GE2025 Wananchi wakutana kushangilia kifo cha Ndugai!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Tumuombee KIFO sio adhabu bali ni haki ya kila kiumbe
 
Nimesikitishwa na kutishika na video hizi zinazodaiwa kuwa za Wananchi jimboni kwa Job Ndugai wakishangilia kifo chake

View attachment 3434487
Hii mbegu iliyopandwa kwenye mioyo ya wananchi inazidi kukua tunakokwenda tusishangae ukitokea msiba mkubwa zaidi wanachi wakiandamana nchi nzima kusherekea!
Hii sio kitu kizuri lakini inapaswa viongozi wenye dhamana wabadirike Waache kuwaumiza wananchi hii chuki imesababishwa na mwenendo wa kiongozi husika alipokuwa madarakani
 
Huyo wa msoga, nadhani watu watapika na pilau.

Japo kifo sio adhabu, ni tundu ambalo, wema na wabaya watapitia.
 
Inasikitisha sana, hao viongozi wenyewe hawashtushwi na mauaji yanayoendelea nchini, wacha wavune walichopanda.
 
Hongereni wananchi
 
Maisha haya,Mariam Ditopile nilisoma nae advance.Wanakondoa hawamtaki.
 
Mungu afanyi kazi Kwa hisia .we muombee mabaya yeye atazid kushine
 
Nimesikitishwa na kutishika na video hizi zinazodaiwa kuwa za Wananchi jimboni kwa Job Ndugai wakishangilia kifo chake

View attachment 3434487
Plato alisema, jamii yoyote yenye matabaka, migogoro haikwepi.

Kwa Tanzania hali inazidi kuwa mbaya kuhusu chuki kati ya maskini na matajiri kwa sababu maskini wanahisi matajiri wanawaibia rasilimali na kula keki ya taifa peke yao.

Sijafika huko lakini nahisi nchi zilizoendelea hakuna chuki kama hizi kwa sababu labda maskini katika nchi wanapewa huduma za msingi nzuri mfano shule, afya, miundombinu nk.
 
Hawa watu wanaweza kua wametengenezwa kwasababu flani flani wanaoshangilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