Wananchi wanataka maendeleo, wanasiasa wanataka Katiba

Bila shaka itakua ni wachache wanaonufaika na ulaji, hofu yao ni kama katiba itaboreshwa watakosa ulaji.
 
"Kuweka nchi sawa kwanza" ni kazi isiyoisha na ni ya kila siku. Nchi huwekwa sawa kwa kutumia katiba na sheria si kwa kuahirisha matumizi ya katiba na sheria.

Unapoanza kuahirisha matumizi ya Katiba/sheria unakuwa umekabidhi nchi iongozwe na mtu au kundi. Madhara yake ni haya: Hata wawekezaji hawawezi kukuamini kwa sababu hawajui kesho utaamua nini. Usalama wa mitaji huletwa na sheria siyo matamshi wala ahadi.Kwa hiyo hakuna maendeleo bila katiba imara.
 
Maendeleo bila katiba nzuri yapo kweli!!!!
 
Ajabu sana mkuu,matakwa yao wanawapakazia wananchi,mama kawastukia kawapiga TKO,wamebaki kuhenyahenya tu mitandaoni.

Mama shikilia hapo hapo,hakuna kucheka na nyani.
Umuhimu wa katiba hauna mbadala siku wakikuminya pumbu na ukakosa watetezi usije kulialia humu. Wakina nape pole pole makamba mzee makamba na mwanane plus kinana hawakujua Kama zamu zao za kubatizwa kwa Moto zitafika.
 
maendeleo endevu yanahitaji demokrasia na kimsingi,,demokrasia haiwezi kuzuia maendeleo ila utawala wa kiimla na wa kutokuzingatia sheria waweza kukwakisha maendeleo,,
 
Umuhimu wa katiba hauna mbadala siku wakikuminya pumbu na ukakosa watetezi usije kulialia humu. Wakina nape pole pole makamba mzee makamba na mwanane plus kinana hawakujua Kama zamu zao za kubatizwa kwa Moto zitafika.
Katiba haikatazwi kuombwa,ila kwa taratibu zinazotakiwa sio kelele kelele za mitandaoni tu
 
Katiba ni nchi na pia ni maendeleo. Wanasiasa uongea kwa niaba ya wananchi. Wakati mwingine wananchi uongea kwa niaba ya wanasiasa. Wanasiasa ndo wanaoongoza nchi ambayo ni ya wananchi. Hauwezi tenganisha wanasiasa na wananchi. Wanasiasa ni wananchi na wananchi ni wanasiasa pia. Matakwa yao ni mamoja japokuwa msemaji anaweza kuwa tofauti.
 
Umeacha wizi simu hizi ndugu yangu 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
pamoja na kuwa na katiba ya zamani lkn nchi yetu bado ktk kipindi chote hicho imekuwa ikizingatia utawala bora wenye kuheshimu haki za binaadamu, uhuru wa mahakama umetamalaki, kila baada ya miaka 5 Uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani na uhuru, uhuru wa vyombo vya habari unaheshimiwa sana, uhuru wa watu kutoa maoni yao bila woga upo sana, maendeleo kila kona ya nchi yetu n.k n.k.
hivyo kwa sasa nchi yetu haipo kwenye ulazima na uharaka wa kuharakisha kutaka katiba mpya, bado tunafanya vizuri zaidi kuliko hata mataifa yenye katiba mpya.
kwa sasa tujenge na tuimarishe uchumi wetu kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi in wajinga wengi Sana ndio Mana akina jobo wanajitengezea Kinga ili waibe kwa ufanisi
 
katiba tuliyo nayo hivi sasa ni MADHUBUTI sana ndio maaana imetuvusha bila matatizo ktk kipindi kigumu cha kuondokewa na Rais wa awamu ya 5.
Amani na utulivu tulio nao msingi wake ni katiba tuliyo nayo na viongozi makini wanao tuongoza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi katiba mpya inazuiaje. Nchi kuendelea?
 
Tuko tupate uhuru bado tunataka maendeleo tu?
 
Inatakiwa tupate katiba mpya ambayo inaelekeza tunafanya nn ili tupate maendeleo sio kila baada miaka kumi tunabadili malengo maana kwakweli kila tunapokuwa na kiongoz mpya tunabadili vipaumbele na anapoondoka vipaumbele alivyoacha nusu vinabadilika inatakiwa tuwe katiba mpya ili kuepuka waziri kubadili jina la division 0 kuwa division 5 na bado akajisifu et ameboresha elimu, Au waziri kuja kubadili grading na anajisifu ameboresha elimu, Tuwe na katiba ambayo wataalamu wanasikilizwa kuliko mwanasiasa kwenye taaluma husika, Kama ni kuboresha elimu wadau wa elimu wahusishwe kujua changamoto kubwa na namna gani kusolve hizo changamoto, Kwa sasa tupo kama mlevi, Tukipata kiongozi fulani tunapiga hatua kumi kwenye kujenga na mambo mengine ila akija mwingine hatua kumi hizo zinahamia upande mwingine na hatua kumi zile za mwenzake zinavurugwa na kuonekana mwenzake hakufanya kitu, Tunatakiwa kuwa na katiba mpya ili kiongozi akiingia kuna kipaumbele ambacho katiba inampa
 
mambo hayo uliyo yasema, mambo ya maendeleo, mipango ya elimu, afya n.k wala hayahitaji katiba mpya yapo tayari ktk SERA YA TAIFA 2020/2025, 2025/2035.

sera zipo ndio zina ongoza mipango yote ya maendeleo ya taifa letu hakuna kiongozi yeyote anaye enda kinyume na sera/Dira ya Taifa.

hao wanao dai katiba mpya lengo lao ni moja tu uchu wa MADARAKA sio maendeleo ya wananchi.

sisi wananchi tunataka maendeleo tu.
 
Subira yavuta kheri, na kazi ziendelee...
 
Katiba ndiyo yenye kila kitu. Maendeleo yanayopatikana bila utaratibu ulio wazi na uliowekwa na wananchi, ni mapenzi ya viongozi na wanafanya hivyo kwa ubaguzi kwa kuangalia wanaowaunga mkono.
 
Sidhani kama unaelewa uwezo wa katiba katika kudhibiti viongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…