Wananchi wanataka maendeleo, wanasiasa wanataka Katiba

Wananchi wanataka maendeleo, wanasiasa wanataka Katiba

Kama ulikuwa kwenye mawazo yangu, kwakweli haja kubwa ya watanzania ni maendeleo hasa uchumi wao, kujikwamua kutoka katika wimbi la umaskini,

Lakini wanasiasa kwa tamaa zao za kushika dola na uongozi wa nchi wanapakazia watanzania wanauhitaji mkubwa wa katiba mpya kumbe ni matakwa yao binafsi.

Kenya walipitia mchakato kama huu wa katiba mpya, je, uliwaondolea umaskini wananchi wakenya?! Zaidi ya kuwapa madaraka wanasiasa?! Leo tunaona tena wanasiasa hao hao kwa kutaka madaraka wanakuja na BBI shake hands, wananchi wakawaida wakenya wamebaki na umaskini wao kama mwanzo.

Kwakweli tunachohitaji watanzania ni maendeleo tena maendeleo na uchumi wa mtu mmoja mmoja kumtoa kutoka wimbi la umaskini na sio vinginevyo vinavyo pandikizwa na wanasiasa kwa mgongo wa wananchi.

Watanzania wanataka ajira, wanataka uchumi , wanataka maendeleo full stop!
 
Kuna mijitu humu kutoka mataga ni mipumbavu sana yaani eti hayaoni umuhimu wa katiba mpya hapo hapo yanaamini fix za wanasiasa wanavyodemka Kwa kusema wanajenga nchi

Nchi gani inayojengwa bongo zaidi ya upuuzi wa ngonjera za kijamaa miaka na miaka mambo ni Yale Yale hakuna mabadiliko Wala maendeleo,taifa linaendeshwa kienyeji na Kwa mazoea na genge moja tu la watu wao ndio wanajiletea maendeleo kwenye matumbo yao miaka nenda Rudi

Nadiriki kusema hii nchi ni Kama watu wanasindikiza maisha tu hakuna lolote wananchi wengi wanajipigania wenyewe wapate kula waishi hakuna hata sapoti ya serikali japo kuwawezesha pasipo kutumia nguvu zao wenyewe
Ajabu ukipiga uinuke na kabiashara Kako ndio utaona hao mbio na TRA kujifanya wanakujua sana ndipo wakukamue vizuri

Serikali ya ma CCM haijawahi kuwa seriously Kwa wananchi wake wapo wapo tu kusindikiza watu wa dunia ya kwanza


Povu ruksa mataga

Bitter truth!
 
Kuna mijitu humu kutoka mataga ni mipumbavu sana yaani eti hayaoni umuhimu wa katiba mpya hapo hapo yanaamini fix za wanasiasa wanavyodemka Kwa kusema wanajenga nchi....
Mimi ni mfuasi wa chadema lkn kwa sasa nakubaliana na msimamo wa Rais wangu Samia kuwa kwa sasa tuvumilie kwanza ashughulikie mambo ya uchumi.

hii haimaanishi kuwa Katiba mpya haina maaana la hasha!! ila kupanga ni kuchagua.
tupunguze jazba, mambo mazuri hayataki haraka.
tusiwe ving'ang'anizi kama ruba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
katiba ni mchakato....muda unahitajika.
katiba ni gharama kubwa....fedha zinahitajika.
kwa sasa nchi yetu imeyumba kiuchumi kutokana na janga la korona, hakuna fedha,
fedha zimeelekezwa kwenye miradi mikubwa ya kimkakati n.k.
kutokana na mambo yote hayo kama nchi haifai kulazimisha katiba mpya kwa sasa.

