super hero1
JF-Expert Member
- Jul 27, 2024
- 2,339
- 1,888
Sabaya alienda jela ILA Makonda akateuliwa kuwa Mwenezi then RCYaani nchi hii kwa Sasa inasikitisha sana. Yaani ccm kimekuwa chama Cha manyangany'i na mafisadi ya taifa hili.
Kupitia kuwa mwanachama wa CCM, waziri, katibu mkuu, mkuu wa shirika, mkurugenzi wa halmashauri, rais wa nchi anaweza kuamua kuiba mali (rasilimali ) yoyote ya watanganyika na Bado akawa juu ya Sheria, hakuna Cha kumtisha zaidi ya kivuli Cha kifo chake pekee😫😫.
Wezi na mafisadi ya nchi hii, kwa Sasa yanaiba kwa urefu wa kamba zao maana rais wa nchi alishawaruhusu, yanaiba Hadi haki ya wazee, yatima na wajane wa taifa kwa maslahi Yao binafsi bila huruma yoyote.
Report za CAG zipo Kila mwaka Zina wizi mpya lakini hakuna anayethubutu kumuwajibisha mwingine kwa sababu mfumo mzima kuanzia juu Hadi chini kwenye serikali za mitaa ni wizi TU na kubambikia raia wema makosa na Kodi zisizo na kichwa Wala miguu.
Kwa mfano serikali ilikuwa na haja Gani kuteketeza zaidi ya billion 250 kwa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 ingali inataka viongozi wa CCM pekee ndio waibuke washindi?
Hizo billion 254.82 SI Bora zingepelekwa kwenye ruzuku ya umeme ili kupunguza gharama za kununua umeme au maji?
Kwa mfano serikali hii inasititiza matumizi ya nishati safi kwenye makaratasi na sio kwenye uhalisia, Kuna haja Gani unit 2.8 za umeme kunuliwa kwa tsh 1000 wakati vyanzo vya umeme kwa Sasa vimeongezeka nchini kwetu?
Hizo billion 254.82 SI Bora zingeruzuku gharama tanesco ili Sasa mwananchi wa TANZANIA kwa tsh 1000 apate angalau unit 5 za umeme kuliko hivi Sasa anapata unit 2.8? Serikali haioni kwamba hii itakuwa chachu ya wananchi wengi kuhamia kwenye nishati safi ya kupitia na viwanda vingi vidogo vitaanzishwa nchini kwetu na hivyo kusaidia kukuza hali na uchumi wa mtanzania mmoja mmoja?
Lakini Cha ajabu pesa hizo zimepotea Bure kwa maagizo ya waziri wa tamisemi kukata majina ya wapinzani Hadi kuua baadhi ya viongozi kisa TU nafasi za mwenyekiti wa mtaa!
Sasa kwa maagizo kama hayo na upotevu wa pesa za watanganyika kiasi hicho nani anayefanya makosa ya uhaini kwenye taifa hili?
CCM muelewe Tundu Lissu ni mjumbe wetu sisi wananchi juu ya Yale yote yatukwazayo ambayo ninyi mnayaendekeza na kulindana, msiposikiliza ujumbe wa Tundu Lissu mkadhani kumuweka rumande mtamkomesha, eleweni Tundu Lissu sio saizi yenu yeye alishapitishwa kwenye tanuri ya moto na akatoka salama.
Sina hakika endepo wenye nchi (wananchi ) wataamua kuwapitisha ninyi wezi na mafisadi ya taifa hili mnaolindwa na mifumo mibovu ya uchaguzi na kuteuana kama mtahimili maumivu hayo.
Kama mmeamua kufumbia macho kesi za UAHINI wa wezi na mafisadi ya CCM yanayo sababisha umasikini na dhiki kwa watanzania wengi, tunaomba Tundu Lissu atoke rumande mara moja.
Tukitaka kufatilia kwa undani zaidi juu ya kesi za UAHINI nchi hii viongozi wengi wa serikali (mawaziri) ndio wanapaswa wawe rumande muda huu. Hivyo wezi na mafisadi hayana uhalali wa kumtuhumu Tundu Lissu kwa jambo lolote lile zaidi waanze kutoa maboriti kwanza kwenye macho Yao.
Double Standards