Wananchi wanataka maendeleo, wanasiasa wanataka Katiba

Wananchi wanataka maendeleo, wanasiasa wanataka Katiba

Wapuuzi kama wewe wanaodhani kwamba Katiba mpya ni manufaa kwa wanasiasa tu ni JANGA KUBWA LA Taifa.
Kwa ufinyu wako wa akili ngoja nikueleweshe.
👉🏽 Katiba mpya itahakikisha chaguzi zetu ni HURU na za HAKI.
👉🏽 Watanzania tutakuwa na uhuru na haki ya kuchagua Viongozi tuwatakao bila kuporwa kura zetu kwa kutumia mtutu wa bunduki.
👉🏽 Vyombo vya habari vitakuwa huru na haki ya kufanya kazi zao bila hofu ya kufungiwa, kutekwa na hata kuuawa.
👉🏽 Na huu ujinga wako wa kutumia katiba ya Kenya achana nao kabisa. Katika uchaguzi wa Kenya wa mwaka 2017 taratibu mbali za uchaguzi zilikiukwa na Mahakama Kuu ya Kenya ikatumia vipengele kuyafuta matokeo ya uchaguzi ule na kuitisha uchaguzi mwingine ndani ya siku 60.

Mkuu antimatter pita mtaa huu.



Wewe ni mwana siasa unaye tamani kupata nafasi ktk serikali,au kuteuliwa kupitia katiba mpya ila sisi wananchi tunataka kwanza maendeleo.

Katiba mpya ni MAANDISHI TU angalia Jirani zetu wa kenya kati ya mwaka 2014/2015 waliandika katiba mpya ambayo iliitwa katiba bora haijawahi kutokea! lkn leo hii baada ya miaka 6 wanadai tena katiba ibadilishwe!! lkn wanao taka ni wana siasa ili kurahisisha kushika dola.
sisi wananchi hatutaki kupotoshwa, Mama kwa sasa fanya kazi ya kujenga uchumi wetu ili tujigombowe kutoka kwenye umasikini.
 
Prof. Issa Shivji mwanazuoni mbobezi alisema kwamba;
"Katiba Mpya sio Mwarobaini"
kinacho takiwa kwanza ni kujenga uzalendo na uadilifu kwa wananchi.
kwa sasa kuna tatizo la uzalendo na uadilifu sasa nani anaweza kuisimamia hiyo katiba mpya mnayo idai?!
lkn pia katiba tuliyo nayo bado inatufaa ndio maaana hadi leo tunayo amani na utulivu.
tunacho taka kwa sasa ni maendeleo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa sasa wanasiasa haswa viongozi wa Chadema waache chokochoko,
watuache tuchape kazi, Rais wetu kasema mambo ya katiba mpya badaee sio sasa, waache kulazimisha, watii mamlaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sisi kama Raia wema hitaji letu kwa sasa ni KATIBA MPYA
kwa maana bila katiba mpya hakutakuwa na misingi imara ya kimfumo.
Hatuna haja na matakwa na hisia za mtu mmojammoja, kwa matakwa yake
 
Sisi wananchi lini tulikaa tukakubaliana kwamba hitaji letu ni hilo?
Nikweli ikipatikana Katiba mpya itaweka urahisi wa kuwapa watu Fulani uongozi ILI wafanye maendeleo Yao binafsi kwa amani na utulivu
 
Mkuu sisi kama Raia wema hitaji letu kwa sasa ni KATIBA MPYA
kwa maana bila katiba mpya hakutakuwa na misingi imara ya kimfumo.
Hatuna haja na matakwa na hisia za mtu mmojammoja, kwa matakwa yake
sasa mkuu unapingana na mamlaka.
Mamlaka imesha sema kwa sasa kutokana na changamoto za maradhi ya korona uchumi wa nchi yetu umeporomoka sasa ktk kipindi hiki sio busara kung'ang'ana kutaka katiba mpya.
ni busara kukubaliana na mamlaka kwa kuwa hawajakataa bali kwa sasa wamesema hapana. tukiendelee kubishana na mamlaka utakuwa ubishi, na madhara ya ubishi unayajua.
kwa sasa tuendelee kuchapa kazi ili tujiletee maendeleo na kujenga uchumi wa Taifa letu, tusikubali kuburuzwa na wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa kiongozi huwezi kumridhisha kila mtu au kila kundi
ukitaka kumridhisha kila mtu au kila kundi unaweza kukumbwa na mambo makubwa mawili:
1. utachelewa sana kufikia malengo.
2. Unaweza kupoteza mwelekeo.

Kinacho takiwa ni kufanya maendeleo yanayo wagusa wananchi wengi.
Madai ya katiba mpya ni madai ya kikundi kidogo cha wanasiasa wachache.
wananchi walio wengi mijini na vijijini wanataka kasi ya maendeleo iongeze, tunamuomba Rais wetu asicheleweshwe na kelele za watu wachache, wananchi wengi ambao hawapigi kelele wanamatumaini makubwa na yeye.
Kanyaga twende mbele kwa mbele.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom