Wananchi wengi wakilipa kodi ndio wataweza kuwadhibiti viongozi wao. Lakini sio kwa nchi yetu ambayo walipakodi hawafiki hata robo ya idadi

Wananchi wengi wakilipa kodi ndio wataweza kuwadhibiti viongozi wao. Lakini sio kwa nchi yetu ambayo walipakodi hawafiki hata robo ya idadi

Umemtukana lakini yuko sahihi kwa kiwango kikubwa..

Watu wengi wameongelea VAT - lakini kwenye nchi yetu VAT compliance ni chini ya asilimia 8. Wakati huo huo bidhaa nyingi za vyakula zimesamehewa kodi ya VAT. Hivyo, watu wengi hawalipi na wanaolipa hawadai risiti.

Pia, umewahi kujiuliza kwa wale wafanyakazi wanaolipa direct tax na bado wanalipa hizo indirect?? Kwa hiyo ni muhimu kundi la wanaolipa direct tax liongezeke la sivyo kulipa indirect tax sio excuse kwa kweli.
Kwanza sijamtukana popote na si vyema kuniwekea tafsiri yako kwenye nilichokiandika. Unadhani ni sahihi kuwalaumu wananchi kuwa hawalipi kodi na hivyo wanapaswa kuacha kudai huduma za kijamii ambazo ni wajibu wa serikali kuzitoa?.
Kwamba katika nchi ambayo sekta nyingi haziko katika mifumo rasmi ulitaka wananchi walipeje hizo kodi mnazodai. Ni wajibu wa na nani kuhakikisha hizo bidhaa tunazonunua na kulipia kodi, hizo kodi zinafika serikalini? Ni nani asiyeona matumizi makubwa na ubadhilifu uliokithiri unaowavunja moyo wananchi kwa kiasi kikubwa. Kwa hili wananchi hawapaswi kulaumiwa kwa kiwango hicho hata kidogo.
 
Ni kazi ya nani kuhakikisha kodi ninayokatwa kama mlaji wa mwisho inafika serikalini?

Wajibu wako ni kudai risiti.
Kama mlaji unapuuzia risíti kwa nini unaamini aliyekuuzia hajapuuzia kulipa kodi kama wewe ulivyopuuzia kudai risiti?
 
Kwanza sijamtukana popote na si vyema kuniwekea tafsiri yako kwenye nilichokiandika. Unadhani ni sahihi kuwalaumu wananchi kuwa hawalipi kodi na hivyo wanapaswa kuacha kudai huduma za kijamii ambazo ni wajibu wa serikali kuzitoa?.
Kwamba katika nchi ambayo sekta nyingi haziko katika mifumo rasmi ulitaka wananchi walipeje hizo kodi mnazodai. Ni wajibu wa na nani kuhakikisha hizo bidhaa tunazonunua na kulipia kodi, hizo kodi zinafika serikalini? Ni nani asiyeona matumizi makubwa na ubadhilifu uliokithiri unaowavunja moyo wananchi kwa kiasi kikubwa. Kwa hili wananchi hawapaswi kulaumiwa kwa kiwango hicho hata kidogo.

Hakuna aliyelaumiwa.
 
Kwema Wakuu!

Taifa ambalo wananchi wanaolipa kodi ni robo tuu ya idadi ya Watu lazima viongozi wawe na nguvu kuliko raia. Zaidi mafisadi huneemeka kwenye nchi za namna hiyo

Kwa sababu watakaolipa kodi ndio watakaokuwa na uchungu na nchi. Watakaokuwa na uchuñgu na kodi wanayoitoa.

Sasa kama robo tuu ndio wanaotoa kodi unafikiri wataweza kupambana na robo tatu iliyobakia. Hawataweza.

Raia ambaye halipi kodi atawezaje kupambana nd viongozi mafisadi?

Mtaani sio ajabu robo tatu ya wafanyabishara hawalipi kodi. Wajasiriamali hawalipi kodi. Bodaboda sijui fundi gereji, fundi nguo, mama nitilie. Hao watakuwaje na uchungu na mafisadi?

Ôooh! Taikon hakuna mtu asiyelipa kodi. Ukinunua kitu au kupata huduma yoyote ukatoa pesa inalipa kodi indirect.
Hiyo najua.

Lakini indirect Tax haiumi kama Direct Tax.

Pesa ya kutoa kwa mkono inauma kuliko pesa hewa ambayo inakatwa juu kwa juu bila kupitia mikononi mwako.

