KERO Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa tunakumbana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi

KERO Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa tunakumbana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa tunakumbana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi. Kwa sasa, maji yanapatikana mara moja tu kwa wiki, na hata yanapopatikana hutoka kwa saa chache pekee, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi katika shughuli zetu za kila siku.

Tunaomba Mamlaka ya Maji ya Wilaya ya Ruangwa itoe ufafanuzi kuhusu sababu za hali hii na, ikiwa upungufu wa maji hauwezi kuepukika kwa sasa, basi itangaze ratiba rasmi ya mgao wa maji.

Ratiba hiyo itawawezesha wananchi kupanga matumizi yao na kupunguza athari zinazotokana na ukosefu wa maji.
 
Mgao wa maji ya wilaya ya RUANGWA haipo sawa tunakaa wiki mbili mzima bila ya maji maeneo ya kulimani hewa kuelekea halmashauri hivyo tunaomba kama kuna ratiba ya mgao wa maji ifuatwe na maji yatoke kwa siku mzima sio masaa tu halafu yanakatwa inakera
 
Back
Top Bottom