Wanaochukia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 wana ajenda gani nyuma ya pazia?

Unakataa mzee wangu bali ulikua mwanafunzi usiyekua na nidhamu UDSM
Nelson...
Sikupata kujua hili.

Kuna mahali nilisoma hapa kuwa Mohamed Said alikuwa ''kilaza,'' yaani hayamudu masomo.

Sina hakika kama ni wewe uliandika au mtu mwingine.

Wakati mwingine vitu kama hivi vina raha yake kusoma.

Vinakufanya ushukuru.
 
Count...
Hapana haja ya kutukana.
Tufanye mjadala wa adabu na heshima.

Hapa Tanzania Bara iliyosaidia mapinduzi ya Zanzibar kuna fursa sawa kati ya wananchi wake wote?

Ni nani wanaohodhi nafasi za elimu kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu?
Ni nani walioshika serikali na bunge na nafasi za kazi huko kote?

Ni nani waliodhalilishwa toka uhuru upatikane mwaka wa 1961?
Unaijua jamii iliyoshika madaraka kwa 80%.

Unaijua jamii iliyodhalilishwa?
Unalijua tatizo hili hapa Tanganyika?

Vipi uyaone ya Zanzibar chini ya Sultan ushindwe kuliona hili lililopo nchini kwako?

Ikiwa Zanzibar imenufaika na mapinduzi iweje serikali ya CCM Zanzibar inashindwa kila uchaguzi?

Wazanzibari hawataki kunufaika na mapinduzi?

Unalo jibu la swali hili?
 
Nelson...
Sikupata kujua hili.

Kuna mahali nilisoma hapa kuwa Mohamed Said alikuwa ''kilaza,'' yaani hayamudu masomo.

Sina hakika kama ni wewe uliandika au mtu mwingine.
Wakati mwingine vitu kama hivi vina raha yake kusoma.

Vinakufanya ushukuru.
Hapana mzee wangu siwezi kukuita kilaza!!!Ila nasikia ulichochea uvunjwaji mabucha ya nguruwe!!
 
Rud
Rudi nyuma kidogo toka Mwaka 1700,s mpaka 1964!!!Usianzie 1964 tu mzee wangu
 
Sasa ila uwe radhi kufundishika
 
Sasa ila uwe radhi kufundishika
Nelson...

Mimi sina tatizo kusomeshwa na wewe kwa hakika unanifanyia ikhsani kubwa sana mimi kupiga goti kwako ukanisomesha.

Hili ni jambo halijapata kunitokea toka nimalize masomo.

Siku zote mimi ni kuingia Vyuo Vikuu kusomesha.

Leo wewe umenipa fursa kubwa.

Niko tayari na ni radhi kuwa mwanafunzi wako.
 
M
Bas ucjsli

Basi ucjali nitapanga utaratibu wa kukufikia!!!Mzee wangu
 
Kuna watu wanadai wewe ulikua kinara wa zile vurugu za mwembe chai na mwanzilishi wa vuguvugu la kutaka tanzania iwe nchi ya kiislamu na ijiunge na IOC na pia unahusika na mihadhara ya kidini katika nyumba za ibada kuwashawishi watu kuvunja sheria za nchi!!!Na umekua unatumia platforms za mitandao ya kijamii kueneza sera zako hizo mzee wangu!!!!Una lolote la kusema kuhusu tuhuma hizi???
Nelson...
Hapana siwezi kufanya uchochezi wa aina yoyote.

Umesikia wapi taarifa hizi?
Una lolote la kusema kuhusu tuhuma hizi mzee wangu???
 
Nelson...
Mimi niseme nini?

Kama nilihusika na hizo shutuma mbona sikukukamatwa na kufikishwa mahakamani nijitetee?
 
Nelson...
Umepotea na darsa lako.

Wakati tunakusubiri nimeona nijaze ombwe hili kwa mimi kutoa darsa kwako na kwa wanafunzi wangu ambao niliwaambia kuwa utatoa darsa na nimewaalika wafuatilie utusomeshe sote.

Kumekuwa na vichekesho kidogo nilipowaambia kuwa wewe umekusudia kunisomesha mimi.

Lakini haya tuyaache kwa sasa.
Naweka hapo chini darsa langu:

''Wazanzibari na Miaka 25 ya Sanduku la Kura Faida Ipi Imepatikana?''

