Wananchi wanataka maendeleo, wanasiasa wanataka Katiba

Wananchi wanataka maendeleo, wanasiasa wanataka Katiba

Huu mfano wa Kenya unatolewa na watu Fulani wasiojielewa. Kenya walitengeza Katiba mpya nzuri, baadaye wakaona hata hiyo nzuri ina upungufu kidogo, wanataka waondoe huo upungufu. Nyie mnakiri mna katiba mbovu lakini kwa vile katiba mpya ya Kenya imeonekana ina mapungufu mnaona kumbe hamna haja ya kutengeneza Katiba yenu kwa vile mpya ya Kenya ina mapungufu. Hizi akili sijui mlipewa za nini?
Bila shaka itakua ni wachache wanaonufaika na ulaji, hofu yao ni kama katiba itaboreshwa watakosa ulaji.
 
"Kuweka nchi sawa kwanza" ni kazi isiyoisha na ni ya kila siku. Nchi huwekwa sawa kwa kutumia katiba na sheria si kwa kuahirisha matumizi ya katiba na sheria.

Unapoanza kuahirisha matumizi ya Katiba/sheria unakuwa umekabidhi nchi iongozwe na mtu au kundi. Madhara yake ni haya: Hata wawekezaji hawawezi kukuamini kwa sababu hawajui kesho utaamua nini. Usalama wa mitaji huletwa na sheria siyo matamshi wala ahadi.Kwa hiyo hakuna maendeleo bila katiba imara.
 
Huo ndio ukweli, kwa sasa wanasiasa ndio wanataka katiba mpya kwa lengo lao moja tu tamaa ya kushika DOLA lakini sisi wananchi kwa sasa tunataka maendeleo kwanza, tunataka maisha yetu duni ya kimasikini yakwamuliwe, kwa sasa tunataka elimu bora kwa watoto wetu, tunataka maji safi na salama, tunataka umeme wa uhakika, tunataka huduma za afya bora.

Kwa sasa tunaye Rais aliye na dhamira ya dhati kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kisasa hivyo tumpe muda kama alivyo sema ili aweze kujipanga na kushughulikia jambo moja baada ya jingine, tusilazimishe mambo twendeni kwa busara, wanasiasa acheni jazba, wananchi tumemuelewa vizuri Rais wetu Samia.

Kila mwananchi anafahamu umuhimu wa katiba mpya baada ya zoezi la Jaji warioba, ila kwa sasa Rais wetu katumia kauli ya kiungwana huvyo na sisi tuwe waungwana, tusijifanye wajuaji sana, tusiwe wabinafsi, tuache kejeli,tusimbananishe, kila jambo lina muda wake,tuwe wavumilivu kwani mvumilivu hula mbivu.

kazi iendelee.
Maendeleo bila katiba nzuri yapo kweli!!!!
 
Ajabu sana mkuu,matakwa yao wanawapakazia wananchi,mama kawastukia kawapiga TKO,wamebaki kuhenyahenya tu mitandaoni.

Mama shikilia hapo hapo,hakuna kucheka na nyani.
Umuhimu wa katiba hauna mbadala siku wakikuminya pumbu na ukakosa watetezi usije kulialia humu. Wakina nape pole pole makamba mzee makamba na mwanane plus kinana hawakujua Kama zamu zao za kubatizwa kwa Moto zitafika.
 
maendeleo endevu yanahitaji demokrasia na kimsingi,,demokrasia haiwezi kuzuia maendeleo ila utawala wa kiimla na wa kutokuzingatia sheria waweza kukwakisha maendeleo,,
 
Umuhimu wa katiba hauna mbadala siku wakikuminya pumbu na ukakosa watetezi usije kulialia humu. Wakina nape pole pole makamba mzee makamba na mwanane plus kinana hawakujua Kama zamu zao za kubatizwa kwa Moto zitafika.
Katiba haikatazwi kuombwa,ila kwa taratibu zinazotakiwa sio kelele kelele za mitandaoni tu
 
Katiba ni nchi na pia ni maendeleo. Wanasiasa uongea kwa niaba ya wananchi. Wakati mwingine wananchi uongea kwa niaba ya wanasiasa. Wanasiasa ndo wanaoongoza nchi ambayo ni ya wananchi. Hauwezi tenganisha wanasiasa na wananchi. Wanasiasa ni wananchi na wananchi ni wanasiasa pia. Matakwa yao ni mamoja japokuwa msemaji anaweza kuwa tofauti.
 
Basi nyie Mataga ni wapumbavu miaka 61 bado unataka maendeleo ambayo hujui utayapata lini.Hivi nyie mataga nani aliye waroga.

