Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeongea kwa uchungu sana,na kwa kweli kama taifa tumepotea jangwani,hatujui wapi tunaelekea,kama ni ndege,iko OUT PILOT.Kiongozi wa nchi anapohangaika kufurahisha magenge na wanasiasa kwa lengo la kujinasibu kisiasa na kusahau majukumu na kazi ya kiongozi wa nchi ni yapi, si dalili njema kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa taifa lolote.
Unapohangaika kufurahisha vikundi vya watu ni wazi kwamba kamwe hautafanikiwa kukamilisha kufurahisha kila mmoja kwa 100% na ukizidi kulazimisha kukubalika miongoni mwa watu unakuwa mtumwa wa kuhangaikia kuwafurahisha watu badala ya kutekeleza majukumu ya msingi ambayo yatakuwa kielelezo cha ufanisi wako katika kazi na kuacha watu wapongeze wenyewe.
Maendeleo ya nchi hayaji kwa porojo za jukwaani na kufurahisha makundi ya watu bali kwa jasho na damu, kwa kuchapa kazi, kuweka sera bora za maendeleo na kuzisimamia kwa ukamilifu n.k angalia mfano wa China, hawakupata maendeleo waliyonayo kwa porojo za jukwaani.
Kiongozi wa nchi anayetumia muda wake mwingi kufurahisha watu kwa malengo ya kunufaika kisiasa na kusahau wananchi ambao mpaka sasa wanahangaika na mgao wa umeme,maji n.k HAFAI HATA KIDOGO!
Leo hii Tanzania hakuna mipango wala mikakati mikubwa ya maendeleo.Miradi mikubwa kama SGR, JNHP na mashirika makubwa kama ATCL yanaelekea kufa kutokana na usimamizi mbovu na viongozi kugeuka wanasiasa wa kufurahisha magenge na kuzungumzia petty issues ambazo sio kipaumbele kwa nchi masikini kama Tanzania.Hakuna mikakati na focus ya jumla kama taifa, huku viongozi wakichoma mamilioni kwenda kuhudhuria mkutano kujadili athari ya gesi ya ukaa!
INASIKITISHA SANA
Ni mpumbavu tu anayeweza kuamini huu upumbavu ulio uandika,hakuna utawala uliowahi kupiga mtu risasi.... majukumu ya kiongozi ni kupiga watu risasi? Elewa hili, no matter utatenda mazuri namna gani but as long as unaua au kuumiza watu kwa sababu na visingizio vya kipumbavu (e.g. walituchelewesha sana) huna maana yoyote!
Nani tajiri aliyekufa hovyo?!, kwa hiyo wewe kila kifo ama tukio linalotokea,serikali ina husika?!, kwa nn wajinga wanazidi kuongezeka hapa nchini?Kuna watu vichwani ni empty kabisa, bila kujenga amani kwa njia ya kukaa mezani, nchi itaendaje, au mlifurahia habari za matajiri kufa ovyo na watu kutekana na kutoweka?
Vp, Bado una Imani naye?Kama ulifuatilia rais aliahidi kuwa karibuni Ile kamati itaanza kazi kuhusu jinsi ya kuendeleza mchakato wa Katiba mpya ikihusisha pia vyama vyote.
Hatuna sababu ya kutilia shaka kauli ya rais ambayo aliitoa hadharani.