Wananchi wengi wakilipa kodi ndio wataweza kuwadhibiti viongozi wao. Lakini sio kwa nchi yetu ambayo walipakodi hawafiki hata robo ya idadi

Uko sahihi, maana wasiolipa hawana uchungu na ufisadi.
 
Nikweli mkuu, kuna jamaa ana duka la spare za magari lkn yeye uvusha kidokidogo kutoka nchi jurani kwa baiskeli na wala hauwezi kumdhania.

Hatari sana

Tumekadhania tunalipa kodi. Najua wapo wanaofanua hivyo lakini wachache mno.

Wengine utasikia Vat, mara indirect Tax 😀
 
Mkuu logic ni moja tu kwamba kila mtu analipa kodi sio kusema kwamba eti watu wanaolipa kodi ni watu wachache tu !
Sijaelewa ni kwa nini unasema kila mtu huwa analipa Kodi.

Jee unadhani ni kwa nini kupewa Taxpayer Identification Number (TIN) hutolewa Kwa mtu wa kuanzia miaka 18?

Kodi ya uficho (Indirect tax) watu wengi wanalipa ikiwa na pamoja na wale wanaolipa Kodi ya moja kwa moja.

Halafu kusema wafanyabiashara wanapata Faida tu, ni kukosea Sana. Wale wafanyabiashara wanaofilisika huwa inakuwaje!?

Mbona wafanyakazi kila siku wanalalamika mishahara haitoshi lakini bado tu hawaachi kazi...???
 
Wafanyabisha wao wanaelewa utitiri huo wa kodi upo wapi.

Kama swali hilo litakuwa hujalielewa.

Unafikiri ni kwa nini vijana wanaona ni akheri kuajiriwa kuliko kujiajiri na kuanzisha biashara?
we jamaa sijakuita bwege kwa sababu u wa home! Nadhani andiko lako ungeiambia serikali iache anasa kwenye kodi tunazolipa! Mchukulie abiria analipa nauli ambayo tra amechukua kodi, latra amechukua za route, ewura amekata za mafuta,tanroad kakusanyiwa zake na tra, mwenye basi pia kalipa kodi, tbs nae kachukuamo! Halaf unakuja na fact eti hatulipi kodi mpare wa wapi usiejua abc za uchumi? Au nunua vocha weka kwenye simu halafu soma ule mchanganuo! Serikalini humo kumejaa wezi na wanyonyaji
 
Huwezi nielewa
 
Anayepika maandazi amelipia kodi aliponunua unga, sukari na mafuta.
Pia sio kila mfanyabiashara anatakiwa kuwa VAT agent au kulipia kodi ya mapato.
Pia Kuna bidhaa au huduma ambazo ni VAT exempted, hazilipiwi VAT kwa hiyo usikariri kodi kodi tu.
 
Kama mtu kiwango cha biashara yake hakijafikia kulipa kodi unataka afanyaje?? Sio upambane na serikali ikawabane hao wanaoingiza mizigo huko bandarini. Yani mtu ananua pair tatu za viatu za kutembeza mtaani unataka aanze kumkagua muuzaji kama alilipia kodi bandarini!
 
Hakuna mwananchi asiyelipa kodi sema wafanyabiashara ambao kimsingi ni mawakala tu wa kodi ndiyo wengine wanazila hizo kodi wanazokusanya toka kwa wananchi.
Hana elimu ya kodi huyo, Watanzania wengi huwa wanafikiri VAT inalipwa na wafanyabiashara wakati wao wateja ndio wanailipa na wafanyabiashara ni agents/wakusanyaji tu wa hiyo kodi.
 
Huwezi nielewa
sio mimi tu ambaye siwezi kukuelewa hata ma genius hapa hawatakuelewa! Kwa kifupi kodi inayolipwa kwenye manunuzi makusanyo yake ni makubwa kuliko hyo inayolipwa na makundi/wafanyabiashara! Ndo maana nkakupa mfano wa vocha ya simu! ya elfu moja! Hiv kwa siku wamiliki wa simu wananunua vocha ngap? Kadiria tu halafu uzidishe x 152/= halafu useme hatulipi kodi
 
Wéwe ndio huelewi hata ninachozungumzia.