Moja ya njia kukomboa nchi dhidi ya mafisadi ni kuhamasisha Watu walipe kodi kwa wingi angalau nusu au robotatu ya watazania walipe kodi.
Alafu utaona mtiti wake.

Wengi ni wengi tuu.

Serikali za kifisadi kikawaida hazitii ñguvu kubwa kuongeza idadi ya walipa kodi izidi wasiolipa kwa sababu matokeo yake huwa magumu ingawaje yanatija kwa maendeleo ya nchi.

Hivi uliona wapi mtu mzalendo anahitaji mambo ya burebure ilhali nchi ni maskini.

Ukishaona wewe ni maskini alafu serikali yako haitaki uchangie hata kidogo elewa huo ni mkakati wa kukufanya usiwe na nguvu daima.
Mnataka elimu bure wakati nchi ni maskini. Uliona wapi uzalendo unajengwa bila wananchi kugharamia ili wapate maumivu ya kile kizuri wanachohitaji?

Mnataka Afya sijui Dawa bure. Maskini bado utake bure.
Matajiri ndio hupewa vitu bure kwa sababu tayari walishalipia gharama.

Wananchi lazima waambiwe ukweli kuwa kodi na michango yao hata kama ni kidogo ndio itakayowapa huduma.
Watu wajengewe uzalendo kwa kujipigania hata kwa kile kidogo ili viongozi wao wasipate sababu ya kuwatawala kwa njia za dhulma.

Sio ajabu ukasikia kiongozi mmoja mpumbavu akimwambia mtu anayepigania Haki fulani akisema, tumekusomesha bure alafu leo sisi ndio wabaya. Bila sisi kukusomesha bure ungekuwa hapo ulipo? Embu kuwa na shukrani.

Yaani baadaye itakuwa ni lazima ukae kimya ukiona wale waliokupa burebure kama hisani ya kukusomesha.

Ukisema kodi za wananchi ndio zilikusomesha akiwepo mzazi wako. Huyo mzazi wako hana hata leseni yoyote na hajawahi kulipa kodi yoyote Direct.
Ukisema wananunua vitu unauhakika gani hivyo vitu vimelipiwa kodi?

Mangi unayenunua vitu halipi kodi. Pengine sehemu ambayo mangi ananunulia mzigo wake ndiye halipi kodi.
Hujasikia kuna Watu wanapitisha mizigo bandarini bila kulipa kodi.
Kama wapo kwa nini unasema unalipa kodi indirect Kwa kununua vitu kwa Mangi au dukani.
Huoni upo uwezekano wa kununua bidhaa ambayo haijawahi kulipiwa kodi?

Viongozi wa serikali wanajiamini kwa sababu wanajua robo tatu ya watanzania hawalipi kodi.
Hivyo ulileta fyokofyoko wanaanzia na shughuli unayoifanya ambayo hauna kibali wala huna mpango wa kuwa nacho ili ulipe kodi.

Mhalifu mdogo hawezi mdhibiti mhalifu Mkubwa.
Wenye haki wachache hawawezi kuwashinda wasiohaki waliowengi.

Unafikiri kama Watu wengi wangekuwa wanalipa kodi kungekuwa na hayo mambo ya Kikokotoo.
Lakini walipa kodi wachache lazima wamenyeke vilivyo ili serikali iendeshe mambo yake

Acha nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
We kweli hujielewi,hapa ninavyoandika tu hivi tayari nimelipa kodi kupitia bando
 
Nnaponunua bidhaa iwe jumla au rejareja obvious nimelipa kodi,nnaposafiri nimelipa kodi,nikinunua vocha/kutuma hela/kutoa hela nimelipa kodi.Nnapoenda hos nnalipa kodi yaan kiujumla kila nnachotaka kukifanya hapa Tz nnalipa kodi there is no anywhere kwenye uafadhali.
Nchi hizo zilizoendelea ambazo unahisi watu wengi wan kodi(according to you) actually hawatozwi na kuumizwa na gharama kama huku kwetu.Niambie nchi gani iliyoendelea mtu akitaka kununua gari analipa kodi zaidi ya thaman ya gari tena inaeza enda mara mbili!!!???
Bidhaa ambayo kwenye mataifa yaliyoendelea unaezaipata kwa sh 120,000/- kwa hapa unaeza ipata kwa sh 450,000/- na imetengenezwa China ikasafirishwa kupelekwa huko Ulaya ama pia ikasafirishwa from China to Tz.
Mkuu kiufupi sema kwamba shida ni corruption,Ufisadi na ulaf ni tatizo.Gharama za viongozi wa nchi yetu ni kubwa compared.Hapo bado wizi unaofanyika kwenye idara za Serikali unategema nn?

