Aaah mzeee wangu umeanza kuleta ubishi kama ulivyokua unafanya pindi upo UDSM???
Nelson...
Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam sikuwa nafanya ubishi kwani si tabia yangu.
Chuo Kikuu nilikuwa nawashangaza walimu wangu kwa yale niliyokuwa nayajua katika historia ya Tanganyika.
Nakumbuka siku nilipomwambia mwalimu wangu kuwa Julius Nyerere hakuasisi TANU kama inavyoelzwa.
Kishindo chake kilikuwa kizito.
"Una hakika na unalosema?"
Nikamjibu mwalimu kuwa chama cha TANU kimetoka mbali sana toka 1929 babu zangu walipounda African Association.
Nikamweleza mwalimu hadi kufika kwa Nyerere Dar-es-Salaam na kukutana na Abdul Sykes.
Siku nyingine nikamshangaza mwalimu mwingine akisomesha historia ya vyama vya wafanyakazi.
Nikamwambia kuwa hicho kitabu anachotumia kina makosa.
Nikasema hakijamtaja babu yangu ambae maisha yake ni katika sehemu ya historia ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika.
Darasa zima likaangua kicheko.
Walidhani nafanya maskhara.
Nikaeleza historia ya babu yangu Salum Abdallah akiwa muasisi wa TANU Tabora na muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) na Kassanga Tumbo 1955.
Nikaeleza mgomo wa 1960 uliodumu siku 82.
Darasa zima lilikuwa kimya kama limemwagiwa maji baridi.
Siwezi kubishana kuhusu historia hizi kwani mimi ni sehemu ya historia hii.
Anaeleta ubishi ni yule ambae unaumia roho hataki kukubali kuwa historia yote hii ni ya wazalendo hao niliowataja na wao hawamo.
Kulia ni Kassanga Tumbo na Pembeni yake ni Salum Abdallah