Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Huu ndio ukweli mchungu kwa wote waliowahi kuwa Maraisi wa nchi hii baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka madarakani.Raisi Mstaafu Kikwete alikaribia sana kupata nafasi hii ya kihistoria ila inawezekana alipotoshwa na wenzake ndani ya chama na huenda hili ni jambo analolijutia katika maisha yake na si ajabu siku moja anaweza kuja kukiri/kusema hadharani.
Watawala watambue hakuna kitu wanachoweza ku-achieve na kitachowapa heshima ya kudumu kama kuipatia nchi hii katiba Mpya, Katiba itayokubaliwa na makundi karibu yote ya watanzania kuanzia wanasiasa, wakulima,wafanyakazi,viongozi wa dini, watanganyika, wazanzibari, n.k.
Unaweza kujenga barabara na ma-flyover nchi nzima, kusimamisha majengo makubwa nchi nzima, kuinua uchumi wa watu na Taifa kwa ujumla, n,k, lakini baada ya muda yote haya yatazoeleka na kuonekana ni ya kawaida tu lakini kamwe sio Katiba Mpya inayoweza kuweka msingi bora wa ku-achieve zaidi ya hayo katika Taifa letu.
Raisi Samia, wewe ndio Raisi uliepo madarakani leo hii, hivyo uzi huu unakulenga wewe moja kwa moja na ukiifunyia kazi utakuja kukumbuka maneno yangu haya siku zote za maisha yako.
Mama kazi kwako, kwani fursa sasa iko kwako, hivyo usiache mwingine akaja kuitumia ukaishia kujilaumu.
Unapokuwa Raisi, si ajabu ukazungukwa na watu wanaotamani kuipata fursa hiyo, hivyo wanaweza kukupotosha ili wao au watu wao waje waipate hiyo fursa(sio rahisi kuliona hili au kuliamini, ila ni jambo linalowezekana kabisa kwa wenye kuona mbali).
Nelson Mandela aliepigani uhuru na usawa wa watu weusi nchini mwake, anaheshimika nchini mwake na duniani kuliko makaburu walioijenga Afrika Kusini tena akiwa amekaa madarakani kwa muhula mmoja wa miaka mitano tu.