Wewe unajuaje úkinunua mfano kibériti umelipa kodi?
Kama hicho kiberiti kimepitishwa kimagendo au pale bandarini hakijalipiwa kodi kwa nini uamini umelipa kodi kwa kununua kitu.
Nini ushahidi ulionao?

Hao wanaolipa kodi nimekuambia hawafiki robo ya watanzania.
Sio ajabu hiyo robo tatu isiyolipa kodi ndio unanunua bidhaa kutoka kwao.

Tukirudi kwenye magari.
Unajua ni watanzania wangapi wenye Magari kama ukikadiria? Bila shaka hawazidi milioni moja na nusu kati ya watanzania milioni 60.

Vocha, unajua makampuni ya simu yànategemea wateja postpaid ambao hawazidi 10% hao waliobaki ni prepaid yaani Mimi na wewe ambao wengi wetu simu zinaweza kukaa Wiki nzima bila kuingiza vocha ya mia tano.
Bado robo ya watanzania haifiki.

Umetaja bidhaa zikiwa nje ya nchi ni gharama nafuu lakini zikija huku gharama zinaongezeka maradufu.
Mbona kuna bidhaa huku ndani ni gharama kuliko bidhaa zinazotoka nje ya nchi. Mfano Sukari kutoka Brazil.

Vipi mafuta kutoka Singida?
Vipi viatu vya ngozi vinavyotengenezwa hapa Bongo?
 
Mkuu, pata kwanza elimu ya mlipa kodi ndiyo uje umwage madini yako hapa.

Raia yeyote wa nchi hii aliyepo hai ni mlipa kodi bila kujali umri ama status yake.

Kwa mfumo wetu wa kodi usivyo rafiki, watu wengine wanalipa kodi zaidi ya mara moja: mf.

Mfanya kazi anakatwa Payee kwenye mshahara wake, akienda Bank kutoa pesa anakumbana na tozo za miamala, akienda dukani kununua bidhaa anakumbana na Vat.

Na hiyo Vat ipo kila kona ya mauzo, hivyo bidhaa moja inaweza kulipiwa Vat zaidi ya moja.

Kifupi ni hivyo kuna utitiri wa kodi usio na mpangilio kwa kila mwananchi.

Utitiri wa kodi ni tafsiri ya kuwa nchi inawalipa kodi wachache ambao ndio wanakamuliwa hasa kwenye Direct tax

Wewe unaponunua bidhaa kwa mfanyabiashara asiyelipa kodi unasemaje kuwa umelipa kodi?

Hiyo ndio hoja. Kitu gani hakieleweki
 
Ujue we jamaa huwa ninakukubali sn lakin nashangaa leo unaandka pumba tu. Hivi hujui kila bidhaa unaponunua ile bei si halisi inakuwa si halisi sababu ya kodi. Uliwahi jiuliza kwann petrol Zambia 🇿🇲 bei iko chini kuliko tz na wakati mafuta hayo yanapita hapa bongo issues ni kodi. Nenda kafanye utafiti kiwanda cha cement utapata majibu kwann cement inauzwa bei hiyo. Wakati wangeweza uza hata elfu 10.

Hapohapo nakuuliza.

Kama ishu ni kodi inayoongeza bidhaa kuwa na gharama(nakubalo nusu na kukataa nusu) mbona kuna wasiolipa kodi na wanauza bidhaa bei moja na wale wanaolipa kodi?

Nakupa Mfano,
Hapo mtaani kwako kuna kiwanda cha kutengenezea viatu vya ngozi. Hakilipi kodi.
Wanauza viatu elfu 30.
Alafu kuna mtu ameagiza viatu china vya aina ileile na analipa kodi na bei ya kiatu ni elfu 25 unazungumziaje hilo?
 
