu basi inaonekana tunawalaumu watu wasiohusika,ndio maana nikasema bora ibaki tu serikali.
Tatizo mhimili mmoja uitwao executive ni bingwa wa rushwa za waziwazi. Kwanza kupitia chama chao wanaamua wao executive nani atakuwa mbunge na sio wananchi, Hapo mbunge lazima awatumikie halafu ubunge ni kazi ya mishahara mikubwa na marupurupu lukuki huku wakijinadi ni watumishi wa wananchi wakati hata mishahara wanajipangia. Kumbuka kikokotoo walikipitisha bila aibu ila wao hakiwahusu
 
Back
Top Bottom