Wananchi wahimizwa kujifunza kutumia mfumo wa e-ARDHI

Wananchi wahimizwa kujifunza kutumia mfumo wa e-ARDHI

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
5622a6ff-fe09-4a31-872f-1190d0efa94d.jpeg


SINGIDA

Wataalamu wa sekta ya ardhi Mkoa wa Singida wakiambatana na wale wa kutoka Makao makuu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wametoa elimu kuhusu matumizi ya mfumo wa e-Ardhi na kuhimiza wananchi kujifunza na kutumia mfumo huo kwa usahihi.

Elimu hiyo imetolewa leo Septemba 18, 2026 kupitia kituo cha redio cha Standard (Standard Radio), ikiwa na lengo la kujenga uelewa kwa wananchi wa namna ya kutumia mfumo huo katika kupata huduma za ardhi kwa urahisi na kwa wakati.

Wataalamu hao wameeleza kuwa, kupitia mfumo wa e-Ardhi, wananchi wanaweza kufuatilia na kupata baadhi ya huduma za ardhi bila kulazimika kufika mara kwa mara katika ofisi za ardhi.

Aidha, wananchi wametakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo watakutana na changamoto katika matumizi ya mfumo huo wakati wa kupata huduma.

Mfumo wa e-Ardhi umeundwa kuwezesha huduma mbalimbali za ardhi kutolewa kwa njia ya kidijitali, ikiwemo uwasilishaji na ufuatiliaji wa maombi, usimamizi wa taarifa za ardhi pamoja na kurahisisha upatikanaji huduma kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom