MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Wananchi wanapopoteza imani kwenye taasisi za serikali huwa kuna uwezekano mkubwa kwa nchi husika kuingia kwenye korongo. Haijalishi idadi ya hao wananchi, madhara ni lazima yawepo tu. Ukisoma historia, mifano iko mingi mno. Wananchi wakikata tamaa kuna kitu huzaliwa ambacho wengi kifalsafa hukiita NIHILISM, ambapo watu huamini kwamba hakuna jambo la maana kwenye hii dunia, kila kitu ni bora liende tu.
Watu wakifikia hatua hii, hata likifanyika jambo baya kiasi gani ndani ya nchi hawawezi kustuka sana zaidi ya kuwa na hasira. Pia hata serikali ikifanyika jambo jema kiasi gani watu hawawezi kuwa na bashasha kubwa sana kwasababu wanaamini kila kitu ni moto wa mabua uliolenga kuwahadaa kiakili. Nchi ikifikia hapa, suala zima la OBJECTIVITY hufa bali watu huendeshwa na PASSION & VENGEANCE (Hisia na kisirani). Bahati mbaya sana hata wasomi huingia kwenye huu mtego.
Taifa likifia hatua hii, basi fahamu fika kwamba likitokea janga lolote kubwa kama Vita (War of Industrial Scale), Mlipuko wa magonjwa (Epidemics), Anguko la kiuchumi (Economic Collapse) au Maafa ya kijiografia (Natural Disaster) nchi haiwezi kusimama kwasababu kila mtu atajiangalia yeye na kuchukua chake mapema. Hatua hii ndiyo tunaita A FAILED STATE, na bahati mbaya sana kama hatutaangalia sisi nasi tunaweza kuelekea huko.
Swali ambalo huwa najiuliza sana ni hili lifuatalo:
Hivi yakitokea kama yale ya mwaka 1979 kule Kagera na nchi ikavamiwa kijeshi, Tanzania yetu ya leo inaweza kushikamana na kuwa moja dhidi ya adui. AU ndiyo wananchi wanaweza kukaa pembeni wakitazama na kusema bora tukose wote kwasababu wanaamini kwamba hawana hisa yoyote ile kwenye taifa lao. Au hata wengine wanaweza kumuunga adui mkono na kusaidia nchi ivurugike ili tukose wote ???
MUNGU EPUSHIA MBALI: Lakini, hivi ikitokea vita, mlipuko wa ugonjwa au baa la njaa , serikali ya Tanzania inaamini kabisa kwamba inaweza kuwatuliza watanzania ambao wamepoteza nayo imani, wenye kisirani na wasio na utii (IMBETTERED NIHILISTIC TEENS) kama ilivyo leo hii. Unaweza kudhani kwamba hili nalozungumza halipo, lakini taswira halisi ya hisia za watanzania ilionekana kwa kiwango kidogo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Wananchi wengi hawakupiga kura kwa Mzee Edward Ngoyai Lowassa kwasababu walikuwa wanataka mabadiliko peke yake, bali kwasababu walikuwa na hasira na Mzee Jakaya Kikwete na CCM kwa ujumla. Huku wengine wakiwa wanapiga kura wakitegemea yatokee madhara ya kulipizana visasi huko mbele dhidi ya baadhi ya wana-CCM endapo upinzani utachukua nchi.
Kama taifa, tuko hatua mbaya sana.
MUNGU ATUSAIDIE SANA NA AEPUSHIE MBALI.