Pre GE2025 Wananchi wa Kilimanjaro wachangishana kurekebisha barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 72

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huu ni ujumbe kuwa Dr. Kimei anapelea hapo Jimboni.
Kati ya jimbo ambalo halina mbunge ni jimbo la Vunjo.
Alitokea mfadhili mmoja kutaka kurekebisha barabara ya Mamba Kiria, Kimei kwa woga alienda kumshtaki bungeni kwamba ana ingiliwa kwenye jimbo lake. Bahati nzuri mfadhili alisha weka kifusi hadi nyumbani kwake na mchezo uka ishia hapo.
Kimei ni bomu hatuna mbunge.
 
Mimi nilidhani moshi yote ni lami hadi chooni. Sasa km 72 zimetoka wap?
Pamoja na kuchanga lakin ibane serikali iwajengee Barabara mnalipa kodi kubwa kupitia luku nk halafu pesa zinapeleka wasanii korea?
Na mimi nilikua najua hivyo zamani mpaka pale nilipompeleka binti yangu shule. Kuna sehemu moshi barabara ni mbaya sana. Kipindi cha kiangazi vumbi kama lote, kipindi cha masika tope kama lote. Tabu tupu
 
Hongera sana wananchi na kanisa la KKKT. Barabara inayotengenezwa sio straight line road Moja ni muunganiko wa feeder road way za mitaa mingi ambazo wanaishi watu huko vijijini na kuunganisha na barabara kuu.
Ni SAWA tunatoa pongezi ila km 72 parefu sana hata ingekuwa mitaa 20
 
Inashindwa vipi kutimiza on time? Mbona Barabarani kumejaa Magari Bland mpya za Serikali?Huu ujinga haupaswi kuendelea kuwepo.
maybe right but gov ina priorities, the truth hizi hawawez kubrovide everything everywhere. Ni ukweli ambao hawataki kuusema, na hapa ndipo uchawa unapoanzia

back to wananchi wamefanya the right thing, hawawez kaa wanaisubiri serikal wakati wana uwezo huo, na wao ndio wenye shida
 
The Geneva of Africa?! We’ve failed to put in place infrastructure to attract investment for the many multinationals who are disappointed at their arrival in Arusha only to find a tiny shoddy town. When would the government care for rural infrastructure which they don’t even think exist.
 
Utasikia CCM kwenye kampeni wakijinadi kuwa Mama Samiah amewajengea wanakijiji wa Kiruweni kwa kiwango cha changarawe jambo ambalo wanaume walishindwa.
 
I agree with you, it's really disappointing how bad the road standards are.

It seems like nobody cares.

Why are we so selfish and careless?

Don't we want better streets?

The roads in Arusha ARE IN TERRIBLE CONDITION .

It's a shame that neither us residents nor the so called government seem interested in improving our city.

I believe corruption and selfishness are to blame. It's ridiculous that so much money is collected but only a few benefit and we just allow it to happen 🤡
 
Hawalipi Kodi? Yaani Kodu walipe zineende kununua wapinzani, kulipa Bongo Muvi kule Korea then Raia wachangishane kijenga Barabara. Wachaga wamenza ufala
Fikiri boss, Nchi nzima tukiweza kufanya hivi nini kitatokea. Maana tunawanyang'anya wagombea na viongozi sababu ya kuwapa kura na kodi. Unakuja unakuta tushatengeneza barabara zetu, tushavuta maji yetu, tuna hospitali zetu. Haya tuambie unataka pesa zetu ukafanyie nini? Unataka kura zetu utupe nini?
 
Kwa hiyo ni sawa kununua v8 ila sio sahihi kutenga fedha kwa ujenzi wa barabara za vijijini?
 