Kwanza sijamtukana popote na si vyema kuniwekea tafsiri yako kwenye nilichokiandika. Unadhani ni sahihi kuwalaumu wananchi kuwa hawalipi kodi na hivyo wanapaswa kuacha kudai huduma za kijamii ambazo ni wajibu wa serikali kuzitoa?.
Kwamba katika nchi ambayo sekta nyingi haziko katika mifumo rasmi ulitaka wananchi walipeje hizo kodi mnazodai. Ni wajibu wa na nani kuhakikisha hizo bidhaa tunazonunua na kulipia kodi, hizo kodi zinafika serikalini? Ni nani asiyeona matumizi makubwa na ubadhilifu uliokithiri unaowavunja moyo wananchi kwa kiasi kikubwa. Kwa hili wananchi hawapaswi kulaumiwa kwa kiwango hicho hata kidogo
i
Kwanza sijamtukana popote na si vyema kuniwekea tafsiri yako kwenye nilichokiandika. Unadhani ni sahihi kuwalaumu wananchi kuwa hawalipi kodi na hivyo wanapaswa kuacha kudai huduma za kijamii ambazo ni wajibu wa serikali kuzitoa?.
Kwamba katika nchi ambayo sekta nyingi haziko katika mifumo rasmi ulitaka wananchi walipeje hizo kodi mnazodai. Ni wajibu wa na nani kuhakikisha hizo bidhaa tunazonunua na kulipia kodi, hizo kodi zinafika serikalini? Ni nani asiyeona matumizi makubwa na ubadhilifu uliokithiri unaowavunja moyo wananchi kwa kiasi kikubwa. Kwa hili wananchi hawapaswi kulaumiwa kwa kiwango hicho hata kidogo.
Kaka umeongea nadharia nyingi sana

Hoja ya mtoa hoja inasimama kwakweli. Kama nchi tukiwa na walipa kodi wachache ni ngumu kuifanya serikali kuwa acountable.

Watu wanaolipa kodi kikamilifu ni wafayakazi pekee, na ni kwa sababu na wao wamewekewa utaratibu wa lazima na ni rahisi kuwa capture.

Sekta isiyo rasmi hailipi kodi, na ni ngumu kuipata. Mfano watu wenye kipato cha chini ya 4M, hawatozwi kodi y mapato wamesamehewa..sasa hawa watahoji vipi kuhusu accountability ya serikali??? Wakitozwa kodi ni kelele kwenda mbele wakati nchi za wenzetu hata pesa ya matunzo kwa mtoto kwa wana familia walioachana inatozwa Kodi?
 
Kama hukudai risiti kosa ni la nani?
Kama unanunua bidhaa ambapo duka halilipi kodi na hauoni cheti cha kibali kosa nila nani?
Mkuu, haya matatizo yote hayajaibuka ghafla tu. Mwananchi yeyote akizisoma zile ripoti za CAG na akaona ni hatua zipi wanachukuliwa wale watuhumiwa, hatoona kamwe umuhimu wa kudai hizo risiti.
Akiona taabu na mahangaiko anayoyapata kwenye huduma za muhimu za kijamii (maji, afya, nishati, elimu n.k) huwezi kusumbuka na hizo risiti.
Akiona matumizi ya kufuru na ubadhilifu kuanzia ngazi za halmashauri hadi serikali kuu, hawezi hata kusumbuka kudai risiti.
Akiona taabu anayopata kushindia shambani kwa jembe la mkono na uhuni anaofanyiwa akishavuna mazao yake, hawezi hata kuiulizia hiyo risiti.
 
Unachosema ni sahihi
Ila wananchi wengi hawana hiyo Morali authority kutokana nao ni wahalifu. Wengi hawalipi kodi
 
Hakuna aliyelaumiwa.
Mkuu, tukubaliane kabisa kuwa kulipak kodi ni suala la muhimu na lazima kwa maendeleo ya nchi. Ila kama waliopewa dhamana wataendelea na ubinafsi huu, nina hakika wa kulaumiwa ni serikali yenyewe.
Hii nchi wananchi wamebebeshwa mzigo mkubwa sana, wakiamua hata kukwepa kodi ni sahihi kabisa. Wanashiriki na kuchangia ujenzi wa shule, vituo vya afya, vyoo n.k kuanzia msingi, matofali, ukuta, mawe na nguvukazi, serikali inakuja kuapua kwa bati za gauge 32.
Wanashiriki kuchimba mitaro ya kutandaza mabomba na maji yanatoka wiki moja yanakata jumla.
Wanashiriki.
Kila kaya unachangishwa kwa lazima shughuli zote hizo na kama huna wataondoka hata na godoro, masufuria na chochote kile. Nchi hii ina kodi na tozo zilizopitiliza pengine kuliko nchi nyingi tu za kusini mwa jangwa la sahara. Kiujumla nchi hii imeshindwa kabisa kutimiza lengo lake kuu la kuhakikisha ustawi na usalama wa watu wake, kwa mujibu wa katiba yetu.
 