Ifahamike kuwa Katiba sio mali ya CCM wala Chadema, wala ACT, Katiba ni Mali ya Watanzania wote hivyo wanasiasa wasijimilikishe madai ya katiba mpya.hivyo kwa sasa tuvumilie tumuache Rais wetu ajenge uchumi wa nchi yetu kwanza.
tusiwe ving'ang'anizi, tuwe na subira kwani subira yavuta heri.
tujenge nchi yetu kwa kufanya kazi kwa bidii, tujikwamue kutoka ktk umasikini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio Tanzania tu iliyo pigika kiuchumi bali Dunia nzima ipo ktk kipindi kigumu sana kiuchumi, ni ajabu kwa wanasiasa kudai mchakato wa katiba mpya ktk kipindi hiki kigumu cha kiuchumi bila hata kuwaonea huruma wananchi.
wanacho waza wanasiasa wao ni kutwaa dola tu hawana mpango na umasikini unao tukabili.
hata hivyo katiba mpya ni jambo jema ila ni vyema tukawa na subira kwani subira yavuta heri.
tusiwe ving'ang'anizi kama ruba.
kwa sasa wanasiasa tushirikiane pamoja na serikali kujenga uchumi wa nchi yetu, tushirikiane kutatua kero za wananchi, tunachangamoto za barabara, maji safi, afya,elimu n.k.
tujenge uzalendo kwa wananchi wetu ili katiba mpya itukute tuko imara na timamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukiwauliza lini mliandamana au kuhamasisha maandamano kudai maendeleo na mambo yanayomgusa mwananchi moja kwa moja kama huduma bora za afya, elimu nk...sidhani kama watakujibu ila majaribio kazaa ya maandamano kudao tume huru ya uchaguzi na katiba mpya yamefanyika mara nyingi sana...
 
Wao wanataka katiba mpya ili waende ikulu kirahisi...hakuna mteremko pambaneni, Kenya walibadirisha katiba lakini mpaka leo bado kuba migogoro isiyoisha inayotaka katiba mpya...uchaguzi wao nao uligubikwa na sintofahamu mpaka busara ilipotumika..

Katiba zote dunia ni kandamizi hakuna katiba iliyonyooka hata huko USA...katiba ya haki anayo Mwenyezi Mungu tu...ila hapa duniani kila mtu ana takwa lake na huwezi kutimiza la kila mtu...Siku wakija wale LGBT na wanawake wanaotaka waolewe na wanaume 100 tuseme sawa tu katiba ibadirishwe.

Siku majambazi wakitaja ruhsa ya kuiba tuseme sawa tu, siku watoto wakidai haki yakwenda bar tuseme sawa tu......Katiba sio issue ya oyaoya ni issue inayohitaji majadiliano ya wadau wote sio CDM na wanasiasa tu hapana, wadau wote then mchakato uwekwe mezani, hela zitafutwe, muda upangwe na vikao viendelee hapo unazungumzia miaka miwili...
 
Mimi ni mfuasi wa chadema lkn kwa sasa nakubaliana na msimamo wa Rais wangu Samia kuwa kwa sasa tuvumilie kwanza ashughulikie mambo ya uchumi...
uchumi gani anaojinasibu anataka aujenge hapa Tanzania?

Hata mtu pori alikuja na swagger za anainyoosha nchi mwisho wake tunauona kaharibu kila kitu sababu ya mifumo ya nchi mibovu nchi inaongozwa Kwa matakwa ya wanasiasa uchwara Kama alivyokua jiwe

Hatuwezi kuendelea Kama tutaendelea kuongozwa Kwa hisani za raia mmoja mwenye madaraka ya kifalme hatutafika mbali tutakufa tutaacha kizazi Cha hovyo sana sana amini nakwambia huu upuuzi atakayekuja kuumia ni mwanao SI unaona wenyewe waliokua na vyeo wanavyowarithisha madaraka watoto zao?

Amini nakuambia Kwa mfumo huu tutakua watawaliwa milele tusipofanya jitihada familia zao zitaendelea kula keki wenyewe tu

Amini ndugu!
 
