Pre GE2025 Wananchi wa Kilimanjaro wachangishana kurekebisha barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 72

Pre GE2025 Wananchi wa Kilimanjaro wachangishana kurekebisha barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 72

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jukumu la serikali kwa wananchi ni maeneo mengi saana, mfano, amani, ajira, kupandisha madaraja watumishi, kujenga vituo vya afya na kusambaza huduma mbalimbali katika jamiii, kama vile umeme shule n.k, n.k
Tofauti iko wapi kati ya mambo ambayo wananchi wanawajibika “kujiletea maendeleo wenyewe” na hayo majukumu ya serikali?

Kubwa zaidi, uhusiano kati ya wananchi na serikali yao unatakiwa kuwaje?
 
Binafsi napongeza juhudi hizo! Natamani mikoa yote Tanzania iige hivyo.
Hapa sasa Serikali ambacho ingefanya ni kuwaunga mkono kwa kumalizia na rami.
Hapa Dar kama wakazi wangefunguka wakaiga mfano huo kusingekuwa na vilio vya barabara wakati wa mvua!
Kodi na mikopo zinaenda wapi?
 
Nakwambia hao jamaa wa huko Kilimanjaro ni akili kubwa sana, ungewaelewa usiandike hayo.
Kukupa mwanga tu, issue iko hivi. Serikali ni watu, na ukitaka kuwawin wasome walivyo na wanavyofanya mambo yao. Hao wachaga baada ya kujichangisha pesa walienda TARURA, na huko TARURA kwa aibu ikabidi waunge mkono juhudi zao! Wewe endelea kusubiri serikali ikulteee maendeleo tu.
Sorry, hukunielewa kabisa. Sijahoji uzuri au ubaya wa walichofanya hao wananchi.
 
Changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara katika eneo la Kiruweni, Kata ya Mwika Kusini, Wilaya ya Moshi, imewalazimu wananchi wa eneo hilo waishio maeneo mbalimbali nchini kuchangishana fedha na kuanza ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 72 kwa kiwango cha changarawe.

Eneo hilo ambalo wananchi wake wanajishughulisha na uzalishaji wa ndizi na kilimo cha mazao mbalimbali, limekuwa na changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara.

Hali hii imewalazimisha kusafirisha mizigo kwa kichwa hadi sokoni, hivyo kushindwa kufikia ndoto zao za kujikwamua kiuchumi.

Chimbuko la wazo la ujenzi wa barabara lilianzia katika Usharika wa Kiruweni wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), baada ya mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa Machi na Aprili, 2024.

Mvua hizo zimesababisha barabara hizo zishindwe kupitika kwa vyombo vya usafiri, zikiwamo pikipiki.

Akizungumza kuhusu ujenzi huo, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kiruweni, Joram Mamuya amesema barabara hizo zimefikia hatua mbaya na kufanya wananchi kushindwa kutumia vyombo vya usafiri na hivyo kulazimika kubeba mazao yao kichwani kuyapeleka sokoni, huku wakitembea umbali mrefu.
Watafanya nini sasa?!

Mama yupo busy na wasanii KOREA?

Yuko busy kuuza Maliasi na Rasilimali za nchi! Pesa zenyewe hatuzioni?!

Kutwa kusema #royaltuors inaleta $! Ziko wapi!

Kutwa kubadilisha wanaoharibu, kuiba na kuvurunda na kuwapachika sehemu nyingine tena?!

Kutwa yeye na mpango kudai upendo na amani! Huku wakimzidi VASCO DA GAMA!

Kutwa mipasho na kudai yeye ni (chura kiziwi) huku gharama za maisha zikipanda huku wao wakiponda hela za umma kwa kujilinda, kula Bata, kujilimbikizia mali na kudai tuna maisha bora?!
 
Tofauti iko wapi kati ya mambo ambayo wananchi wanawajibika “kujiletea maendeleo wenyewe” na hayo majukumu ya serikali?

Kubwa zaidi, uhusiano kati ya wananchi na serikali yao unatakiwa kuwaje?
Kodi yako wewe mwannchi inalipa mishahara ya watumishi wa umaa wanaotuhudumia
 
Excellent!

