Wanaomiliki Toyota Starlet wanaonekana vituko wakiwa mjini na Vigari vyao

Wanaomiliki Toyota Starlet wanaonekana vituko wakiwa mjini na Vigari vyao

Mbongo asipokuwa nacho anataka yule aliyenancho awe kama yeye...

#Roho za kichawi...
Sawa wewe unavimbia nini na starlet yako, unatofauti gani na bajaji bora bajaji anaingiza hela
 
Nakuonea huruma kwa huo mtazamo wako. Wee tembea tu na mguu mwenzako na starlet yake tuone nani anamudu maisha zaidi[emoji23][emoji1787]
Kwani kuna watembea kwa miguu na wapanda daladala wangapi wanamudu maisha yao. Kwangu daladala ni best option kwanza sidharauriki, hakuna mtu anayejua kipato changu, nakutana na jamii na watu tofauti tofauti na jifunza maisha na ki ujamaa nikiwa ndani ya daladala
 
wenye wivu utamjua tu!!
Sasa mimi nina nini cha kumuonea wivu mwenye starlet? Kama ni usafiri napata kupitia daladala, kama kunyeshewa na mvua hata kwenye daladala sinyeshewi, kuhusu comfortable hata ukipata siti kwenye daladala comfortable ipo hasa seat iwe ya dilishani. Sasa wivu utoke wapi??
 
Mbongo asipokuwa nacho anataka yule aliyenancho awe kama yeye...

#Roho za kichawi...
Nataka watu wote wenye vigari vya starlet myaache magari yenu au ikiwezekana myafanye vyuma chakavu au toeni siti iwe banda la kufugia kuku. Msiwe na haraka ya kumiliki gari ya bei ya chini. Jaribuni kuendelea kujiwekea fedha zaidi na mnunue magari yenye hadhi ili hata sisi watembea kwa miguu mtutolee uvivu wa kuomba lift
 
Unakuta jitu lina mwili mkubwa linaendesha starlet halafu vioo kashusha maana hakina Ac, mwili wote unajaa kwenye gari yaani ni vituko halafu unakuta mtu kama huyu anajiamini kumiliki gari Aisee mimi bora niendelee kutembea kwa mguu lakini sio kumiliki hili gari la starlet na aina nyingine za baby Walker.
mjini mipango ndugu, fata yako !!

Unaweza kuendesha gari kubwa la kifahali ila fala mmoja tu hivi.
 
Wewe sio kila jobless hana hela. Watu tuna miradi ya biashara tunaiyendesha wemyewe wala hatutegemei kuwa mtumwa wa biashara ya mtu.
Kwani wewe mtu akisema jobless unaelewa nini??? Kwani huko kwenye miradi ya biashara si ndo mtu anakofanyia kazi?? Au kwako wewe jobless ni ile kutokuwa na ajira pekee?? U-JOBLESS WA HUYO JAMAA NI KWAMBA HANA AJIRA NA WALA HANA MRADI WALA BISHARA INAYOMWINGIZIA KIPATO, LAKINI ANADIRIKI KUMCHEKA KWENYE GARI DOGO.
 
kunasiku niliazima spacio ya blaza Ford yangu ilizingua.gari haikuwa na ac ilibidi nishushe kioo nilijiona mnyonge kinyama Kila nikipita mjini nahisi kilamtu ananijua kama vile natembea nje😁😁
 
Nataka watu wote wenye vigari vya starlet myaache magari yenu au ikiwezekana myafanye vyuma chakavu au toeni siti iwe banda la kufugia kuku. Msiwe na haraka ya kumiliki gari ya bei ya chini. Jaribuni kuendelea kujiwekea fedha zaidi na mnunue magari yenye hadhi ili hata sisi watembea kwa miguu mtutolee uvivu wa kuomba lift

Wewe una stress zako tu, ushakata tamaa...