Huo ndio ukweli, kwa sasa wanasiasa ndio wanataka katiba mpya kwa lengo lao moja tu tamaa ya kushika DOLA lakini sisi wananchi kwa sasa tunataka maendeleo kwanza, tunataka maisha yetu duni ya kimasikini yakwamuliwe, kwa sasa tunataka elimu bora kwa watoto wetu, tunataka maji safi na salama, tunataka umeme wa uhakika, tunataka huduma za afya bora.
Ukisema maendeleo nafikiri hakuna watu waliojenga hii nchi kama wakoloni ambapo mpaka sasa hutujaweza kuwalipa kabisa waliojenga mashule makubwa ambayo ndio mpaka Leo yanatumika. Reli ya Kati na ndio waliochora ramani za barabara nchi nzima

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
alipokua makam alishindwa leta maendeleo saiz ndo atayaleta ana buy time tu amna jipya apo
 
Huo ndio ukweli, kwa sasa wanasiasa ndio wanataka katiba mpya kwa lengo lao moja tu tamaa ya kushika DOLA lakini sisi wananchi kwa sasa tunataka maendeleo kwanza, tunataka maisha yetu duni ya kimasikini yakwamuliwe, kwa sasa tunataka elimu bora kwa watoto wetu, tunataka maji safi na salama, tunataka umeme wa uhakika, tunataka huduma za afya bora...
Hujui maana ya katiba mpya.ukiijua ina dhamira gani utaitafuta kwa gharama zote.Hayo maendeleo unayoyadai ndio utayapata kwenye katiba mpya.

Mfano hata mawaziri,majaji,wakurungezi,hawateuliwi na Mh Rais bali wanaomba na kusailiwa na kamati za bunge.Tena wabunge hawawezi kuwa mawaziri,wala madiwani hawawezi kupata umeya.

Kifupi Mh.Rais anapunguziwa madaraka kwa asilimia 45 hadi 50 .Wanachaguliwa kutokana na ujuzi na taaluma zao.pia nafasi za kazi zitaongezeka sana.
 
Hujui maana ya katiba mpya.ukiijua ina dhamira gani utaitafuta kwa gharama zote.Hayo maendeleo unayoyadai ndio utayapata kwenye katiba mpya.mfano hata mawaziri,majaji,wakurungezi,hawateuliwi na Mh Rais bali wanaomba na kusailiwa na kamati za bunge.Tena wabunge hawawezi kuwa mawaziri,wala madiwani hawawezi kupata umeya.Kifupi Mh.Rais anapunguziwa madaraka kwa asilimia 45 hadi 50 .Wanachaguliwa kutokana na ujuzi na taaluma zao.pia nafasi za kazi zitaongezeka sana.
mwaka 2010 Wakenya waliandika katiba mpya na ilisifiwa kuwa katiba nzuri na bora haijawahi kutokea, lkn leo waulize imewasaidia nn mpaka sasa? leo hii 2021 wanasiasa wanataka tena mabadiliko, wananchi shida ziko palepale, ubadhirifu kama kawa.

Katiba ni jambo moja lkn pia utashi ni jambo jingine, unaweza kuwa na katiba kama tuliyo nayo ss watz lkn tukafika mbali zaidi kimaendeleo kuliko hata nchi yenye katiba mpya.

Unapaswa utambue kuwa katiba haileti maendeleo bali watu ndio wanao leta maendeleo. kwa sasa tujiandae, tujenge uchumi lkn pia bila kusahau kujenga uwezo wa watu; uzalendo na uadilifu maaana bila viongozi wazalendo na waadilifu katiba mpya ni kazi bure.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ulikuwa kwenye mawazo yangu, kwakweli haja kubwa ya watanzania ni maendeleo hasa uchumi wao, kujikwamua kutoka katika wimbi la umaskini,

Lakini wanasiasa kwa tamaa zao za kushika dola na uongozi wa nchi wanapakazia watanzania wanauhitaji mkubwa wa katiba mpya kumbe ni matakwa yao binafsi...
Kwa maana nyingine unachosema ni kwamba tungebaki tu na magu tuendelee tu na maendeleo full stop.
 