Wrong!
Wilaya ya Mwanga ipo milimani ' Ugweno na Usangi' ambako kuna population kubwa sana na shughuli nyingi sana. Hospitali ya Wilaya ipo Usangi. Shule nyingi za sekondari zipo milimani. Kumbuka kuna kilimo cha ndizi, kahawa, Iliki n.k. Kwa ufupi pale Mwanga unapopaona ni kwasababu ya ''convinience'
Lami kwenda Ugweno na Usangi si upendeleo ni kwasababu ya shughuli za kiuchumi za Wilaya.

Wilaya ya Mwanga pale barabarani ni Lami ya barabara kuu hakuna kitu kingine.
Nimekueleza kwamba Wilaya imewekwa pale Mwanga ili kupunguza umbali na watu wa Bondeni kuanzia Nyumba ya Mungu, kuja Lembeni hadi Same na watu kutoka Lake Jipe hadi Njia panda.

Wilaya ilipaswa kuwa katika maungano ya Usangi na Ugweno lakini pia walizingatia maeneo ya Bondeni ikaamuliwa ijengwe pale Barabara kuu ya Moshi-Arusha

Kuhusu Same, ni Wilaya iliyodumaa kwasababu tangu Mkoloni imekuwa Wilaya na Boma.
Harakati za kupinga kodi '' Kodi ya Mbiru' dhidi ya Wajerumani ilifanyika Boma Same wakati huo ikiwa pamoja na Mwanga. Kwahiyo haikutakiwa iwe kama ilivyo. Same ni sawa na Korogwe , Wilaya Kongwe sana nchini zilizodumaa. Tukipata Uhuru Korogwe ilikuwa ''Town council''
Kuhusu Usangi na Ugweno kuwa na shughuli nyingi za kichumi au population kubwa kwa wilaya ya Mwanga hiyo kitu HAPANA, na sio sahihi kwa 100%. Nitakujibu kitakwimu hapa kutumia takwimu za serikali.

1. Ugweno na Usangi ni tarafa mbili tu, wakati wilaya ya Mwanga ina tarafa tano. Tarafa zingine ni Jipendea, Mwanga na Lembeni.

2. Wilaya ina jumla ya kata 19 (wakati Ugweno na Usangi kuna kata 8), hivyo kata nyingi haziko milimani.

3. Wilaya kwa sasa ina idadi ya watu inayofikia 148,000, na waliopo Ugweno na Usangi ni pungufu ya watu 40,000/=. Hivi huwezi tena kuwa na shule nyingi, maana wanafunzi watatoka wapi? Hata shule za private tunaelezwa nyingi zimekufa au kudorora mnoo (kuanzia sijui minja, shighatini, Kiriki, Lomwe, Usangi girls), vyuo vilishakufa kama chuo cha ualimu usangi, chuo cha ufundi usangi nk.

4. Hakuna kahawa wala ndizi zinazolimwa kibiashara kutoka huko milimani (Usangi na Ugweno), imebakia migomba ya ndizi za chakula nyumbani. Kahawa na ndizi sio zao la biashara kwa wilaya Mwanga. Kahawa ni historia, ndizi ni chakula.

5. Uchumi wa wilaya ya mwanga unategemea hizi shughuli, na hizi shughuli kwa 99% hazipo kabisa Usangi na ugweno.
-Uvuvi wa samaki wa bwawa la nyumba ya Mungu, ambalo liko tambarare
-Mifugo (hawa ni wamasai waliopo tambarare)
-Biashara za mijini (Maduka, hoteli, migahawa, bars, vituo vya mafuta, mabenki) ambazo kwa zaidi ya 90% ziko Mwanga mjini.
-Machimbo ya mchanga.

Hata Hospitali kubwa ya wilaya kwa sasa nasikia imejengwa Mwanga mjini.

Narudia kuandika hapa, zile barabara za lami na zile taa za kisasa za usiku barabarani kule milimani zimewekwa kisiasa tu, kwa ushawishi na heshima ya wale wazee na mabregadia waliowahi kuendesha hii nchi na sio kwa sababu nyingine yoyote. It is for loyal and pride.
 
ila tuendako pagumu,bajeti ya tanroad imepita ila inadaiwa na italipa madeni na itabakia 500 bil tu,watajenga nini mwaka wa 2024/2025?
 
