Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Unaweza kuwaita chawa,wanaa,wambeya na jina lolote fanani nalo.
Picha hapo juu ni Mwijaku na Baba Levo vijana maarufu kwa sasa hapa Tanzania hasa kwenye tasnia ya sanaa.
Kinachonivutia kwao ni namna wanavyoisaka shilingi pasi na kujali kuitwa majina tajwa hapo juu bali wao wanajali kinachoingia baada ya!
Binafsi naona biashara yao ya uchawa inawalipa hasa ukizingatia kwa sasa makampuni mengi makubwa yanawahitaji kufanya nao kazi kueneza sifa zake.
Nawaona ni watu waliofanikiwa sana kiuchumi hapo baadae kwa kupitia uchawa wao.