Tunaitaji Katiba bora ambayo itaenda kuondoa wanasiasa sample ya Ccm tunahitaji wawajibishwe na wananchi pale wanaposhindwa kuleta maendeleo

Fala wewe mtoa mada
Umeacha wizi simu hizi ndugu yangu 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
pamoja na kuwa na katiba ya zamani lkn nchi yetu bado ktk kipindi chote hicho imekuwa ikizingatia utawala bora wenye kuheshimu haki za binaadamu, uhuru wa mahakama umetamalaki, kila baada ya miaka 5 Uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani na uhuru, uhuru wa vyombo vya habari unaheshimiwa sana, uhuru wa watu kutoa maoni yao bila woga upo sana, maendeleo kila kona ya nchi yetu n.k n.k.
hivyo kwa sasa nchi yetu haipo kwenye ulazima na uharaka wa kuharakisha kutaka katiba mpya, bado tunafanya vizuri zaidi kuliko hata mataifa yenye katiba mpya.
kwa sasa tujenge na tuimarishe uchumi wetu kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi in wajinga wengi Sana ndio Mana akina jobo wanajitengezea Kinga ili waibe kwa ufanisi
 
katiba tuliyo nayo hivi sasa ni MADHUBUTI sana ndio maaana imetuvusha bila matatizo ktk kipindi kigumu cha kuondokewa na Rais wa awamu ya 5.
Amani na utulivu tulio nao msingi wake ni katiba tuliyo nayo na viongozi makini wanao tuongoza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ndio ukweli, kwa sasa wanasiasa ndio wanataka katiba mpya kwa lengo lao moja tu tamaa ya kushika DOLA lakini sisi wananchi kwa sasa tunataka maendeleo kwanza, tunataka maisha yetu duni ya kimasikini yakwamuliwe, kwa sasa tunataka elimu bora kwa watoto wetu, tunataka maji safi na salama, tunataka umeme wa uhakika, tunataka huduma za afya bora.

Kwa sasa tunaye Rais aliye na dhamira ya dhati kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kisasa hivyo tumpe muda kama alivyo sema ili aweze kujipanga na kushughulikia jambo moja baada ya jingine, tusilazimishe mambo twendeni kwa busara, wanasiasa acheni jazba, wananchi tumemuelewa vizuri Rais wetu Samia.

Kila mwananchi anafahamu umuhimu wa katiba mpya baada ya zoezi la Jaji warioba, ila kwa sasa Rais wetu katumia kauli ya kiungwana huvyo na sisi tuwe waungwana, tusijifanye wajuaji sana, tusiwe wabinafsi, tuache kejeli,tusimbananishe, kila jambo lina muda wake,tuwe wavumilivu kwani mvumilivu hula mbivu.

kazi iendelee.
Tuko tupate uhuru bado tunataka maendeleo tu?
 
Inatakiwa tupate katiba mpya ambayo inaelekeza tunafanya nn ili tupate maendeleo sio kila baada miaka kumi tunabadili malengo maana kwakweli kila tunapokuwa na kiongoz mpya tunabadili vipaumbele na anapoondoka vipaumbele alivyoacha nusu vinabadilika inatakiwa tuwe katiba mpya ili kuepuka waziri kubadili jina la division 0 kuwa division 5 na bado akajisifu et ameboresha elimu, Au waziri kuja kubadili grading na anajisifu ameboresha elimu, Tuwe na katiba ambayo wataalamu wanasikilizwa kuliko mwanasiasa kwenye taaluma husika, Kama ni kuboresha elimu wadau wa elimu wahusishwe kujua changamoto kubwa na namna gani kusolve hizo changamoto, Kwa sasa tupo kama mlevi, Tukipata kiongozi fulani tunapiga hatua kumi kwenye kujenga na mambo mengine ila akija mwingine hatua kumi hizo zinahamia upande mwingine na hatua kumi zile za mwenzake zinavurugwa na kuonekana mwenzake hakufanya kitu, Tunatakiwa kuwa na katiba mpya ili kiongozi akiingia kuna kipaumbele ambacho katiba inampa
 
mambo hayo uliyo yasema, mambo ya maendeleo, mipango ya elimu, afya n.k wala hayahitaji katiba mpya yapo tayari ktk SERA YA TAIFA 2020/2025, 2025/2035.

sera zipo ndio zina ongoza mipango yote ya maendeleo ya taifa letu hakuna kiongozi yeyote anaye enda kinyume na sera/Dira ya Taifa.

hao wanao dai katiba mpya lengo lao ni moja tu uchu wa MADARAKA sio maendeleo ya wananchi.

sisi wananchi tunataka maendeleo tu.
 
Katiba ndiyo yenye kila kitu. Maendeleo yanayopatikana bila utaratibu ulio wazi na uliowekwa na wananchi, ni mapenzi ya viongozi na wanafanya hivyo kwa ubaguzi kwa kuangalia wanaowaunga mkono.
 
mambo hayo uliyo yasema, mambo ya maendeleo, mipango ya elimu, afya n.k wala hayahitaji katiba mpya yapo tayari ktk SERA YA TAIFA 2020/2025, 2025/2035.

sera zipo ndio zina ongoza mipango yote ya maendeleo ya taifa letu hakuna kiongozi yeyote anaye enda kinyume na sera/Dira ya Taifa.

hao wanao dai katiba mpya lengo lao ni moja tu uchu wa MADARAKA sio maendeleo ya wananchi.

sisi wananchi tunataka maendeleo tu.
Sidhani kama unaelewa uwezo wa katiba katika kudhibiti viongozi
 
Back
Top Bottom