Mimi nina miaka michache sana niingie kwenye umri wa kustaafu, tokea niko Sekondari Mrema alikuwepo na ni yeye aliyepigania wakulima wa kahawa walipe bei kamili wakanunue pembejeo wenyewe; matokeo yake kahawa Kilimanjaro imebaki kwenye mashamba ya wazungu tuu.
Kama nchi tufikie mahali tuwe na utamaduni wa kufanya "OVERHAUL" na kuingiza damu mpya; Kanisa katoliki pamoja na kuwa uongozi ni kujitolea lakini wana ukomo wa miaka tisa (9) sasa sisi mtu tokea miaka ya 80 ni huyo huyo ndio atoe mawazo ya kutuletea maendeleo, atayatoa wapi wakati kufikiri kwake ni yale yale ya miakaya 80 ya kutamani viwanda na biashara zote zimilikiwe na Serikali?
Embu Bunge pitisheni sheria mwaka huu UDIWANI na UBUNGE wagombea wote wasiwe na umri wa "RETIREMENT AGE"