Wananchi watakula hayo maridhiano?

Wananchi watakula hayo maridhiano?

mtoa post umeeleza ukweli kabisa ila utaona chawa watakavyokuita sukuma gang huku wakikibaliana na wewe kimoyomoyo 😀
 
Huko nyuma hakukuwa na maridhiano ni kipi kilifanikiwa? Tukianzia na maji, umeme afya(madawa) kilimo, biashara nk?
 
Ugali + uji - unga 2200 kwa kilo na elf50 kilo25 kutoka sh 900 siku 366 zilizopita

Mchele 3200 hadi 4000 kwa kilo kutoka 1200 siku 360 zilizopita.

Ngano sh 2000 kutoka 1300.
 
Kiongozi wa nchi anapohangaika kufurahisha magenge na wanasiasa kwa lengo la kujinasibu kisiasa na kusahau majukumu na kazi ya kiongozi wa nchi ni yapi, si dalili njema kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa taifa lolote.

Unapohangaika kufurahisha vikundi vya watu ni wazi kwamba kamwe hautafanikiwa kukamilisha kufurahisha kila mmoja kwa 100% na ukizidi kulazimisha kukubalika miongoni mwa watu unakuwa mtumwa wa kuhangaikia kuwafurahisha watu badala ya kutekeleza majukumu ya msingi ambayo yatakuwa kielelezo cha ufanisi wako katika kazi na kuacha watu wapongeze wenyewe.

Maendeleo ya nchi hayaji kwa porojo za jukwaani na kufurahisha makundi ya watu bali kwa jasho na damu, kwa kuchapa kazi, kuweka sera bora za maendeleo na kuzisimamia kwa ukamilifu n.k angalia mfano wa China, hawakupata maendeleo waliyonayo kwa porojo za jukwaani.

Kiongozi wa nchi anayetumia muda wake mwingi kufurahisha watu kwa malengo ya kunufaika kisiasa na kusahau wananchi ambao mpaka sasa wanahangaika na mgao wa umeme,maji n.k HAFAI HATA KIDOGO!

Leo hii Tanzania hakuna mipango wala mikakati mikubwa ya maendeleo.Miradi mikubwa kama SGR, JNHP na mashirika makubwa kama ATCL yanaelekea kufa kutokana na usimamizi mbovu na viongozi kugeuka wanasiasa wa kufurahisha magenge na kuzungumzia petty issues ambazo sio kipaumbele kwa nchi masikini kama Tanzania.Hakuna mikakati na focus ya jumla kama taifa, huku viongozi wakichoma mamilioni kwenda kuhudhuria mkutano kujadili athari ya gesi ya ukaa!

INASIKITISHA SANA
Umeongea kwa uchungu sana,na kwa kweli kama taifa tumepotea jangwani,hatujui wapi tunaelekea,kama ni ndege,iko OUT PILOT.
 
... majukumu ya kiongozi ni kupiga watu risasi? Elewa hili, no matter utatenda mazuri namna gani but as long as unaua au kuumiza watu kwa sababu na visingizio vya kipumbavu (e.g. walituchelewesha sana) huna maana yoyote!
Ni mpumbavu tu anayeweza kuamini huu upumbavu ulio uandika,hakuna utawala uliowahi kupiga mtu risasi.
 
Kuna watu vichwani ni empty kabisa, bila kujenga amani kwa njia ya kukaa mezani, nchi itaendaje, au mlifurahia habari za matajiri kufa ovyo na watu kutekana na kutoweka?
Nani tajiri aliyekufa hovyo?!, kwa hiyo wewe kila kifo ama tukio linalotokea,serikali ina husika?!, kwa nn wajinga wanazidi kuongezeka hapa nchini?
 
Kama ulifuatilia rais aliahidi kuwa karibuni Ile kamati itaanza kazi kuhusu jinsi ya kuendeleza mchakato wa Katiba mpya ikihusisha pia vyama vyote.

Hatuna sababu ya kutilia shaka kauli ya rais ambayo aliitoa hadharani.
Vp, Bado una Imani naye?
 
Back
Top Bottom