Inaonekana vyuo vyetu vinafaulisha vijana ambao hawajaelimika.
Mngekuwa mmeelimika mngejua kwamba ajira hakuna.
Ajira ni zao la kukua kwa UCHUMI. Hakukuwepo na uwiano wa ukuaji elimu ukilinisha na uchumi.
Kwa mfano mwaka 90 wilaya yangu ilikuwa inafaulisha watoto 60, mkoa wangu ulikuwa na shule 12 na tulikuwa na vyuo vikuu 2 tu. Leo wanafunzi 60 wanafaulu kutoka shule moja ya kijijini hapa wilayani kwangu.
Mkoa mzima zinakaribia sekondari 200. Vyuo vikuu nchini sasa vinakaribia 50. Umewahi kujiuliza huu ni ukuaji wa % ngapi!?
Hata ajira zilizokuwepo kipindi cha JK nyingi zililenga kuhudumia ukuaji wa sekta ya elimu.. ndipo tukaona ajira za walimu wa msingi, sekondari, vyuo na vyuo vikuu. Sekta hii ndio iliajiri kwa wingi. Kama kuna msomi hajui haya basi huyo hajaelimika ni bure kabisaa