Huo mfuko wa cement unaosema unauhakika gani umelipiwa kodi? Hilo ndio swali
Kwani si unapewa risiti za huo mfuko ulionunua? Kama hujapewa linganisha bei ya wanapotoa risiti utajua kama umelipiwa au haujalipwa.
 
" No taxation without representation "
Huu ulikuwa ni usemi uliotumiwa na waasisi wa taifa la Marekani ,walipokuwa kwenye harakati za kujikomboa kutoka kwa mkoloni mwingereza .
Tanzania mkoloni ni ccm na anatakiwa kung'olewa .
Ni ajabu sana hii nchi
Taifa mfu
 
Hii nchi inatakiwa mass civil disobedience , watu wagome kulipa kodi mazima ili kuwaforce hawa majambazi wauawa laana wang'oke
 
Wapo watu wameajiriwa na wanalipwa mishahara kuhakisha kuna VAT compliance, wanaitwa TRA.
Bidhaa nyingi za vyakula zimesamehewa kodi ya VAT kwa sababu wanunuzi wake wengi ni masikini walalahoi wanaoishi maisha ya kuganga njaa, na hii ni kanuni ya kodi duniani Kate kwamba watu walipishwe kodi kulingana na uwezo
Lengo la kodi sip kukusanya mapato tu kama wendawazimu ndio maana hizo direct tax kama kodi ya kichwa zilifutwa kwa sababu kodi nyingine ni uharibifu kwenye uchumi na stability ya nchi.
 
TRA wana njia zaidi ya milioni kupata kodi zao, kwenye daladala wakichukua risiti za mafuta tu za gari wanaweza kujua kodi anayopaswa kulipa mwenye gari bila hata kopi ya risiti za abiria, wakichukua risiti za kuingiza mizigo hapo bandarini za mfanyabiashara kwa mwaka wanaweza kumkadiria kodi vizuri tu. Fahamu tu kwamba TRA hawajawahi kushindwa kumkadiria mfanyabiashara kodi eti kwa kukosa risiti, hizo risiti huwa ni kwa ajili ya kufanya kazi yao tu kuwa rahisi.
 
Ni muhimu watu kulipa kodi kwa wingi, hii itasaidia kuihoji serikali na pia kugharamia maendeleo yetu. Tusidanganyane, hizo nchi zilizoendelea watu wanalipa kodi hadi wanachanganyikiwa.
Dubai raia hawalipi direct tax, VAT ni 5% na wana maendeleo makubwa tu.
Kuwait, Saudi Arabia na Qatar hakuna direct tax.
 
Dubai raia hawalipi direct tax, VAT ni 5% na wana maendeleo makubwa tu.
Kuwait, Saudi Arabia na Qatar hakuna direct tax.
Si kweli kuwa hawalipi direct tax, Bali hawalipi income tax tu. na rate ya VAT ni 5%. Kodi zingine zinalipwa mfano hotel levy n.k
 
Si kweli kuwa hawalipi direct tax, Bali hawalipi income tax tu. na rate ya VAT ni 5%. Kodi zingine zinalipwa mfano hotel levy n.k
Kuna direct tax gani nyingine muhimu zaidi ya income tax hapa duniani??
 
Literature nyingi duniani zinaekeza VAT compliance huwezi kúiweka kwa kutumia tax administrators pekee. Je watanzania tuna huo utamaduni was kudai na kutoa risiti? Jibu ni hatuna.

Pili, ni kweli huwezi kutoza maskini yaani walio chini ya threshold au bidhaa za msingi.. Sasa kwetu hapa hilo kundi lililo chini ya threshold ni kubwa na ndiyo hoja ya mtoa hoja ilipo - watawezaje kuifanya serikali kuwa accountable? Wakati ni ukweli kuwa hawalipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…