Darasa sio hapa kuna sehemu inaandaliwa na ninaalika pia wanazuoni wa kidini na wazee wa ASP na TANU na ACT Wazalendo na CUF!!!!Usiwe na haraka nimekwambia uwe radhi kufundishika usijali!!
Nelson ...
Labda nikutahadharishe.
Wewe huwezi kuwa na wazee wa ASP na TANU ikawa mimi hawanijui.
TANU imeundwa na wazee wangu.
Waasisi wa African Association 1929: Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Ibrahim Hamisi, Raikes Kusi na Rawson Watts na wote hawa ni rika la babu yangu Salum Abdallah katika Dar es Salaam ya 1920s.
Waasisi wa TANU wengine wameniona mimi nazaliwa hapa Dar es Salaam.
Nimeishi na wao hadi wanakufa.
Mimi nimeandika kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," Minerva Press, London 1998.
Hawa ndiyo walimu wangu walionisomesha historia ya uhuru na historia ya Julius Nyerere.
Sisi wazee wetu wote ndani ya TANU walikuwa ASP.
Abdul Sykes na Dossa Aziz ndiyo waliompeleka Nyerere Zanzibar kumjulisha kwa Karume.
Abbas Sykes ndiye aliyekuwa mpelekaji fedha kwa Karume hadi wakati wa mapinduzi.
Haya ni machache tu ningeweza kukueleza mengi.
Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala ASP wanamapinduzi walikuwa marafiki wakubwa wa baba yangu wakija hadi kwetu.
Hawa waliuliwa baada ya mapinduzi.
Wewe utaniletea mimi wazee gani wa TANU na ASP wanifundishe mimi historia.
Unaizungumza CUF na ACT Wazalendo.
Mimi siko hapa kufanya utani.
Angalia picha hapo chini.
Picha inazungumza maneno 1000.
Kushoto Juma Duni Haji, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na Mohamed Said
Kampeni za Uchaguzi Mkuu 1995 nyumbani kwa Mama Ummy bint Anzuwani, Ngamiani Tanga.
Kulia ni Dome Okochoi Budohi (TANU Card No. 6) na Mohamed Said Nairobi 1972.
Kushoto Ally Kleist Sykes (TANU Card No. 2) na Mohamed Said Muthaiga Club, Nairobi 1989
(TANU Card No. 3 Abdulwahid Kleist Sykes TANU Card No. 1 Territorial President Julius Kambarage Nyerere).