Wanao date na watoto Wa 2000 sijui wanawezaje?

Wanao date na watoto Wa 2000 sijui wanawezaje?

Kuna dem mmoja kitoto Cha elfu mbili na nne(2004) kinasoma pale IFM daresalama mwaka wa pili kozi ya Taxation.
Tumekuwa na mahusiano nacho kwa muda mrefu, mahitaji yake Sasa

1.kila baada ya wiki tatu anasuka,gharama za kusuka sio chini ya elfu 45,000
2.anataka asubuhi kabla sijaenda kazini nikachek na kukasalimia
3.jioni nikitoka kazini nimchek tuongee naye
4.usiku kabla sijalala nimpigie simu tuongee
5.kuombwa hela ni kugusa tuu,mara ohh nimesahau hela geto naomba unitumie hela ya kula
6.bando namuwekea kila baada ya siku tatu la shillingi elfu tatu(3000)
7.aliniambia nimnunulie vitu vya kuboresha geto lake,Kama feni,kabati ya nguo, dressing table n.k

Duhh kiufupi huyu dogo alikuwa FINANCIAL VAMPIRE 🦇.
juzi hapa tarehe 17/12/2024 nikawa bize nikasahau kumtafuta kuanzia asubuhi mpka saa tatu usiku ndo nikamchek.
Cha kishangaza dogo alinijibu kuwa
TUACHANE KILA MTU AENDELEE NA MAISHA YAKE,kisa tuu tangu asubuhi sijamtafuta.

Nilikubali na mpka saivi nasema Bora alienda maana alikuwa Kama liability kwangu.
 
Back
Top Bottom