Wanaolilia legacy ya Hayati Magufuli someni alichoandika Bollen Ngetti

wazee wa 'soft science' tunawaachia mtoe hizo definitions za neno 'legacy' na hoja nyepesi, sisi wengine tunajua tumepoteza nini
 
Na unajiita justice? Wewe ni fukn
 
Hivi azimio la Arusha na siasa ya ujamaa vingaliko?
Au ni vilishabaki kama ngano na simulizi za kale? Wanaoamini katika hizo ziitwazo "ujamaa na azimio la Arusha" ni wanasiasa walaghai na waumini wao wasiojua wakitakacho...
Hata kufeli nako ni legacy!!
 
Teh😅,kunywa maji upunguze hizo hasira,hakuna kiongozi aliyepita nchi hii bila kuacha legacy,kwanini iwe nongwa kwa Uncle Magu?
 

Kama hata Hitler ana legacy (soma Wikipedia) basi Magufuli hakosi. Labda mgogoro uko kwenye “maana” ya Legacy. Elewa legacy iko pande zote: kwenye mambo chanya na mambo hasi.

Magufuli kaacha athari kubwa sana katika taifa hili. Nilichokiona dhahiri katimiliza lile tishio aliloeleza Nyerere kwamba kwa katiba tuliyo nayo anaweza kutokea Rais akawa dikteta mbaya sana. Yeye kathibitisha kivitendo hatari inayokabili taifa kutokana na katiba na taasisi dhaifu zilizopo.

Magufuli anasifiwa sana kwa “ujasiri na uthubutu”. Kwa Tafsiri sahihi ni kuamua na kutenda bila kuzingatia Katiba, sheria, kanuni wala kuhusisha taasisi muhimu. Bila hata kusikiliza ushauri wa wataalamu. Kwa mfano, hakuna Rais aliyewahi kuwa na ujasiri wa kujenga international airport kijijini kwake. Au kuanzisha miradi ya mabilioni kwa utashi wake tu.

Aidha, jinsi uchaguzi mkuu wa 2020 ulivyoendeshwa na kulazimisha kuwaondoa wapinzani wote bungeni halafu kuingiza wa viti maalum toka CHADEMA kinyume cha taratibu ilikuwa ni kuonyesha kivitendo (demonstrate) jinsi katiba ya JMT inavyompa madaraka yote (absolute power) Rais wa JMT.

In fact, alithubutu kulipanga Bunge anavyotaka na kuwafanya wabunge wote wajue kuwa wako bungeni kwa hisani yake - sio ya wananchi! Inawezekana kabisa wako wabunge wa CCM walioshinda kihalali lakini wakaongezewa kura za ziada (wizi) kuchafua ushindi wao. Hivyo wote kujikuta wanaimba “sifa na utukufu” kwake bila kupumzika. Watangulizi wake walikuwa na chembe ya soni; wasingeweza kufanya hivyo.

Hiyo ni legacy nzito sana ya kuzingatia kwa watakaoandika biography yake.
 
Legacy ni kitu ambacho ni generational hakifutiki ni urithi,Hayati Nyerere na Karume waliacha Legacy ya Muungano, Mwalimu legacy yake nyingine ni matumizi ya kiswahili nchi nzima kinachokiunganisha taifa kilichoua matumizi ya lugha za makabila,ukombozi wa Afrika na falsafa ya utu na umoja wa Afrika ndiyo maana wanajenga sanamu yake AU makao makuu. Magufuli kaacha legacy moja kuu ni umuhimu wa falsafa ya kufanya kazi na maamuzi yenye ujasiri kwa taifa. Inawezekana asiwepo rais mwingine atakayewafundisha watanzania umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii. Matokeo yake ni hiyo miundo mbinu tajwa kila mahali siyo ya kupuuzwa..
 
Yaani mpaka hapo wewe mwenyewe tayari ushaipinga LEGACY ya huyo SHAITWANI kwa sababu hakukitaka KINGEREZA na hata sheria zilitakiwa kuwa za kiswahili

Sasa imekuwaje unatuletea KINGE humu we si ni kina SHOLOLE usitutoe kwenye reli nimekujibu wala sijasoma
 
Mleta maada kuna mahala ni kweli na sehemu Nyengine ni mwongo.soma hii

Legacy:
: 1.a gift by will especially of money or other personal property : bequest She left us a legacy of a million dollars. 2 : something transmitted by or received from an ancestor or predecessor or from the past the legacy of the ancient philosophers The war left a legacy of pain and suffering.

Sasa ukisema Hayati Magufuli hakuacha Lagacy yoyote ni uongo mtu.
Ameanzisha mifumo mingi mfano ukusanyaji Kodi ki electronic hii haiwezi badirika milele,
Kwamba tunaweza kukusanya kodi na tukajiendeleza bila kuwa omba omba hii haibadiriki milele,

Mikataba ya madini kubadirika tusiibiwe makinikia ambayo yana madini 60% ; hii haitabadirika yawezekana milele

Amepambana na rushwa kwa kazi ya ajabu hii ni legacy haifutiki .Yako mengi

So inategemeana legacy umeilewaje?
 
Yaani kweli nilikuwa na nia ya kusoma, nilipofika pale aliposema daraja la Manzese limejengwa na Masumbuko Lamwai ndio nikaona hii ngoma ya machizi ngoja nijitoe.
Lamwai alikuwa Mbunge tu wa Ubungo baada ya uchaguzi wa 1995 tena wa upinzani (Nccr-Mageuzi) baada ya kumshinda M-CCM Venance Ngula
Swali Lamwai alijenga hilo daraja kwa utaratibu upi kama Mbunge tena wa Nccr! Hivi mwandishi anajua lile daraja lilijengwa lini kweli.
Nimebaki hapa kwenye habari ya daraja sababu mwandishi anaonekana hana adabu na facts lakini anataka tuamini hayo mengine kuhusu habari za legacy? How?
 
Mawazo yako mfu ni sawa na mtu mwenye utindio wa ubongo
 
Mapato, kweli kila mtu anazake! Kuongezeka mapato kila mwaka yanayokusanywa na traffic bila kutoa neno? Maana yake watu hawakuwa wanaelimishwa au walivurugwa na yeye mpaka wakawa wanavunja sheria za barabarani bila kujijua. Kama huo ndiyo ubora wake mnaompamba nao! Hongera zake kwa kukatiwa umeme.
 
Uchaguzi au Uchafuzi?
 
Hivi kuanzisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 haitoshi kusema mwinyi aliacha legacy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…