Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Wasanii wengi wa kwetu na watu maarufu wanasahau kuwa Raia ndio waliowafikisha pale juu kwenye mafanikio na wala sio serikali wala Mwanasiasa yeyote.
Nchi kama Marekani, Wananchi walichoma magari, wengine kuyaharibu na kadharika magari ya Elon Musk baada ya kuonekana anatumika vibaya kisiasa jambo lililopelekea soko la magari hayo kuyumba. Hapa nazungumzia magari ya tajiri namba 1 duniani ambaye ana pesa chafu.
Lakini ukija Tanzania Watu Maarufu wenye followers wengi uwa wana dharau nguvu ya umma, Wamesahau kuwa hayo madili ya pesa wanayopata kutangaza kwenye account zao ni kutokana na wingi wa Followers ambao kimsingi ndio Wananchi au Raia wenyewe. Hao Wananchi wakiamua kukugeuzia kete na ku-unfollow account zako zote na kutokufuatilia content zako, lazima urudi kwenye umasikini.
Wasanii na watu maarufu mnatakiwa muheshimu Wananchi kwa sababu ndio maboss zenu, ukileta Uchawa unapigwa No Reform No Election na tunaku-unfollow kwenye account yako. Sisi ndio tumekuweka pale na sisi ndio tunauwezo wa kukushusha hukose hata hayo madili wanayokupa kisa followers.
Operesheni Unfollow Chawa Wote,
Operesheni No Reform No Election
Aluta Continua