Pre GE2025 Wanaojadili Urais wa 2030 ilihali 2025 Kuna Uchaguzi mkuu, wanatuonaje Watanzania?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa katiba na uzuzu wa watanzania, Samia ndiye mahindi wa uchaguzi wa 2025
 
....utadhani wamekubaliana na Muumba kuwa watakuwepo hiyo 2030..!
 
Salaam, Shalom!!

Nchini petu Tanzania , mwaka kesho 2025 kutakuwapo na uchaguzi mkuu Kwa ngazi zote, Udiwani, ubunge na nafasi ya Urais.

Limeibuka kundi dogo la watu linaloanza kujadili habari za 2030 kana kwamba 2025 tayari Kuna kiongozi special amekwishawekwa tayari Kwa nafasi ya Urais, kwamba tutaingia Uchaguzi 2025 kuchagua Wabunge na Madiwani pekee, hili Si sawa na kinatakiwa kukemea vikali.

Rais aliyepo, ikifika muda wa mchakato ndani ya vyama, itafikia time atakuwa mgombea sawa kabisa na wagombea wengine ikitokea chama chake kikampa ridhaa kupeperusha bendera.

Watanzania 2025 Wana HAKI ya msingi kabisa kumchagua kiongozi wamtakaye katika nafasi zote kuanzia Udiwani,ubunge na Urais.

Soma Pia: Wanasiasa na mbinu ya kuweka TV kwenye mikusanyiko ili kuhadaa wapiga kura

Nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi, wananchi Wana HAKI kabisa kumchagua Rais, Mbunge au Diwani Kutokea chama chochote Cha Siasa na akawa Kiongozi.

ANGALIZO: 2025 Kuna Uchaguzi Mkuu, Wananchi tunajua HAKI zetu na tutamchagua kiongozi tumtakaye utakapowadia muda huo adhimu, na kamwe hatutapangiwa. Na wote wanaojadili Urais wa 2030 kana kwamba 2025 hakuna uchaguzi Kwa nafasi ya Urais "WAPUUZWE".

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Kwa akili yako uchaguzi hautofanyika au?
 
Kufanyika uchaguzi na kukawa na kupotoa HAKI na kukithiri vitendo vya RUSHWA na wizi wa kura,

Ni sawa tu na "KUTOFANYIKA UCHAGUZI."

Kama hujaelewa, basi hutaki kuelewa.
 
Ukitizama kwa makini viongozi wote waliopo madarakani kwasasa kwa ngazi za juu haonekani mtu mahiri na mwenye sifa za raisi wa 2030.

Katika mazingira ya kisiasa ya sasa, Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinatokana na uongozi dhaifu. Hali hii imeibua maswali mengi kuhusu mustakabali wa nchi na jinsi uchaguzi wa raisi mwaka 2030 utakuwa na athari kwa kizazi kijacho. Wakati viongozi wa sasa wanaonekana kukosa mwelekeo, maadili, na maono, ni wazi kuwa kuna haja ya mabadiliko makubwa ili kuweza kupata kiongozi anayefaa mwaka 2030.

Uongozi Dhaifu wa Sasa
Viongozi wengi wa sasa wanaonekana kuegemea zaidi kwenye maslahi binafsi kuliko yale ya wananchi. Badala ya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na uwazi, wengi wanajikita katika rushwa, ubinafsi, na maamuzi yasiyo na misingi thabiti. Hali hii imepelekea maendeleo duni katika sekta muhimu kama vile afya, elimu, na miundombinu. Zaidi ya hayo, upungufu wa uwajibikaji na uadilifu miongoni mwa viongozi umekuwa ukidhoofisha imani ya wananchi kwa serikali.

Athari kwa Uchaguzi wa Mwaka 2030

Iwapo hali hii itaendelea bila kubadilika, kuna uwezekano mkubwa kwamba uchaguzi wa mwaka 2030 utakumbwa na changamoto nyingi. Kwanza, huenda upatikanaji wa kiongozi bora ukawa mgumu kutokana na kukosekana kwa viongozi wenye uwezo wa kusimamia vizuri masuala ya kitaifa. Pili, imani ya wananchi kwa mchakato wa uchaguzi inaweza kuendelea kudhoofika, hali ambayo inaweza kupelekea kushuka kwa ushiriki wa wapiga kura na kuongezeka kwa migogoro ya kisiasa.

Umuhimu wa Kuibua Viongozi Wenye Maono

Ili kuhakikisha kuwa mwaka 2030 Tanzania inapata raisi mwenye uwezo na maono, ni muhimu kwa vyama vya kisiasa, asasi za kiraia, na wananchi kwa ujumla kuanza kujenga mazingira yatakayowezesha kuibuka kwa viongozi wenye maadili, uadilifu, na uwajibikaji. Hatua za makusudi zinapaswa kuchukuliwa katika kuelimisha na kuandaa kizazi kipya cha viongozi ambao wataweka mbele maslahi ya nchi na wananchi wake.

Hitimisho

Wakati tunaelekea katika uchaguzi wa raisi mwaka 2030, ni lazima tuzingatie hali ya uongozi wa sasa na kufanya mabadiliko yanayohitajika ili kuleta viongozi bora wenye maono. Ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kwamba tunapata kiongozi anayestahili na anayeweza kusimamia maendeleo ya nchi kwa uwazi, uadilifu, na upendo wa dhati kwa watu wake. Hili linawezekana tu kama tutajitolea kwa dhati kuboresha mazingira ya kisiasa na kijamii kwa ajili ya kizazi kijacho.
 
Waambie 2030 tunaenda na Paul Christian Makonda,,
 
Hata mimi sioni.

Ndio tunaenda kuitupa Nchi popote maana sioni mwenye sifa hata hiyo 2025.
 
Si mlisema wenyewe mnahitaji dira ya taifa ya miaka 50 hadi 100 ijayo?
 
Back
Top Bottom