Pre GE2025 Wananchi wa Kilimanjaro wachangishana kurekebisha barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 72

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama walijenga sasa wanafanya nini? Wanabomoa?

Ungenambia kuiba ningekuelewa.
 
Nyie badala ya kuwaunga mkono hawa watu kwamba wanajitahidi kujenga barabara za kuunganisha mtaa na mtaa huko vijijini badala yake mnawacheka?!! Kweli nchi ina watu!
Nioneshe kicheko changu
 
Mbunge kazi yake sio Kujenga Barabara ni kuisimami Serikali,
Kazi ya Bunge ni kuisimamia Serikali. Hata hivyo, mbunge anapaswa kuwasilisha changamoto za eneo lake kwa Serikali ili zipate utatuzi. Hata hivyo,.kwa miradi midogo inaweza kutekelezwa kupitia fedha za Mfuko wa Maendeleo wa Jimbo. Fedha hizi ziko chini ya mbunge. Hivyo, hakuna utetezi kwa mbunge ikiwa Jimbo lake litakosa huduma muhimu.
 

..Watz wengi wameaminishwa kwamba Kilimanjaro "imependelewa" kwa miundombinu ya kila aina. Hata ukisoma mijadala mbalimbali hapa JF utakutana na hoja za namna hiyo.
 
🙄
 
Mimi naona sehemu za vijijini vya kilimanjaro zote zinafikika kwa gari na lami imeunganisha sehemu zote muhimu labda useme lami hazipo kwenye hizo chochoro za kuunganisha kijiji kimoja kwenda kingine ambazo ndio wanaziweka kokoto tu.
 
Mimi naona sehemu za vijijini vya kilimanjaro zote zinafikika kwa gari na lami imeunganisha sehemu zote muhimu labda useme lami hazipo kwenye hizo chochoro za kuunganisha kijiji kimoja kwenda kingine ambazo ndio wanaziweka kokoto tu.
Wilaya zote safi ila ndani hapana sio sehemu zote labda Machame na Rombo
 
Nawe acha uongo, wivu na uzushi.
Wewe umeambiwa hicho ni kijiji kimoja huko Kilimanjaro, tena hamasa imeanzia kanisani, na wanafanya ukarabati wa zaidi ya km 72 za barabara.
Sasa ya Mwanza yametokea wapi?
Kuna kijiji gani huko Mwanza wananchi wamefanya hivyo?
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wapi ametajwa kuhusika?

Jifunze kuwa mkweli na muungwano. Toa hongera kwa wachaga na wakristo wa kijiji cha kiruweni huko Kilimanjaro kwa kuonyesha njia.
 
Wilaya zote safi ila ndani hapana sio sehemu zote labda Machame na Rombo
Kilimanjaro naijua yote vizuri rombo barabara ya mkato ya kenya ikipata lami itakua imezungukwa na lami pande zote , marangu ila lami pande zote mpaka vichochoroni , barabara ya kilema kanisa la katholic ,panda barabara ya hospitality ya marangu njoo barabara ya shule ya Uchira unganisha mpka mwika zungukia himo kote kumewekwa kati na lami .

Panda barabara ya kcmc katisha rau mpka mamboleo panda juu barabara zote za v ya kwend uru mnini na uru kishumundu zote zina lami .

Banda barabara zote za kwenda kibosho umbwe , kibosho kirima ,kibosho singachina mpka mweka zote zina lami .


Katisha barabara ya kwenda masama panda juu mpka soko la mula katika kona ya kwenda machame kwa juu barabara ya masama secondary tokea machame msikitini ,panda juu mpaka machame hospital ,shuka chini mpaka nshara kwa mbowe , kata chochoro ya kwnda narumu tokezea barabara ya kibosho umbwe kote kuna lami .
 
Wapi gov wamefanya vitu vingi at once na vikaenda sawa? Suala la kuwa wanatumia pesa vibaya hilo kila mtu anasema but ni kiasi gani has no body knows? Can you prove it ?
 
Watu wenye akili kubwa tumekuja hapa kupongeza hili kwa sababu kuu tatu.
1. Hatua hiyo inawafanya wananchi hao kuwa na nguvu juu ya maamuzi ya maendeleo hao. Hakuna kitu au mtu wakuweza kuwababaisha.

2. Hatua hiyo inalazimisha maendeleo mengine kuwafuata. Kesho na keshokutwa serikali itajikuta kwa lazima inaboresha na mengine. (Penye nia pana njia, mwenye nacho ataongezewa)

3. Wananchi hao wamedhamiria kuwa na maisha bora kwa gharama zote. Lazima watafika mbali zaidi.
 
Hao wananchi wana nia ya dhati na ni mfano wa kuigwa kabisa.
 
Uongo wanini? Nimekwambia mmechelewa sana, Mwanza wameanza zamani sana, tena kiwango cha mawe, unabisha hilo nikuwekee ushahidi?
 
Uongo wanini? Nimekwambia mmechelewa sana, Mwanza wameanza zamani sana, tena kiwango cha mawe, unabisha hilo nikuwekee ushahidi?
Mkoa wa kwanza Tanzania kupata lami ni dar es salam unaofuati ni kilimanjaro 1960 na harakati za wanakimanjaro kujipambania zilianza zaman mno kipindi cha KNCU 1933
 
Otanenyi wameeku wa Kiruwenyi na papa Mlisi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…