Hawa jamaa wako tofauti sana na jamii zingine

Kuna siku nilisema mnashindwa hata kuondoa takataka zenu na mitaro iliyojaa maji machafu na harufu
Nilishambuliwa sana na baadhi ya watu

Kwa nchi masikini kuna wakati mnajiongeza maana unaweza kukuta kuna hela zilitengwa ila zimepigwa zote
Sasa utasubiri sana
 
Kuhusu Usangi na Ugweno kuwa na shughuli nyingi za kichumi au population kubwa kwa wilaya ya Mwanga hiyo kitu HAPANA, na sio sahihi kwa 100%. Nitakujibu kitakwimu hapa kutumia takwimu za serikali.

1. Ugweno na Usangi ni tarafa mbili tu, wakati wilaya ya Mwanga ina tarafa tano. Tarafa zingine ni Jipendea, Mwanga na Lembeni.
Population! milimani ni Ugweno na Usangi ni densely populated.
2. Wilaya ina jumla ya kata 19 (wakati Ugweno na Usangi kuna kata 8), hivyo kata nyingi haziko milimani.
Kata zinatengwa 'for admin activities'' . Hivi kwa mfano, unalinganisha vipi kata ya Lembeni na Ugweno? au Mpendae na Usangi? Kuna kitu una miss hapa. Maeneo ya Mwanga, Same, Rombo na Hai nayafahamu vizuri sana si kupita barabarani
3. Wilaya kwa sasa ina idadi ya watu inayofikia 148,000, na waliopo Ugweno na Usangi ni pungufu ya watu 40,000/=. Hivi huwezi tena kuwa na shule nyingi, maana wanafunzi watatoka wapi? Hata shule za private tunaelezwa nyingi zimekufa au kudorora mnoo (kuanzia sijui minja, shighatini, Kiriki, Lomwe, Usangi girls), vyuo vilishakufa kama chuo cha ualimu usangi, chuo cha ufundi usangi nk.
Wakazi wa Ugweno na Usangi wameondoka wapo mijini. Mfano, Arusha, Moshi, Tanga , Dar es Salaam na kwingineko. Hao unaosema ni Familia hasa za Wazee . Trust me, hebu temebelea nyakati za shughuli za kidini iwe Eid au Krismas uone population unayoelekea huko.

Tena Wachaga wanasingiziwa sana nyakati kama za Krismas, ukweli ni kuwa wanaokwenda Kilimanjaro ni Wachaga na Wapare, kwa uelewa kidogo watu wanadhani kila wa K'Njaro ni Mchaga

Kigezo cha population si kweli

4. Hakuna kahawa wala ndizi zinazolimwa kibiashara kutoka huko milimani (Usangi na Ugweno), imebakia migomba ya ndizi za chakula nyumbani. Kahawa na ndizi sio zao la biashara kwa wilaya Mwanga. Kahawa ni historia, ndizi ni chakula.
Pengine si kwa kiwango cha zamani lakini zipo shughuli, temmbelea magulio ya Mwanga, Njia panda hata Moshi uone bidhaa za milimani.
5. Uchumi wa wilaya ya mwanga unategemea hizi shughuli, na hizi shughuli kwa 99% hazipo kabisa Usangi na ugweno.
-Uvuvi wa samaki wa bwawa la nyumba ya Mungu, ambalo liko tambarare
Si kweli, kuna samaki kiasi gani kutoka Nyumba ya Mungu katika kiwango cha uchumi?
-Mifugo (hawa ni wamasai waliopo tambarare)
Hawa wanahama baina ya Wilaya huwezi kusema ni wakazi wa Mwanga. Wengine hufuata malisho Simanjiro, Mkomazi , Same hata Gonja. Naelewa haya kwa uzoefu si kusoma
-Biashara za mijini (Maduka, hoteli, migahawa, bars, vituo vya mafuta, mabenki) ambazo kwa zaidi ya 90% ziko Mwanga mjini.. Machimbo ya mchanga.
Yes zimejengwa Wilayani lakini jiulize wateja wanatoka wapi? Ukikata mawasiliano na Milimani ' Ugweno na Usangi'' hakuna Wilaya ya Mwanga! nitty gritty!
Hata Hospitali kubwa ya wilaya kwa sasa nasikia imejengwa Mwanga mjini.
Haiondoi ukweli kwamba Hospitali ya Wilaya ipo Usangi. Hii imekuwepo kama Gov Hospitali kuanzia zama za mkoloni. Kujenga Bondeni ni kurahisha huduma kwa watu wa Bondeni kwasababu Mwanga ni kati kati.
Narudia kuandika hapa, zile barabara za lami na zile taa za kisasa za usiku barabarani kule milimani zimewekwa kisiasa tu, kwa ushawishi na heshima ya wale wazee na mabregadia waliowahi kuendesha hii nchi na sio kwa sababu nyingine yoyote. It is for loyal and pride.
Hakuna taa za barabarani, unachokiona ni taa za makazi ya Watu.
Wape maua yao, katika Wilaya ya Mwanga hasa Ugweno na Usangi kitu kinachoitwa nyumba ya nyasi ni kwa ajili ya mifugo. Wapeni maua yao, wale watu wamejitahidi kujiletea maendeleo

