Wananchi wa Tanzania tunakupongeza Rais Samia kwa mazuri unayoyatenda

Wananchi wa Tanzania tunakupongeza Rais Samia kwa mazuri unayoyatenda

Biashara ya sasa sio lazima kuwa na stock, biashara ya sasa sio lazima kuwa na fremu, kusafirisha mizigo ya watu sio lazima kuwa na gari nk, nk, dunia imebadirika.
ulivyovitaja vyote ni sharti viambatane sambamba kama pete na kidole vinginevyo hakuna bilashaka 🐒
 
Huyo mama Samia amedhihirisha inawezekana kwa kina mama kutawala kwa amani na wakafanikisha, inapaswa Wakenya tukaiga pia.
 
SI MPANGO WA MUNGU MWANAMKE KUWA KICHWA( HEAD OF STATE) WALIUMBWA WAWE WASAIDIZIIII...

NI AJABU,AIBU NA KINYUME NA MAPENZI YA MUNGU MTAWALA KUWA MWANAMKE HATA KAMA ANAYO AKILI KIASI GANI.

MWANAUME MZIMA ETI ANASIFIA KUONGOZWA NA MWANAMKE NA ANACHAGUA HIVYO NA KUFURAHIA.

MWANAUME WAHIVYO ANASTAHILI KUOLEWAA,TUACHE UMARIOO WANAUME TUSIMAME PANAPOSTAHILI NA WASAIDIZI WETU WASHIKE VYEO VYA CHINI YETU.
 
Mie nampongeza kwa kuimarisha ufisadi serikalini, kwa mdomo wake amekiri kuna mirija ya wizi kwenye serikali yake!
 
Huyo mama Samia amedhihirisha inawezekana kwa kina mama kutawala kwa amani na wakafanikisha, inapaswa Wakenya tukaiga pia.
Msithubutu, wanawake ni ngumu sn kutawala huku afrika...waishie kwenye uwaziri tuu.
Huyu wetu anaogopa kuyachukulia maamuzi magumu baadhi ya midume sijui anaona watampa talaka?!
 
Ningekuwa mshauri wa Mungu ningeshauri tukuchape viboko
Wananchi wa Tanzania tunakupongeza kwa mazuri ambayo unayatenda. Usikatishwe tamaa na kelele sisi tulioishi muda mrefu na kujua mwenendo wa nchi tunakuona unaenda vyema sana. Furaha, amani, mshikamano miongoni mwa watanzania ni wa hali ya juu.

Uhuru wa kuabudu, uhuru wa kutoa maoni, hata uhuru wa kutukana viongozi pia upo juu sana.....labda wale wanaopitiliza kutukana hata shetani mwenyewe anashangaa. Lakini matusi ya reja reja watu wanatukana tu kwa raha zao. Usalama pia ni mkubwa, hakuna wasiwasi wa ujambazi, ugaidi wala utekaji.

Serikali inalipa madeni ya ndani, madai ya malipo, hakuna kukatwa deni, sijui kuhakikiwa deni. Pia huna wasiwasi kuwa fedha ikiingia kwenye akaunti utakuta imechukuliwa au kupunguzwa. TRA wamekuwa wakifanya kazi kwa weledi na very friendly, wanatuma meseji kila mara kukumbusha wajibu wa kulipa kodi.

Ndugu zetu CHADEMA wanajimwaga kwa raha zao na maandamano; hakuna anayewabughudhi kwamba wawe na term limit kwa Mwenyekiti wao.

Naona Sam Nujoma rd na Old Bagamoyo rd unataka kufanya jambo jipya........

Hongera sana Rais
 
Back
Top Bottom