Wananchi wa Ubelgiji waandamana kupinga kufungiwa ndani, CHADEMA mnaweza kujifunza kitu huko!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nafahamu kwamba makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lissu kwa sasa anaishi Ubelgiji.

Kupitia taarifa ya habari ya Al jazeera wameonekana wananchi wa Ubelgiji wazungu na wale wenye asili ya Afrika na Asia wakiandamana kupinga kufungiwa ndani.

Wanadai kwamba Lockdown ni mateso kupita Corona yenyewe.

Nimeona niwaleteeni hili bandiko makamanda wa Chadema mpate kutafakari na hata kufuatilia kama " Ni yeye " aliandamana.

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nchi za Afrika waliokuwa wakikiuka masharti ya lockdown na mengine hususani uvaaji wa barakola na social distancing, walikuwa wanatwangwa risasi za moto. Je, huko Ubeligiji hawajaanza kuwatwanga watu hao? Lissu atapona kweli au huko kashika adabu?
 
Hivi kila anayekosoa mwenendo wa Serikali ni CHADEMA au UPINZANI, kwanini hamtaki kuamini kwamba wapo raia wasio na itikadi yoyote na hawapendezwi na baadhi ya mambo ya hovyo, hivyo ni haki yao kusema.

Halafu CHADEMA si munasema imekufa mbona bado naona kama watu wanatapatapa.
 
Lini chademaa wamesema serikali ifungie watu ndani. Unafungiaje watu ndani wakati chanjo imeshapatkana? Serikali ikanunue chanjo bhna
 
Hivi kila anayekosoa mwenendo wa Serikali ni CHADEMA au UPINZANI, kwanini hamtaki kuamini kwamba wapo raia wasio na itikadi yoyote na hawapendezwi na baadhi ya mambo ya hovyo, hivyo ni haki yao kusema.
Halafu CDM si munasema imekufa mbona bado naona kama watu wanatapatapa.
na pengine wapo hata hao CCM wengine hukosoa pia
 
Nafahamu kwamba makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lissu kwa sasa anaishi Ubelgiji.

Kupitia taarifa ya habari ya Al jazeera wameonekana wananchi wa Ubelgiji wazungu na wale wenye asili ya Afrika na Asia wakiandamana kupinga kufungiwa ndani.

Wanadai kwamba Lockdown ni mateso kupita Corona yenyewe.

Nimeona niwaleteeni hili bandiko makamanda wa Chadema mpate kutafakari na hata kufuatilia kama " Ni yeye " aliandamana.

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Na tundulissu yumo kwenye maandamano ?
 
Hivi kila anayekosoa mwenendo wa Serikali ni CHADEMA au UPINZANI, kwanini hamtaki kuamini kwamba wapo raia wasio na itikadi yoyote na hawapendezwi na baadhi ya mambo ya hovyo, hivyo ni haki yao kusema.
Halafu CDM si munasema imekufa mbona bado naona kama watu wanatapatapa.
Na mambo "ya hovyo" yenyewe ni Rais kukataa kuwafungia watanzania lockdown??

Mwilini mwako kuna funza anatafuna katika kiungo pasipo salama

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom