Salaam, Shalom!!
Nchini petu Tanzania , mwaka kesho 2025 kutakuwapo na uchaguzi mkuu Kwa ngazi zote, Udiwani, ubunge na nafasi ya Urais.
Limeibuka kundi dogo la watu linaloanza kujadili habari za 2030 kana kwamba 2025 tayari Kuna kiongozi special amekwishawekwa tayari Kwa nafasi ya Urais, kwamba tutaingia Uchaguzi 2025 kuchagua Wabunge na Madiwani pekee, hili Si sawa na kinatakiwa kukemea vikali.
Rais aliyepo, ikifika muda wa mchakato ndani ya vyama,akipita mchujo, itafikia time atakuwa mgombea sawa kabisa na wagombea wengine ikitokea chama chake kikampa ridhaa kupeperusha bendera.
Watanzania 2025 Wana HAKI ya msingi kabisa kumchagua kiongozi wamtakaye katika nafasi zote kuanzia Udiwani,ubunge na Urais.
Soma Pia: Wanasiasa na mbinu ya kuweka TV kwenye mikusanyiko ili kuhadaa wapiga kura
Nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi, wananchi Wana HAKI kabisa kumchagua Rais, Mbunge au Diwani Kutokea chama chochote Cha Siasa na akawa Kiongozi.
ANGALIZO: 2025 Kuna Uchaguzi Mkuu, Wananchi tunajua HAKI zetu na tutamchagua kiongozi tumtakaye utakapowadia muda huo adhimu, na kamwe hatutapangiwa. Na wote wanaojadili Urais wa 2030 kana kwamba 2025 hakuna uchaguzi Kwa nafasi ya Urais "WAPUUZWE".
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Karibuni 🙏