Wananchi wa Kijiji cha Andikoni (Pemba) wabeba Wagonjwa begani kutokana na ubovu wa Barabara

Wananchi wa Kijiji cha Andikoni (Pemba) wabeba Wagonjwa begani kutokana na ubovu wa Barabara

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Wananchi wa Kijiji cha Andikoni, Shehia Chumbageni, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba walazimika kuwabeba wagonjwa wakiwa kwenye vitanda katika mabega kutokana ubovu wa barabara ili kupata Huduma za Afya.

Wakizungumza na HalisiMediaOnline, baadhi ya Wananchi wamesema wanapitia wakati mgumu kutokana na ubovu wa Barabara na kwamba mvua ikinyesha hali inakuwa mbaya zaidi.

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid, amesema Serikali ina mpango wa kujenga barabara hiyo.

Chanzo: HALISI MEDIA ONLINE
 
CCM oyeeeee.
Alafu mkuu w nchi anakumbatia wezi n mafisadi.

KAZI ni kipimo cha utu
 
Haya mambo tumezoea Tanganyika kwa mnaofaham iyo sehemu mna uhakika ni Zanzibar sio Tanganyika kweli???
 
Acha kufuatilia maisha ya jirani wakati kwako yamekushinda
 
"...lakini hakuna kiongozi aliyekuwa hakufika..."
 
Back
Top Bottom