PostGE2025 Wanaobeza maandamano ya Desemba 9 wanarudia makosa haya

PostGE2025 Wanaobeza maandamano ya Desemba 9 wanarudia makosa haya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Maandamano si matembezi ya hisani. Maandamano yaweza kuambatana na riot, migomo na hata kuchoma vitu au kufunga barabara. Hakuna formula ya maandamano. Hii inaweza tokea kama shinikizo la kutaka majibu ya haraka, kulipa kisasi au kuonyesha hasira au kupambana na ukinzani ulioko mbele unaosababishwa na vyombo vya Dola vinapodhibiti maandamano.
Umetaka mifano ngoja nikupe:
1. Maandamano ya Kenya 2007, 2023.
2. Maandamano ya Madagascar
3. Maandamano ya Bangladesh
4. Maandamano ya ufaransa ya vizibau vya njano
5. Maandamano ya ujerumani mwaka 1829, yaliyo pelekea kuchomwa Kwa bunge la ujerumani.

Kiufupi maandamano yaweza kuwa ya Amani lakini yakamalizika Kwa vurugu na kinyume chake. Hivyo usikariri.
hakuna maadamano kama hayo, wewe uende na njaa zako uje uvunje duka langu useme hamna formular ya maadamano, 😂😂 yaani shaba mtakula nyingi aisee na safari hii shaba sio kutoka kwa polisi tu yaani mpaka wafanya biashara lazima mchezee shaba
 
Gen Z wa Tanzania walipotishia kuandamana kupinga uchafuzi ulioitwa uchaguzi, wengi, hasa machawa, waliwabeza wakijipa imani kuwa wasingeweza. Mbona waliweza. Hata haya maandamano yanayopangwa kufanyika siku ya kuadhimisha uhuru wa Tanganyika yatafanyika, na serikali haitafanya kitu.

Mosi, Gen Z hawatishiki wala hawaogopi yeyote. Pili, wanajua wanachotaka, hasa ikizingatiwa kuwa watawala vipofu na viziwi wamewapuuzia, kuwasingizia, kuwakamata, kuwatesa, kuwafunga, na kuwaua baadhi yao. Tatu, wamekomaa na wanajua hali halisi ya kile wanachofanya.

Nne, watawala wameishatishika na wanatafuta ‘maridhiano’ ili kuepuka lawama na kulinda kitumbua chao haramu. Tano, Gen Z licha ya kuwa na dhamira thabiti, wanajua namna dunia ilivyotafsiri maandamano yao hadi kuwakemea watawala na kutishia kuwachunguza.

Sita, watawala watagwaya kwa kuogopa kuchochea moto uliokwisha washa na Gen Z. Saba, wamejifunza kutokana na maandamano yaliyopita na namna dunia ilivyoyapokea vizuri.

Nane, shida zao hazijatatuliwa wala kuonekana, huku watawala wakisingizia kuwa walioandamana si Watanzania.

Tisa, Gen Z wana hasira na kisasi kutokana na walivyotendwa vibaya. Kumi, Gen Z watapata kuungwa mkono na Watanganyika wanaoona nchi yao ikibakwa na kuporwa na wageni kutoka visiwani.

Hizo ndizo baadhi ya sababu zinazonisukuma kuwaonya wanaojidanganya na kukataa kujifunza, wakidhani wanaweza kuzima moto wa Gen Z.
Wewe walishe tu ujinga wako lakini cha moto watakiona. Tanzania sio nchi ya kuchezewa na wajinga wajinga ni taifa limesimikwa kweli kweli.
Tarehe 29 walijitokeza wengi wakizani jeshi liko nao kumbe Tesha kawauza vibaya.
Safari hii mtakaosalimika hamtathubutu
 
Back
Top Bottom