Wananchi wa Kijiji cha Andikoni, Shehia Chumbageni, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba walazimika kuwabeba wagonjwa wakiwa kwenye vitanda katika mabega kutokana ubovu wa barabara ili kupata Huduma za Afya.
Wakizungumza na HalisiMediaOnline, baadhi ya Wananchi wamesema wanapitia wakati mgumu kutokana na ubovu wa Barabara na kwamba mvua ikinyesha hali inakuwa mbaya zaidi.
Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid, amesema Serikali ina mpango wa kujenga barabara hiyo.