Thread 'Bado naumia sana. Huyu binti bado ananichanganya na kunivuruga' Bado naumia sana. Huyu binti bado ananichanganya na kunivuruga
 
kunasiku niliazima spacio ya blaza Ford yangu ilizingua.gari haikuwa na ac ilibidi nishushe kioo nilijiona mnyonge kinyama Kila nikipita mjini nahisi kilamtu ananijua kama vile natembea nje😁😁
😂😂😂Mtuache na boda boda zetu
 
Ukishaona mtu anatumia muda kudharau chombo cha usafiri cha mwenzake kuwa hakina dhamani;
Iwe baiskeli, Pikipiki, Bajaji au hata gari; Ujue tu huyo hana chombo cha usafiri
Wanaoponda vyomba vya usafiri hapa utakuta ni watembea kwa miguu au wanajivunia magari waliyo nunuliwa na wazazi wao, au pengine wanajivunia magari ya ndugu zao au Marafiki zao (lakini sio magari waliyo nunua kwa hela zao walizo zihangaikia); watuache!
Kila mtu anapendeza akiwa kwenye chombo cha usafiri kinachoendana na kipato chake...
 
Kwer kabisa
 
Daladala ni usafiri wa hovyo kabisa, hauna afadhali yoyote, hapo mbezi mwisho napita kila iitwayo leo, ni kero kuanzia mwendokasi hadi hizo daladala, kukanyagana, kuchafuana, kunusishana vikwapa na midomo inayonuka. Huwezi linganisha anayeendesha starket/vitz na anayeshika bomba ya daladala. Tusiwaonee wivu mkuu.
Mpaka nimetaka kumuuliza jamaa daladala za wapi zina nafuu, anafanya kazi gani?

Usafiri wa umma Dar una utaratibu wa HOVYO ,kama mida yako ya biashara au kazi ni asubuhi by 8:00 A.M uwe umewasili na muda wa kutoka ni kuanzia 3:00 P.M unaweza lia.

Tena route kama Kokote kwenda Temeke/Mbagala. Posta-Gongolamboto. Kariakoo-Mbezi. Hata mwendokasi, kuminyana, wanawake wanabambiana.

Ni kweli kale kagari hakana sura nzuri, lakini ukiwa nako kanaokoa mambo mengi sana ya mizunguko.

Starlet na Bajaj dah mtoa mada ana tatizo, Bajaj mkuu hau relax inavyo move, ukimpa mtu lift na starlet anaweza kusinzia, Bajaj labda awe kalewa🤣🤣
 
Natafuta kazi, nina ujuzi wa kusimamia biashara kwa miaka 5

Huna akili mtoa mada tafut kwanz kazi
Kidogo niandike kuwa huyu jamaa ni under 30, halafu anaweza kuwa anakaa kwa ndugu au nyumba ya familia.

Au ana maisha ya kawaida sana. Mtu aseme daladala bora kuliko starlet, daladala hizi hizi za Dar, ujikute uko Morocco saa tisa alasiri kwenda mbele unataka kwenda Mbezi, Temeke au Mbagala.

Chuma zinakuja zimejaa, raia wanagombea mpaka wanajitoa akili, humo ndani ukute wamepanda vichaa fresh watatu wanazozana.

Dereva mla bangi anapiga singeli na miziki usiyoipenda sauti ya juu na sound haina quality.

Umesimama hauna siti,pembeni yako mlevi asiejitambua kila saa anaongea hovyoo unapambana na harufu ya pombe mixer hapigi mswaki🤣.

Kulia kwako kuna Mama hajiwezi stamina kachoka na watu hawamwachii siti anakugeuza nguzo anakuegemea. Na wewe uko hoi umechoka🤣.

Ukicheki pembeni kuna mtu yuko peke yake ktk ki starlet chake, hasimami vituoni taa zikiruhusu anaserereka.

Ni kweli kina sura haivutii(body) na ni ya zamani. Lakini haiondoi fact inarahisisha movement.

Bora mwanao umpeleke shule na starlet kuliko ku risk unampakia bodaboda, au dala dala mwendo mrefu. Watoto wangapi tunawakuta kala mia mbili ya nauli, anakusalimia anaomba umlipie😥, au konda anasamehe lakini kwa masimango unhealthy kwa mtoto.

NIMESIKITIKA SANA
 
Mods fanyeni review ya huu uzi na muufute hauna maana.
 
Starlet inauzwa karibuni wateja
20231023_115410.jpg
 
Kwani mtoa mada unapendekeza watu wawe na magari ya aina gani boss, na yapi kwako ni kichekesho au ni hiyo Starlet peke yake?
 
Kwa sasa hizo ndiyo gari za kumiliki na hizo bei mafuta zulivyo juu.
 
Back
Top Bottom