Wananchi wamechanganyikiwa hawatambui kama wapo awamu ya Nne au ya Sita

Wananchi wamechanganyikiwa hawatambui kama wapo awamu ya Nne au ya Sita

TRA wameacha kutangaza makusanyo ya kila mwezi.

Hali ni mbaya mno.

Hiyo ya TRA, kuacha kutangaza makusanyo ni toka kipindi cha dhalimu, na hata walipokuwa wakitangaza sehemu kubwa ilikuwa ni data za kupika. Usidhani tumesahau. Tena wakati ule dhalimu alipoacha kutangaza mapato ya kila mwezi, kulianzishwa hadi uzi wa kumnanga hapa jukwaani. Hivyo leta porojo nyingine kuhusu bibi ushungi na sio hili.
 
Wanafanya hivyo kwa kuwa figure za kila mwezi ni rahisi kushitukiwa kuwa makisanyo yamepungua.

Ila wakijumuisha na kutoa kwa pamoja haitashitua sana.

Ni mbinu ndogo tu ambayo inafanya kazi kwako.
Utaishia kuwa mjinga kila siku.,

Zama za kupika data na kufanya maigizo zilizikwa Chato,Na mkome kulinganisha awamu ya 6 na awamu ya wajinga wa awamu ya 5..
 
Hiyo ya TRA, kuacha kutangaza makusanyo ni toka kipindi cha dhalimu, na hata walipokuwa wakitangaza sehemu kubwa ilikuwa ni data za kupika. Usidhani tumesahau. Tena wakati ule dhalimu alipoacha kutangaza mapato ya kila mwezi, kulianzishwa hadi uzi wa kumnanga hapa jukwaani. Hivyo leta porojo nyingine kuhusu bibi ushungi na sio hili.
Serikali haijaacha kutangaza bali imebadili utaratibu,inatangaza Kila robo..

Hata sasa ukiingia tovuti ya TRA utazikita Takwimu..

Serikali ya Sasa ina pesa ndefu haina sababu za kupika Takwimu.
 
Serikali haijaacha kutangaza bali imebadili utaratibu,inatangaza Kila robo..

Hata sasa ukiingia tovuti ya TRA utazikita Takwimu..

Serikali ya Sasa ina pesa ndefu haina sababu za kupika Takwimu.

Mkuu mimi siamini sana habari za serikali ya CCM, nyingi zina propaganda ndani yake.
 
Tunafanya mambo yaliyofanywa awamu ya nne yaliyosababisha rais kuitwa dhaifu.
 
Ukiangalia mfumo wa uongozi wa awamu ya sita na nne vinafanana sana. (Makusanyo hafifu ya kodi na gharama kubwa za maisha kwa wananchi kwa manufaa ya wafanaya biashara, huduma mbovu za sekta ya umma).
Labda kwakuwa zote ni even numbers
 
Sasa hivi tuweke tozo ya nini ili tuongeze pesa zaidi?
Tunaongea tozo kwenye vinywaji vikali na sigara,tozo kwenye kubeti na tozo kwenye mitandao ya Kimataifa ya kijamii kama Twitter,google nk..

Mwisho uwekezaji Umeongezeka,utalii unakimbia kwa hiyo pesa ziko kama zote.
 
Ukiangalia mfumo wa uongozi wa awamu ya sita na nne vinafanana sana. (Makusanyo hafifu ya kodi na gharama kubwa za maisha kwa wananchi kwa manufaa ya wafanaya biashara, huduma mbovu za sekta ya umma).

Viongozi waliokuwa awamu ya nne katika mashirika ya umma na taasisi nyingine wamerejea kwenye nafsi zao awamu hii ya nne. ( Kinana, Makamba, Nehemia Mchechu)

Baadhi ya mambo yaliyopewa kipaumbele awamu ya nne yamerejea tena kwa kasi awamu ya sita.( Mfano uuzwaji wa wanyama pori na mbuga za wanyama)

Marafiki na wadau wa awamu ya nne ndio hao wenye nafasi awamu hii ya sita. (Mfano Rostam Aziz).

Sasa tunashindwa kuelewa kama tumerejea awamu ya nne au ni awamu ya sita iliyoboresha ya awamu ya nne.

Tuna kila sababu ya kuiona awamu ya sita na sio kuiona awamu ya nne katika awamu ya sita au kuiona awamu ya sita iliyoboresha awamu ya nne.
Acheni uongo.mama Yuko vzr mnoo kuliko rais yyt kupata kutokea
 
ale aleee ......... mm nashangaa sana.kuna watu huku duniani .Mungu anawaona...na hukumu yao naomba ifanyike hapahapa duniani.maana wengi tunavumilia Kama makondoo hatuna la kufanya.jifanye unjikuna.
 
Attachments

  • 1652873235314.jpg
    1652873235314.jpg
    63.2 KB · Views: 7
Back
Top Bottom