Hizo barabara za lami unazosema zimejengwa na Wananchi si serikali. Kilichofanyika ni kuweka lami l
Nyerere akidai uhuru alikuja na kukuta watu wanajenga barabara zao tena miaka zaidi ya 40 kabal ya Uhuru kwa kutumia Machifu wao wa Ugweno na Usangi. Msaragambo!
 
Population! milimani ni Ugweno na Usangi ni densely populated.

Kata zinatengwa 'for admin activities'' . Hivi kwa mfano, unalinganisha vipi kata ya Lembeni na Ugweno? au Mpendae na Usangi? Kuna kitu una miss hapa. Maeneo ya Mwanga, Same, Rombo na Hai nayafahamu vizuri sana si kupita barabarani

Wakazi wa Ugweno na Usangi wameondoka wapo mijini. Mfano, Arusha, Moshi, Tanga , Dar es Salaam na kwingineko. Hao unaosema ni Familia hasa za Wazee . Trust me, hebu temebelea nyakati za shughuli za kidini iwe Eid au Krismas uone population unayoelekea huko.

Tena Wachaga wanasingiziwa sana nyakati kama za Krismas, ukweli ni kuwa wanaokwenda Kilimanjaro ni Wachaga na Wapare, kwa uelewa kidogo watu wanadhani kila wa K'Njaro ni Mchaga

Kigezo cha population si kweli

Pengine si kwa kiwango cha zamani lakini zipo shughuli, temmbelea magulio ya Mwanga, Njia panda hata Moshi uone bidhaa za milimani.

Si kweli, kuna samaki kiasi gani kutoka Nyumba ya Mungu katika kiwango cha uchumi?

Hawa wanahama baina ya Wilaya huwezi kusema ni wakazi wa Mwanga. Wengine hufuata malisho Simanjiro, Mkomazi , Same hata Gonja. Naelewa haya kwa uzoefu si kusoma

Yes zimejengwa Wilayani lakini jiulize wateja wanatoka wapi? Ukikata mawasiliano na Milimani ' Ugweno na Usangi'' hakuna Wilaya ya Mwanga! nitty gritty!

Haiondoi ukweli kwamba Hospitali ya Wilaya ipo Usangi. Hii imekuwepo kama Gov Hospitali kuanzia zama za mkoloni. Kujenga Bondeni ni kurahisha huduma kwa watu wa Bondeni kwasababu Mwanga ni kati kati.

Hakuna taa za barabarani, unachokiona ni taa za makazi ya Watu.
Wape maua yao, katika Wilaya ya Mwanga hasa Ugweno na Usangi kitu kinachoitwa nyumba ya nyasi ni kwa ajili ya mifugo. Wapeni maua yao, wale watu wamejitahidi kujiletea maendeleo

