Wananchi wa Kijiji cha Nyangunge hawana maji baada ya vituo vya kuchotea kufungwa

Wananchi wa Kijiji cha Nyangunge hawana maji baada ya vituo vya kuchotea kufungwa

KwetuKwanza

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
82
Reaction score
150
1000077327.jpg

Nimeona Habari hii ITV, nikasema ngoja nishare na wanajukwaa.

Inatoka uko Kijiji cha Nyangunge kilichopo katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wananchi wa Kijiji hicho wanasema wamekosa huduma ya maji safi na salama kutokana na vituo vya kuchotea maji kufungwa zaidi ya miezi miwili Sasa.

Wananchi hao wanategemea mradi wa maji ambao ulijengwa na Serikali uliopo kijijini hapo, lakini tangu mradi umekamilika hawapati huduma kutoka na vituo nane ambavyo vipo kijijini kwao kufungwa.

Siyo kwamba mradi hautoi maji, Hapana mradi unatoa maji, tatizo vituo vile Kwa kuchotea maji kwenye jamii vimefungwa.

Wenyewe wanasema wale wachache ambao wamevuta maji majumbani, hao wanapata huduma vizuri, lakini wale ambao ni wengi na wanategemea hivyo vituo vifunguliwe wafuate maji Sasa havifanyi kazi, vimefungwa muda mrefu.

Katika taarifa hiyo wasimamizi wa huo mradi wanasema wamevifunga vituo hivyo Kwa sababu havina wasimamizi.

Wanasema wananchi wenyewe wamekataa kupewa kazi ya kuvisimamia wakidai malipo ni kidogo.

Habari hii nimeiona Global tv.


View: https://youtu.be/WiPyQNkRDI0?si=cMzDVjD91d6hMiss
 
Back
Top Bottom