Na mimi nilikua najua hivyo zamani mpaka pale nilipompeleka binti yangu shule. Kuna sehemu moshi barabara ni mbaya sana. Kipindi cha kiangazi vumbi kama lote, kipindi cha masika tope kama lote. Tabu tupu
Washukuru Mungu zile lami za kuelekea kwenye mageti ya mlima Kilimanjaro ( hizo ndo zinawafanya wajione wameendelea) la sivyo moshi ni sehemu yenye Barabara mbovu kupindukia sio moshi tu. Kasikazini kote ikiwepo hii Barabara kuu ya moshi Arusha ina viraka hatari. Kuna ile ya kuelekea chemka waterspring, kuna ya kahe, mabogini, majengo, kibosho juu kule, uru nk. Kote huko Barabara zinatisha na yale mabonde na milima sasa.
Sijui wachagga huwa kiburi cha kujiona wameendelea kinatoka wap wakati huo mkoa bado sana ( bila kusahau hiace zao chakavu za kuelekea huko vijijini nyingine zina kunguni) na sasa mji wa moshi umevamiwa na bajaji na bodaboda vijana wanatia huruma sio poa.


Sisi Bukoba tushajikubali kuwa na matatizo ndo maana tumetulia. Na kinachopatika kinaijenga Bukoba mdogo mdogo wala hatuna kelele. Bukoba sasa kuna ujenzi wa Barabara ya njia nne km 5.1, stendi mpya mbili, shopping complex, upanuzi wa bandari nk.

Acha takwimu za serikali zizidi kuwadanganya wazubae
 
I believe corruption and selfishness are to blame. It's ridiculous that so much money is collected but only a few benefit and we just allow it to happen 🤡
In addition to these, in Tanzania we have put a gang of dull skunks to lead us, they don’t know the basics for a good town! I believe ignorance rules over the purported leaders of this country and it’s up until we’re tired of these idiots we’re nowhere.
 
Hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa.

Kadiri wananchi wanavyoachana na kuitegemea serikali ndivyo wanavyozidi kupata nguvu na mwishowe serikali haiwezi kuwa na maamuzi juu yao bila wananchi kusema hivyo.

1. Haya mambo si magumu sana. Tuanze kuongea na majirani zetu hapo mtaani tusiwe wabinafsi sana, inawezekana kabisa kuhalikisha barabara za mtaa zinapitika miezi 12 ya mwaka.

2. Jinsi mitaa/vijiji vyetu inavyopendeza kwa kuwa na barabara nzuri, miti imepandwa vizuri, vibanda vya kuuzia vitu vidogo vidogo vimepangwa vizuri ndivyo spirit yakutaka maendeleo zaidi inakuwa kali.

3. Kuishi kwenye mitaa michafu, barabara mbovu, uhalifu etc inakatisha sana tamaa na inazuia watu kuwaza kwa ukubwa kwasababu hii hali ni kifungo. Ukisikia mikono yako haijafungwa pingu lakini haupo free ndiyo hali hii niliyoelezea.
 

Unakosea.

Hii si kuhusu sisi Wachaga wale Wahaya.

Wananchi wa Kilimanjaro walio wengi wala hawana habari yakujisifia eti mkoa umeendelea kuliko mikoa mingine.

Hapa jambo la msingi ni kuboresha hali zetu iwe unaishi Nachingwea au Njiro Arusha.

Watu wote wanastahili maisha mazuri yasiyo na stress.
 
Hizo Greda zipo halmashauri mnachangia mafuta na posho tu ndio mnaita tena kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa , ni mchango tu kwa nyumba hadi nyumba maana zile Greda zinakula mafuta .

Watoto mbona wanachangia wanasafishiwa uwanja wa mpira , ukisema barabara ni ile iko full lami ndio barabara kwa sehemu nyingi ni uongo kusema hamna , ila ukipitisha bila ya lami na huo udongo kipind vcha mvua ndio yale yale tope la kufa mtu .

Kama wanajenga lami ni jambo la pongezi kubwa kwa sababu sio suala la kitoto ila kama wanasafisha ni kawaida sana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…