Pre GE2025 Wananchi wa Kilimanjaro wachangishana kurekebisha barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 72

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe binti vp? Yaani unasema mkuu wa mkoa anawazindua wachagga au wao ndio wamzindua mkuu wa mkoa na boss wake yule bibi wa matumizi?
 
Mtasubiri sana mletewe maendeleo na huyo mama wa matumizi.
 
Mbona Huwa mnatuambua Kilimanjaro Ina lami Hadi kweymigomba,Sasa imekuaje tena? 😁😁😁
 
wakati huo huo report za CAG zinaonyesja upigaji upigaji, mimi concern iko hapo tu.
 
Kabisa. Tukiambukizana hii spirit ni suala la muda tu.
 
Sisi tuliokaa humu toka miaka ya 2016 tunaongea tuchokijua kupitia nyuzi zinazoanzishwa humu kuhusu Moshi na vijiji vyake.
Labda ndo vinafanya serikali ipotezee moshi kwa sababu ya majigambo kuwa wameendelea. Tanzania nzima hii wengi wanaamini Kilimanjaro na huko kasikazini kumeendelea lami kila sehemu, maji safi, makazi bora nk. Jambo ambalo sio kweli hata kidogo. Tanzania kama nchi bado sana
 
Hiiiiiiii jamani!!
Bado sijachanga kwakweli. Watu watumbue pesa huko, mie nichangie!!!
 
Na mimi nilikua najua hivyo zamani mpaka pale nilipompeleka binti yangu shule. Kuna sehemu moshi barabara ni mbaya sana. Kipindi cha kiangazi vumbi kama lote, kipindi cha masika tope kama lote. Tabu tupu
Nyie badala ya kuwaunga mkono hawa watu kwamba wanajitahidi kujenga barabara za kuunganisha mtaa na mtaa huko vijijini badala yake mnawacheka?!! Kweli nchi ina watu!
 
Sasa ukitoa hisia zako kuhusu Kilimanjaro kwasababu ya nyuzi 10, 50 au 100 hapa JF basi you are making a blunder.

Tanzania ni ya kwetu wote.

Nini kuhusu Kilimanjaro, Kagera au Arusha au Mbeya?

Pia tazama namna ulivyoelezea kuhusu serikali haipeleki miradi ya barabara Moshi kwasababu wakazi wa Moshi wanajisifia.

Are you serious man?

Hiyo si namna bora yakufikiria jambo.

Critical thinking ni muhimu. Kwasababu itakusaidia kuwaza kwa usahihi.

Uwe na siku njema.
 
Mbona Huwa mnatuambua Kilimanjaro Ina lami Hadi kweymigomba,Sasa imekuaje tena? 😁😁😁
Ngoja ufike utacheka , sehemu nyingi ni maungio ya kwenda mlima kilimanjaro ndio kuna lami , Na hizo sehemu hawakujenga walipelekewa na serikali kipindi viongozi walikuwa wachaga .

Angalia hata youtube msiba wa Gadner , watu kibao huko kwao hamna lami kawaida sana labda sehemu kama Machame na Rombo kwa mbali .
 
Mnatakiwa kuwa hivi kitu kimoja ipo siku mtafika , japo malumbano ni lazima
 
Tofauti ya watu wa Bukoba na watu wa Moshi ni kwamba watu wa Bukoba wanajengewa wakati watu wa Moshi wanajijengea miundombinu kwa fedha zao za michango.
 
Wewe binti vp? Yaani unasema mkuu wa mkoa anawazindua wachagga au wao ndio wamzindua mkuu wa mkoa na boss wake yule bibi wa matumizi?
Mlikuwa wapi miaka yote, wenzenu mwanza wameanza zamani sana kujenga barabara zao wenyewe, tena kwa kiwango cha mawe, ambazo ni nzuri kuliko za lami.

Mkuu wenu wa mkoa katokea Mwanza nini?
 
Kwa hiyo ni sawa kununua v8 ila sio sahihi kutenga fedha kwa ujenzi wa barabara za vijijini?
I never said ni sawa, but hii nchi ni kubwa mno and kila mkoa kijiji wiliaya mtaa kuna mahitaji? Is a question of priority, hawawez kufanya yote at once
Siwatetei but hili gov hawataki kulisema but ndio hali halisi

Now back to wananchi, wao ndio wenye uhitaji when gov seems slow wakichukua hatua ni jambo jema zaidi and i support them
 
Mlikuwa wapi miaka yote, wenzenu mwanza wameanza zamani sana kujenga barabara zao wenyewe, tena kwa kiwango cha mawe, ambazo ni nzuri kuliko za lami.

Mkuu wenu wa mkoa katokea Mwanza nini?
Hujui historia ya Kilimanjaro miaka ya 1950 watu walishajenga barabara na madaraja vijijini kwenda kwenye mashamba ya kahawa chini ya chama cha wenyeji KNCU. Miaka hiyo watu wa Mwanza walikuwa hawajitambui kwamba wao ndio ng’ombe au ng’ombe ni akina nani!
 
Nani kasema hawawezi kufanya yote? Mnaaminishwa hivyo kwa sababu fedha nyingi zinapelekwa kwenda kushibisha matumbo yao na nyie kwa sababu hamfikirii vizuri mnakubali tu!

Kuna fedha nyingi sana zinatumika ndivyo sivyo hapa nchini na nyingi zinaenda kushibisha kundi la watu wachache.

Endapo zikepelekwa zinapotakiwa kwenda nchi hii ingekuwa mbali sana kimaendeleo
 
Soma reply yangu vzr na hoja imeanzia wap.
Vinginevyo umekurupuka kunijibu.
Uwe na siku njema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…