Kwanza sijamtukana popote na si vyema kuniwekea tafsiri yako kwenye nilichokiandika. Unadhani ni sahihi kuwalaumu wananchi kuwa hawalipi kodi na hivyo wanapaswa kuacha kudai huduma za kijamii ambazo ni wajibu wa serikali kuzitoa?.Umemtukana lakini yuko sahihi kwa kiwango kikubwa..
Watu wengi wameongelea VAT - lakini kwenye nchi yetu VAT compliance ni chini ya asilimia 8. Wakati huo huo bidhaa nyingi za vyakula zimesamehewa kodi ya VAT. Hivyo, watu wengi hawalipi na wanaolipa hawadai risiti.
Pia, umewahi kujiuliza kwa wale wafanyakazi wanaolipa direct tax na bado wanalipa hizo indirect?? Kwa hiyo ni muhimu kundi la wanaolipa direct tax liongezeke la sivyo kulipa indirect tax sio excuse kwa kweli.
Kwamba katika nchi ambayo sekta nyingi haziko katika mifumo rasmi ulitaka wananchi walipeje hizo kodi mnazodai. Ni wajibu wa na nani kuhakikisha hizo bidhaa tunazonunua na kulipia kodi, hizo kodi zinafika serikalini? Ni nani asiyeona matumizi makubwa na ubadhilifu uliokithiri unaowavunja moyo wananchi kwa kiasi kikubwa. Kwa hili wananchi hawapaswi kulaumiwa kwa kiwango hicho hata kidogo.