Wananchi wahoji kulikoni awamu ya 3, ya 4 na ya 5 hakukuwa na kesi za Uhaini, Kulikoni awamu ya 6?

Wananchi wahoji kulikoni awamu ya 3, ya 4 na ya 5 hakukuwa na kesi za Uhaini, Kulikoni awamu ya 6?

Wananchi wengi wanahoji sasa kwamba ilikuwaje katika awamu ya 3, ya 4 na ya 5, ambazo zote hizi zilikuwa na Vyama vya Upinzani hakukuwahi kuwa na kesi za Uhaini?

View attachment 3299580

Why Awamu ya 6 itengeneze kesi ya Ugaidi ya Mbowe na sasa imetengeneza hii ya Uhaini ya Tundu Lissu?

Uchunguzi wetu umebaini kwamba Marais wote wa awamu hizo walitokea Tanganyika, Je hawakuwa na uwezo wa Intelijensia ya kuwaona Magaidi na Wahaini kama huyu aliyepo sasa ambaye anatokea upande wa pili?

Karibuni kwa Mjadala
Acha kabisa kuisemea Awamu ya Tano.
 
...ulianza na mungu...sasa umeenda kwenye milipuko?

...unahatarisha usalama wa taifa la Tanzania kwa uchochezi wa uasi.

=======™
...nilisha tahadharisha kuhusu CHADEMA kupokea na kukumbatia siasa za mungu wenu😌

Kanuni ya dhahabu iko wazi ,lile usilopenda kufanyiwa wewe nasi usimfanyie ,mwenzako .

Tangu mfumo wa vyama vingi umeanzishwa ni Kada yupi wa CCM amewahi kufikishwa hata polisi kwa sababu ya jinai aliyoifanya wakati wa ^chaguzi iwe ni kuua au kuteka au kupiga au hata kutoa lugha ya matusi au kuzidisha hata muda kwenye kampeni ?

Ni nani Kada au Chawa wa CCM uliwahi kumsikia amekamatwa kwa kutumia mitandao kuwatukana viongozi wa dini ,wanaharakati na Wapinzani ?

Walisema hadharani kuwa watawapoteza wapinzani , wakasema hadharani kuwa wataiba kura ,wakasema hadharani kuwa ushindi ni lazima hata kura zipigwe kwa wapinzani atakayetangazwa ni wa CCM ?

Sasa huyo Mungu wako yupo upande upi au ndio ameumba binadamu waishi kwama Simba na Swala wakati wote ni binadamu wenye akili timamu ?

Wenzetu waalishavuka huko kwenye siasa za kuuana wenyewe kwa wenyewe wamebaki kwenye vita vya kiuchumi tena nje ya nchi zao . Sisi mpaka rasilimali zetu hatuna habari ya kuzilinda tunakinda madaraka ya kakundi ka watu wachache bila kujiuliza watu mil.65 miaka 50 ijayo wajukuu wao wataishi vipi bila ardhi na rasilimali zinazomilikiwa na wazawa ambao ndio ndugu zao na serikali yao itakua ina nguvu gani kama watu wachache ndio watakaokuwa wana nguvu kubwa ya kisiasa kiuchumi bila Mifumo yenye kutenda haki .
Tutakua kama Colombia . Wauza madawa walikua wanaweka viongozi mpaka wakuu wa idara na vyombo vyote vya dola na aliyekua kinyume nao walimuondoa haraka haraka .

Hatuwezi kuwa na nchi kama hiyo kisa tu tukisema tutaambiwa tunachanganya dini na siasa.
Watu wote na dini zote wanapenda kutendewa haki.
Hakuna watu wakorofi wanapokamatwa na polisi kama wanaCCM hata kama wametenda Jinai .
Yaani hata kama ameua mtu kwa Ditopile bado atakua mbishi na atasaidiwa . Kada wa CCM akigonga mtu na gari anaonekana kama amekanyaga paka tu .Kila mbinu itatumika kuonyesha kuwa hakufanya kosa .
Hapana , kama kuna Imani,itikadi, falsafa,chama ,kikundi au hata imani ya mizimu inayobaguwa na kunyanyasa watu kwa kiwango hicho hiyo ni Imani mbaya sana .
 
Inasikitisha sana.

Anyway, JPM alisingiziwa mabaya mengi sana 😎
 
Back
Top Bottom