Hizo barabara za lami unazosema zimejengwa na Wananchi si serikali. Kilichofanyika ni kuweka lami l
Nyerere akidai uhuru alikuja na kukuta watu wanajenga barabara zao tena miaka zaidi ya 40 kabal ya Uhuru kwa kutumia Machifu wao wa Ugweno na Usangi. Msaragambo!
Kuwa mkweli.
Ukiondoa eneo la Mwanga mjini na Nyumba ya Mungu, wilaya ya mwanga kiuchumi na kiidadi ya watu linapotea kwa zaidi ya 70%. Mwanga inabebwa na Mwanga mjini (kwa sababu idadi ya watu wahamiaji inaongeza, shughuli za serikali, kupitiwa na barabara kuu ya Dar-Moshi, shughuli za ujenzi zinakuwa kwa kasi na biashara zinakuwa) eneo linalofuata ni Nyumba ya Mungu sababu ya uwepo wa bwawa, lile bwawa ni kubwa mnoo, uvivu umevuta watu huku zaidi ya 60% ya samaki za maji baridi zinazouzwa Kilimanjaro (hususani Moshi mjini) na Arusha mjini zinatokea nyumba ya Mungu. Usangi na Ugweno kumebakia loyal na Pride kwa wenyeji, na idadi ya watu imepungua mnooooo. Vijana wamekimbilia mjini na hawarudi tena, wazee wengi wamekufa, nyumba nyingi zimefungwa, wenyeji wanarudi sikukuu tu na kwenye misiba, na watu hawazaliani kabisa!. Leo hii, idadi ya juu kabisa ya shule moja kuandikisha watoto wa darasa la kwanza kwa maeneo ya usangi au ugweno labda ni watoto 10 kwa mwaka, wakati miaka 20 nyuma ilikuwa sio chini ya 50. Hali ni hiyo hiyo Makanisani na kwa sehemu misikitini, waumini wamepungua mnoo huko milimani wakati tambarare wamezidi kuongeza. Hakuna watu, hakuna shughuli, hakuna pesa.

Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami, hakuna wananchi waliwahi kujenga hata robo kilometa, lami yote imejengwa kwa pesa za serikali kwa 100%. Na hii ni nchi nzima. Barabara za lami zinajengwa na serikali tu unless hiyo barabara isiwe ya umma, iwe barabara ndani ya eneo lako maalum.
 
Ni hivi Nyerere alikwenda kudai Uhuru na alihutubia Usangi na Ugweno. Mwl alikwenda kwa gari akipita juu ya barabara iliyojengwa kwa nguvu za Wananchi kwa njia ya Msaragambo miaka mingi kabla ya Uhuru.
Barabara kutoka Mwanga ilijengwa kwa njia ya kujitolea watu wakiongozwa na Machifu wao

Kuna tatizo gani kuweka lami juu ya barabara iliyojengwa na Wananchi kabla ya Uhuru?

nimetembea sana hii nchi, tunawaonea wivu tu wakazi wa K'njaro, waliwekeza katika maendeleo yao

Barabara imejengwa CD Msuya hajazaliwa lakini utasikia alijenga yeye! Tuwape maua yao Wananchi wa Kilimanjaro. Hao Kiruweni mi mfano tu!
 
..asilimia 60% ya mkoa wa Kilimanjaro ni wilaya za Same na Mwanga. Je, hali ya maeneo hayo kimiundombinu ikoje?
Ipo kama Ulaya, KNCU walianza kujijengea wenyewe barabara kabla ya uhuru.

Hivyo ndivyo wanavyojidanganya.
 
Ni hivi Nyerere alikwenda kudai Uhuru na alihutubia Usangi na Ugweno. Mwl alikwenda kwa gari akipita juu ya barabara iliyojengwa kwa nguvu za Wananchi kwa njia ya Msaragambo miaka mingi kabla ya Uhuru.
Barabara kutoka Mwanga ilijengwa kwa njia ya kujitolea watu wakiongozwa na Machifu wao

Kuna tatizo gani kuweka lami juu ya barabara iliyojengwa na Wananchi kabla ya Uhuru?

nimetembea sana hii nchi, tunawaonea wivu tu wakazi wa K'njaro, waliwekeza katika maendeleo yao

Barabara imejengwa CD Msuya hajazaliwa lakini utasikia alijenga yeye! Tuwape maua yao Wananchi wa Kilimanjaro. Hao Kiruweni mi mfano tu!
Kuwa "mkweli", wachaga walijenga barabara huko kabla hata ya Mjerumani kuja.
 
Ipo kama Ulaya, KNCU walianza kujijengea wenyewe barabara kabla ya uhuru.

Hivyo ndivyo wanavyojidanganya.

..mnaojidanganya ni nyinyi mnaoamini kwamba miundombinu yote ya Kilimanjaro imejengwa na serikali baada ya uhuru.

..wilaya ya Same walikuwa na utaratibu wa wananchi kujitolea kufanya kazi za maendeleo unaitwa " msaragambo. "

..Uchimbaji wa barabara ya Same-Vudee kwa nguvu za wananchi ulimshangaza Mwalimu Nyerere mpaka akawapa jina wana Same kuwa ni " wachina wa Tanzania. "
 
Back
Top Bottom