Historia ya chaguzi za Zanzibar kuanzia mwaka wa 1995 hadi 2020 imegubikwa na umwagikaji damu.

Hii mosi.

Pili ambacho kimekuwa kama sehemu ya kudumu ya chaguzi hizi ni kwa ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) kushindwa kutoa matokeo kwa wakati ingawa kura zinaweza zote zikahesabiwa kwa siku moja.

Tatu ni udanganyifu.

Nne ni kutangazwa matokeo ya kura ambayo yana shaka.

Hili limekuwa sehemu ya uchaguzi Zanzibar.

Lakini katika haya yote tukio lililotia fora ni katika uchaguzi wa 2015 pale uchaguzi wote ulipofutwa na kuitishwa upya.

Haya yalifuatia uchaguzi wa 2010 ambao ofisi za ZEC zilizingirwa na wapigaji kura wakidai watoe matokeo.

ZEC haikuwa katika hali ya kuweza kutoa matokea.

Katika uchaguzi wa marudio 2015 uchaguzi ukawa ni kichekesho kwani hapakuwa na uchaguzi ingawa ZEC iliona imefanya uchaguzi.

Baada ya kupitishwa kwa kuwapo kwa SUK wapiga kura wa Zanzibar waliamini kuwa pakiwa na SUK Zanzibar itatulia na uchaguzi hautosababisha kumwagika kwa damu ya mpiga kura yeyote wala kuvurugika kwa uchaguzi wenyewe.

Haya haya hayakuwa.

Uchaguzi wa 2020 kama chaguzi tano zilizopita nao ukawa na matatizo kiasi wafuatiliaji wengi wa siasa za Zanzibar wakaamini kuwa CCM Zanzibar imeshindikana.

CCM Zanzibar haiko tayari kwa chaguzi huru na haki.

CCM Zanzibar ina hofu kubwa ya sanduku la kura.

Inaamini kuwa haina uwezo wa kushinda uchaguzi huru na wa haki.

Lakini nini sababu ya CCM Zanzibar kuliogopa sanduku la kura?

Sababu ni uchaguzi wa kwanza wa mwaka wa 1995 Salmin Amour aliposhindwa na Maalim Seif.

Ilikuwaje CCM chama kilichokuwa madarakani kishindwe na CUF chama kichanga?

Matokeo ya uchaguzi ule uliwadhihirishia viongozi wa CCM Zanzibar Wazanzibar hawawataki na ndiyo sababu ya kuwanyima kura.

Hii maana yake ni kuwa Wazanzibar hawayathamini mapinduzi.

Mapinduzi hayawezi tena kuwa daima.

Mapinduzi yamefikia kikomo sasa yako ukingoni.

Matokeo yake ikawa CCM kila uchaguzi inachukua serikali kwa mabavu kwa msaada kutoka Tanganyika.

Ikawa kila uchaguzi Wazanzibari wanauawa.

Katika hali hii kikawa kimeingia kitu kipya katika kuchagua viongozi Zanzibar.

Kitu hiki kipya Wazanzibari wanakiita ‘’Usultani Mpya.’’

Watoto wa marais wakawa sasa wanagombea nafasi za Urais.

Alianza Amani Karume akafuatia Dr. Hussein Mwinyi.

Bahati mbaya watoto wa marais waliopita wamegombea nafasi za baba zao lakini hawakushinda na damu ya wapiga kura Wazanzibari ikamwagika.

Katika uchaguzi wa 2020 ACT Wazalendo walikubali kuingia katika SUK na kubwa lililokuwa likitafutwa ni kuwepo kwa amani visiwani.

Pawe na amani Zanzibar pasiwe na sababu ya kuendelezwa kwa kukamatwa watu kupigwa na wengine kufungwa jela na wengine kuuliwa kabisa.

Jambo kubwa lililojitokeza baada ya uchaguzi wa 2020 ni kusikika kwa lugha kutoka kwa Wazanzibari kuwa ni lazima SUK iridhiwe na ACT Wazalendo iiingie katika serikali ili damu ya Waislam isimwagike kwa sababu ya ukaidi wa wanasiasa.

Rais Hussein Mwinyi leo ni Rais wa Zanzibar.

Juu ya haya yote kuna jambo moja linalohangaisha vichwa vya viongozi wa CCM Zanzibar.

CCM Zanzibar ina uwezo wa kushinda uchaguzi huru na wa haki uchaguzi ujao 2025?