mwaka 2010 Wakenya waliandika katiba mpya na ilisifiwa kuwa katiba nzuri na bora haijawahi kutokea, lkn leo waulize imewasaidia nn mpaka sasa? leo hii 2021 wanasiasa wanataka tena mabadiliko, wananchi shida ziko palepale, ubadhirifu kama kawa...
Kwa maana nyingine unachosema ni kwamba tungebaki tu na magu tuendelee tu na maendeleo.
 
Huo ndio ukweli, kwa sasa wanasiasa ndio wanataka katiba mpya kwa lengo lao moja tu tamaa ya kushika DOLA lakini sisi wananchi kwa sasa tunataka maendeleo kwanza, tunataka maisha yetu duni ya kimasikini yakwamuliwe, kwa sasa tunataka elimu bora kwa watoto wetu, tunataka maji safi na salama, tunataka umeme wa uhakika, tunataka huduma za afya bora...
Lini uchumi wa nchi hii ulishuka hadi kufikia hatua kususpend mambo mengine ili tuuinue kwanza ?
 
Wewe ni mwana siasa unaye tamani kupata nafasi ktk serikali,au kuteuliwa kupitia katiba mpya ila sisi wananchi tunataka kwanza maendeleo.

Katiba mpya ni MAANDISHI TU angalia Jirani zetu wa kenya kati ya mwaka 2014/2015 waliandika katiba mpya ambayo iliitwa katiba bora haijawahi kutokea! lkn leo hii baada ya miaka 6 wanadai tena katiba ibadilishwe!! lkn wanao taka ni wana siasa ili kurahisisha kushika dola.
sisi wananchi hatutaki kupotoshwa, Mama kwa sasa fanya kazi ya kujenga uchumi wetu ili tujigombowe kutoka kwenye umasikini.
Huu mfano wa Kenya unatolewa na watu Fulani wasiojielewa. Kenya walitengeza Katiba mpya nzuri, baadaye wakaona hata hiyo nzuri ina upungufu kidogo, wanataka waondoe huo upungufu. Nyie mnakiri mna katiba mbovu lakini kwa vile katiba mpya ya Kenya imeonekana ina mapungufu mnaona kumbe hamna haja ya kutengeneza Katiba yenu kwa vile mpya ya Kenya ina mapungufu. Hizi akili sijui mlipewa za nini?
 
Watu wenye njaa wanataka katiba mpya, tena katiba yenyewe wanataka waandikiwe na CCM..yapo mengi sana yanapaswa kushinikizwa kwa CCM na watawala kwa sasa kuliko hata hiyo katiba mpya wakati ile ya zamani tu vipo vipengele kibao vinavunjwa na wala hatupigi kelele....hapa ninaloona ni kundi fulani kutaka ulaini wa kuingia ikulu bila jasho na kuleta mitafaruku isiyoisha mwisho wa siku..

Eti tunajifariji katiba mpya ndio italeta maendeleo ya watu....
 
Wewe ni mwana siasa unaye tamani kupata nafasi ktk serikali,au kuteuliwa kupitia katiba mpya ila sisi wananchi tunataka kwanza maendeleo.

Katiba mpya ni MAANDISHI TU angalia Jirani zetu wa kenya kati ya mwaka 2014/2015 waliandika katiba mpya ambayo iliitwa katiba bora haijawahi kutokea! lkn leo hii baada ya miaka 6 wanadai tena katiba ibadilishwe!! lkn wanao taka ni wana siasa ili kurahisisha kushika dola.
sisi wananchi hatutaki kupotoshwa, Mama kwa sasa fanya kazi ya kujenga uchumi wetu ili tujigombowe kutoka kwenye umasikini.
Wameongeza kitu kingine BBN sijui ,katiba yao wameiweka kando🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom