Gen Z wa Tanzania walipotishia kuandamana kupinga uchafuzi ulioitwa uchaguzi, wengi, hasa machawa, waliwabeza wakijipa imani kuwa wasingeweza. Mbona waliweza. Hata haya maandamano yanayopangwa kufanyika siku ya kuadhimisha uhuru wa Tanganyika yatafanyika, na serikali haitafanya kitu.
Mosi, Gen Z hawatishiki wala hawaogopi yeyote. Pili, wanajua wanachotaka, hasa ikizingatiwa kuwa watawala vipofu na viziwi wamewapuuzia, kuwasingizia, kuwakamata, kuwatesa, kuwafunga, na kuwaua baadhi yao. Tatu, wamekomaa na wanajua hali halisi ya kile wanachofanya.
Nne, watawala wameishatishika na wanatafuta ‘maridhiano’ ili kuepuka lawama na kulinda kitumbua chao haramu. Tano, Gen Z licha ya kuwa na dhamira thabiti, wanajua namna dunia ilivyotafsiri maandamano yao hadi kuwakemea watawala na kutishia kuwachunguza.
Sita, watawala watagwaya kwa kuogopa kuchochea moto uliokwisha washa na Gen Z. Saba, wamejifunza kutokana na maandamano yaliyopita na namna dunia ilivyoyapokea vizuri.
Nane, shida zao hazijatatuliwa wala kuonekana, huku watawala wakisingizia kuwa walioandamana si Watanzania.
Tisa, Gen Z wana hasira na kisasi kutokana na walivyotendwa vibaya. Kumi, Gen Z watapata kuungwa mkono na Watanganyika wanaoona nchi yao ikibakwa na kuporwa na wageni kutoka visiwani.
Hizo ndizo baadhi ya sababu zinazonisukuma kuwaonya wanaojidanganya na kukataa kujifunza, wakidhani wanaweza kuzima moto wa Gen Z.