Hapa ndipo Zanzibar ilipo hivi sasa.
 
Capone...
Nimekujibu labda ukiwa hukulipenda jibu langu.

Nakujibu tena.
Usawa huo unaouliza Zanzibar wakati wa Sultani upo hapa Tanganyika hivi sasa?

Je upo pia Zanzibar hii ya serikali ya mapinduzi?
Sijui kama unaelewa mzee wangu ila hilo si jibu

Kwenye falsafa hilo ni swali kama nililouliza

Kwakuwa huja jibu swali msingi mpaka sasa sina shaka hata kidogo kuwa aidha hujui historia ya Zanzibar au unafanya propaganda za kupotosha watu na unalipwa na maadui wa Zanzibar kutaka kuturudisha utumwani
 
Sijakufahamu overload vipi ? Yaani Wazanzibari hawakudai uhuru kutoka kwa Sultani wakadai uhuru kutoka Uingereza kwa sababu ya Uingereza kuwa ni overload wa Misri na Sudan ?
Hivi uko serious?
Sio overload, ni Overlord soma komenti zangu kwa makini usijichanganye

Nimekwambia Waingereza walikuwa ndio overlords Zanzibar kama walivyokuwa kwa misri na sudan

Neno kama ni tamathali semi inayotumika kulinganisha vitu na kulinganisha Kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili maana yake ni “ hatua na athari ya kulinganisha, ambayo ni, ya kuona tofauti na kufanana kati ya vitu viwili, iwe watu, vitu, mahali au vitu.”

Overlord kwa kimombo maana yake ni “a person or institute of great power or authority”

Unaelewa hali ilivyokuwa Misri na Sudan? Kama huelewi usione aibu kusema nikupe elimu

Ila kwa Zanzibar mambo yalikuwa hivi
Mwaka 1890 walisaini mkataba wa Heligoland ambapo offficially Zanzibar ikawa protectorate ya Uingereza, unajua maana ya protectorate au nikuelezee? Kama hujui sema nikupe elimu Gavana

Na ili uelewe kuwa ktk utawala wa Zanzibar Uingereza ndio walikuwa ndio mabwana wakuu ile
Incident ya 25/08/1896 ilionesha wazi nani ndio kingmaker

Mwaka huo alikufa sultan mmoja anaitwa Hamad bin Thuwaini, mwanafamilia Khalid bin Barghash akataka kukalia kiti cha enzi lakini Uingereza ikasema hapana

Badala yake waingereza walisambaza kichapo kwa Serikali goigoi ya kisultan kwa vita fupi zaidi duniani ambapo ilichukua dakika 45 tu Barghash akaondolewa kwenye kasri na wakamuweka kibaraka waliomtaka Sultan Hamoud bin Mohammed Hiko kichapo wqtu wa historia wanakiita vita ya Anglo Zanzibar


Hata hiyo mwaka 1963 Uingereza aliacha uhuru wa mchongo chini ya sultan ila mashujaaa wetu mzee Karume na wengine walitupa uhuru kamili mwaka ‘64.



Kajifunze upya historia ya Zanzibar na utawala wa Uingereza ktk makoloni yake kwa kifupi soma sana indirect rule ktk makoloni tofauti duniani upanue maarifq yako
 
Mkuu kama unaleta hoja za kihuni sitasita kuziita za kihuni regardless

Nakuuliza swali la msingi hujibu unauliza swali jingine

Ungetaka sana majibu ya maswali yako kwanini hukuuliza tangu mwanzo?

Jibu swali tufunge mjadala kwa hoja zako za mchongo mkuu

Mtu yeyote mwenye akili zake kamwe hawezi tetea tawala dhalimu za kisultan sababu ni kuwa mbali na ubinadamu baki hata hoja zake hazitakuwa na misingi ya kifalsafa kama za kwako hizi za kihuni mzee wangu
 
Mzee wangu ninatamani sana sana ningenufaika nayo ila ninasikitika kuwa kushindwa kwako kunijibu swali langu kunanifanya nikuone mamluki jambo ambalo lina compromise hata imani na heshima yangu kwako mzee

Turudi kwenye mada na ujibu swali langu ikiwa kweli unaijua historia ya Zanzibar na Sultan hakuwa na damu vidoleni mwake

(Ungeijua sayansi ya siasa kamwe usingethubutu kuzua hoja dhalili kama ya kiongozi kukosa damu vidoleni mwake)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…