Wanaoamini NCCR Mageuzi itaachiwa majimbo na CCM wanaota ndoto za mchana

Wanaoamini NCCR Mageuzi itaachiwa majimbo na CCM wanaota ndoto za mchana

Nijuavyo mimi ni kuwa wale wabunge waliotangulia kuingia CCM wakitokea Chadema na Cuf akina Waitara na wenzake itabidi wapitie utaratibu wa kawaida wa kura za maoni na hakuna mbeleko safari hii.

Sasa kama hawa akina Waitara itawalazimu wapambanie ubunge wao hao akina Selasini ubunge wa bure wanaupataje?

Na ukiwaangalia kwa makini wagombea wa NCCR Mageuzi akina Komu, Selasini, Silinde na Lwakatare hawana ushawishi kabisa kwenye majimbo yao na CCM hawana ujinga wa kupitisha wagombea mizigo.

Rip Mmanda ndoto yako ya ubunge Rombo imeshindwa kutimia.

Maendeleo hayana vyama!
Hii haihitaji akili ya ziada ipo wazi.Hata Mbatia mwenyewe Ubunge Hapati sembuse wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa siasa hizi lolote linaweza kutokea maana lazima kambi ya upinzani iwepo, na dalili zinaonyesha lazima iwe ya kutengenezwa! Maandalizi ndo hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kitu kama hicho hao jamaa wameingia cha kike.CCM wanajua fika kuwa kuna Majimbo CDM watatoboa,ila sasa ili majimbo yasiwe mengi ndo wamegawa kura.Hapo NCCR wanatumiwa tu.Kambi ya upinzani hata CDM wasipoishika Tena ACT Wazalendo wanaweza kuishika hasa kwa uwingi wa wabunge toka Zanzibar.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM wanatumia nguvu mno kujaribu kuihuisha NCCR ili iwe chama chake kikuu cha upinzani.
Hii ni sawa na kujenga mji kwa pesa za mfukoni kwako !!
October sio mbali, mtafurahi.
 
Silinde Sana Sana atapata Ukuu Wa Wilaya kama ana bahati ; maisha yake ya kisiasa yatategemea huruma ya mtawala


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nijuavyo mimi ni kuwa wale wabunge waliotangulia kuingia CCM wakitokea Chadema na Cuf akina Waitara na wenzake itabidi wapitie utaratibu wa kawaida wa kura za maoni na hakuna mbeleko safari hii.

Sasa kama hawa akina Waitara itawalazimu wapambanie ubunge wao hao akina Selasini ubunge wa bure wanaupataje?

Na ukiwaangalia kwa makini wagombea wa NCCR Mageuzi akina Komu, Selasini, Silinde na Lwakatare hawana ushawishi kabisa kwenye majimbo yao na CCM hawana ujinga wa kupitisha wagombea mizigo.

Rip Mmanda ndoto yako ya ubunge Rombo imeshindwa kutimia.

Maendeleo hayana vyama!
Kuna vitu vinasikitisha Sana na kufurahisha pia lakini kwa sababu viko ndani ya Political Game (PG) haina budi kuvikubari,kwa Nguvu gani na umihimu upi aliyonao NCCR-Mageuzi wakupewa Majimbo na CCM,ikiwa tu Ushawishi wa kuitikisa CCM hawana inakuwaje wapewe Majimbo???

Ni dhahiri NCCR-Mageuzi anaweza tumika kuhafifisha vyama vingine,akapunguza CDM na akapunguza ACT lakini hatapata kitu,Ndugu yangu Selasinini alikuwa kule Hali ikamshinda akaja CDM,Je Nguvu ya NCCR ya kipindi kile ni sawa na yaleo??? Labda apate Jimbo through Table Negotiation lakini kupitia Secret ballots nampa mkono wa kwa kheri na karibu huku tulime.

David Lusinde na ndoto za kukuwa kisiasa sawa ni kweli unayo haki ya kupambana mpaka ufikie malengo ila nasikitika kuona ndoto ikiwa imefika kikomo mkuu,karata umezichanga vibaya unamkumbuka Mzee Cheyo, Mapalala lakini sasa wako wap??? Ingelikuwa kheri ungebaki kimpya lakini Umetegwa ukaja broo,Sasa nafikiria CDM wakupinge maana si Wapiga kula wako wote wanakupenda,wengine walikupa sababu tu uko CDM Hivyo mpaka Sasa umewapunguza Kaka,lakini unadhani CCM watakubari

Ule msemo wa aliye fanya kazi masaa 12 na aliye fanya kazi masaa 8 wote ni sawa,broo Kuna watu tayari wanalitaka Jimbo nao hawako tayari kuona strange akipewa nafasi eti sababu anauwezo ilo lifahamu Kaka, lakini pia Leo utapata ngao lakini vurugu za kurudi November kila mtu hufa kivyake Kaka.

Anyway binafsi nakutakia mapambano mema kwenye medani ya siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu kama hicho hao jamaa wameingia cha kike.CCM wanajua fika kuwa kuna Majimbo CDM watatoboa,ila sasa ili majimbo yasiwe mengi ndo wamegawa kura.Hapo NCCR wanatumiwa tu.Kambi ya upinzani hata CDM wasipoishika Tena ACT Wazalendo wanaweza kuishika hasa kwa uwingi wa wabunge toka Zanzibar.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa kimkakati zaidi ili iwasaidie kujisafishe mbele ya Dunia. Hata ndani ya CCM yenyewe wale wote wanaoonyesha chembechembe za kuhoji maamuzi au matakwa ya Mkuu kurudi tena ni ngumu sana. Hata kwa kambi ya Upinzani kwa hulka ya Zitto Kabwe sio rahisi wakubali aongoze kambi ya upinzani.

Huyu jamaa na watu wake ni kama wanajiandaa miaka mitano ijayo wasikumbane na watu wa kuhoji hoji vitu vigumu watakao walazimisha hadi kufikiri kutumia njia za siri kuwanyamanzisha
 
Nani aliyesema lazima kuwe na wabunge wa upinzani?

Mbona Zanzibar barazani wapo CCM watupu na mwakilishi mmoja tu wa upinzani tena wa kuteuliwa na Rais na maisha yanakwenda?!
hili nalo linawezekana lakini kumbuka ameshutumiwa sana kutaka kuua upinzani kwa makusudi hivyo ili kulificha hilo wanaweza kutengeneza upinzani
 
Back
Top Bottom