Wanandoa wengi wameoa/olewa na watu ambao hawakuwapenda, wanandoa mnavumilianaje kwenye hili?

Wanandoa wengi wameoa/olewa na watu ambao hawakuwapenda, wanandoa mnavumilianaje kwenye hili?

Hawakuwapenda?

Hivi kuna mwanadamu dunia hii anaamini eti kuna mwanadamu mshenzi na mwenye mapungufu yote kama yeye eti aje ampende yeye mpaka moyo wake uridhike?

Hana kazi za kufanya kama wewe?

Hii ni ndoto za alinacha ndugu
😂😂😂😂😂😂😂
 
Nimefanya uchunguzi sio rasmi kwa wamama wawili watu wazima Waliodumu Kwenye ndoa kwa miaka zaidi ya 20 Mmoja akiwa na watoto na Mwingine akiwa na watoto na wajukuu Kabisa, Wote story zao zilifanana, ingawa ni watu tofauti hawajuani, utaskia mama anasema huyu mwanaume alienioa, wala alikua hayupo akilini mwangu, ila alinisumbua Kunitongoza kwa muda mrefu sana hadi nikamkubalia, Kwasababu mwanaume nliempenda alikua haeleweki .

Niliongea na mbaba mmoja ndugu yangu mtu mzima mwenye miaka 60+ Aliedumu kwenye ndoa kwa miaka zaidi ya 30+ alikiri mbele yangu Mm kijana wa miaka 20+ kuwa mke wake sio mzuri, Alisema mke wake ana sura mbaya (kiukweli Kabisa mkewe ana sura mbaya si uongo) Ila alimuoa kwasababu huyo mwanamke alimpenda, yani mwanamke alimpenda sana ndugu yangu ndo maana aliolewa.

Jamaa yangu mwingine alieoa na kadumu kwenye ndoa kwa miaka mingi kiasi, aliniambia ameoa huyo mwanamke kwasababu ndio aina ya mwanamke aliyeweza kumpata, hakuwa na option ingine.

Sasa mliooana hii hali mnadeal nayo vipi, maana kukaa kwenye ndoa na mtu usiempenda Wala kuwa na hisia nae daah ni kazi, Si mateso hayo

Sijasoma uzi wako zaidi ya kichwa cha habari. Lkn kifu ni kuwa kumpenda mtu hakumaanishi kwamba ndiyo kunamfanya awe mzuri au bora kwako. Maana hata watu wa hovyo huwa nao wanapendwa.
 
Hakuna mwanamke au mwanaume asiye na kasoro! Anaweza akawa na sura nzuri lakini kwa mambo mengine akawa ovyo.
Tatizo la wanandoa wakishazoeana wanachokana ndiyo maana utasikia maneno kama hayo,nilikosea kuoa/kuolewa,ningejua nisingekuoa/nisingeolewa na wewe,nk
 
Yote ni ubatili,, yafaa nini kuoana bila upendo...

Mahusiano ni kama kivuli,, ukiyafuata yanakimbia,,ukiyakimbia yanakufuata...

Mapenzi ni jambo la hovyo sana
 
Upendo na hisia hua kuna kipindi vyote vinaisha kabisa, so to me hata kama ningepewa nafasi ya kumshauri mtu kuhusu suala la kuoa, nigemwambia upendo unatakiwa uwe kigezo cha mwisho kabisa katika list yake.

Utu, uvumilivu,usikivu, na maarifa ya kijamii kwangu ndo vigezo muhimu sana.

By the way, kurudi hapo juu, kwa ushahidi mdogo tu ndio maana watu ambao hawakuchagua upendo kama kigezo kikuu cha kuingia kwa ndoa wameishi katika taasisi hiyo kwa muda mrefu, na kinyume chake majibu pia unayo.
Umetokota mkuu,upendo kwanza
 
Kumuoa unaempenda kwa dhati utateseka sana maana anaweza fanya atakalo akijua kwake hupindui, kuishi na usiemtarajia inakuwa poa sana mana atakuheshimu na taratibu mtajikuta miaka inasonga tu wala hamzinguani ndani over!!!

hii ni kweli kabisa
Ukwel mtupu kabsa kuoa mwanamke unaempenda kwa dhati kabs no tatzo hapo bdae lazm uteseke
 
Back
Top Bottom