Wajibu wako ni kudai risiti.
Kama mlaji unapuuzia risíti kwa nini unaamini aliyekuuzia hajapuuzia kulipa kodi kama wewe ulivyopuuzia kudai risiti?
Wajibu huo lazima uendane na matumizi sahihi ya hiyo kodi, vinginevyo sitoona umuhimu wa kuidai hiyo risiti, bora nimuachie huyo mwenye duka.
 
Mleta mada ungeainisha ni kodi gani watu hawalipi, maana kuna kodi nyingi sana, katika nchi zenye kodi nyingi huenda TZ pia imo.(mfano ni mafuta ya magari, wanasema karibia 50% ni kodi, maana yake ni kuwa huenda mafuta tulitakiwa kununua kwa 2500 lakini leo yanauzwa 3380)

Sasa uainishe ni kodi ipi watanzania hawalipi, then watu wa kodi waje hapa watoe maelezo ili kila mtu aelewe.

Ila kama ni indirect tax wote tunalipa, kila unachotumia except pumzi unakilipia.
 
Unachosema ni sahihi
Ila wananchi wengi hawana hiyo Morali authority kutokana nao ni wahalifu. Wengi hawalipi kodi
Mkuu, uko sahihi kabisa, lakini mzunguko wote huu utawezwa kuvunjwa na kutupiliwa mbali pale tu viongozi watakapoamua kwa dhati kuuvunjilia mbali. Vinginevyo hiyo moral authority ni lazima ionekane toka serikalini kushuka chini.
 
Wewe jamaa kumbe wakati mwingine huwa unatoa boko kama hili?

Au kwako wewe kodi unatafsiri iwe ile kichwa? Hakuna siku inaisha pasipo mwananchi kulipa kodi iwe directly or indirectly.

Kama unanunua bidhaa ambayo haijalipiwa kodi md hujadai risiti unapata wapi ujasiri wa kusema hakuna ambaye halipi kodi kwa siku?

Hivi unajua Watu milioni 15 wakilipa kodi kila mmoja ni sawa na Tsh 1.5Trilioni?

Kama kwa siku unayosema mtanzania akilipa kodi walau 500 kwa mwezi ni Tsh 15k kwa Mwaka 150k
Sasa kodi 150k × wananchi milioni 30. Unajua ni Trilioni ngapi
 
i

Kaka umeongea nadharia nyingi sana

Hoja ya mtoa hoja inasimama kwakweli. Kama nchi tukiwa na walipa kodi wachache ni ngumu kuifanya serikali kuwa acountable.

Watu wanaolipa kodi kikamilifu ni wafayakazi pekee, na ni kwa sababu na wao wamewekewa utaratibu wa lazima na ni rahisi kuwa capture.

Sekta isiyo rasmi hailipi kodi, na ni ngumu kuipata. Mfano watu wenye kipato cha chini ya 4M, hawatozwi kodi y mapato wamesamehewa..sasa hawa watahoji vipi kuhusu accountability ya serikali??? Wakitozwa kodi ni kelele kwenda mbele wakati nchi za wenzetu hata pesa ya matunzo kwa mtoto kwa wana familia walioachana inatozwa Kodi?
Hizo nadharia ndiyo hali halisi kutokana na mfumo wetu wa kiuchumi ambao sekta nyingi ziko nje ya mfumo rasmi. Serikali inayajua yote hayo na kufidia mapungufu hayo, imeweka tozo na kodi kubwa kwenye kila bidhaa. tunayonunua (mfano mafuta ya petroli,dizeli nk).
Ukienda kwa hao wenzetu walioendelea kodi ni kubwa na pia almost kila kitu kiko kwenye mfumo rasmi, ila pia hawana hizi tozo na usumbufu kwa wananchi hadi kwenda kufyatua matofali ya kujengea zahanati. Ila pia hao wenzetu viongozi wao wana nidhamu iliyotukuka ya matumizi ya hizo kodi na imechochea kuwepo kwa huduma bora kabisa za kijamii na kupandisha morali ya ulipaji kodi.
 
Back
Top Bottom