Wanaopinga bandari kubinafsishwa ni mafisadi wanaogopa mirija kuzibwa na kukatwa au ni wadini?

Yafanyiwe kazi yafuatayo;
1. Mda wa mkataba usizidi miaka 10 na iwe renewable
2. Apewe bandari moja au mbili na sio kupewa bandari zote za nchini
3. Akubali tusuluhishe mahakama za ndani kama mmojawapo akizingua
4. Kiwekwe kipengele cha kuvunja mkataba endapo itabidi
Bado matatizo yapo, hii partnership inawekwaje??

1. Wao wanasika na kushusha kupakia mizigo tu, mambo ya ushuru, ulinzi na usalama wanatuachia sisi!!

2. Kazi zote zinazoweza kufanywa na wabongo waaachie wabongo.

3. Malipo kwa wafanyakazi yawe ya kueleweka

4. Watakaokosa kazi walipwe fidia.
 
Miaka kumi kwa biashara ya bandari naona ni michache sana yaani mtu alete mifumo ya maana ya mabillioni halafu mkataba miaka kumi...hivi anakuwa hata kasharudisha mtaji?
Ungekuwa wewe ungekubali mgogoro wako na serikali utatuliwe katika mahakama ambazo jaji anateuliwa na mkuu wa nchi na wakati Kuna mahakama za kimtaifa za utatuzi wa migogoro ya kibiashara.
Halafu nimeona kama ni partnership kwa hiyo Kuna role Kila mmoja atafanya.
Mengine nakuunga mkono...mkataba gani usiovunjwa ila viongizi wetu utadhani hawakufika darasani.
Obviously kuna kipengele atakuwa ameainisha kwamba atakuwa na performance nzuri kuendeleza bandari so mtaji na faida vitakuwa vimeingia.

Miaka kumi siyo michache ule wakati wa kuwapa favour watu wafanye kazi kuchuja hasara na faida hizo zama zimeisha mtu anaona kazi anaiweza afanye hawezi apewe mwengine.
 
Tunaenda kuongeza mapato, na kuongeza ufanisi kwa ujumla wake
Sasa kupinga bila sababu za msingi na kukazania na uzushi tuuu hii inaleta ukakasi,

Kama ni mapungufu si tuyarekebishe tu?
Kwanini kumkataa mwarabu moja kwa moja?
Angekuwa mzungu tungepinga?
Nini kinasababisha kusiwe na ufanisi?
 
Bado matatizo yapo, hii partnership inawekwaje??

1. Wao wanasika na kushusha kupakia mizigo tu, mambo ya ushuru, ulinzi na usalama wanatuachia sisi!!

2. Kazi zote zinazoweza kufanywa na wabongo waaachie wabongo.

3. Malipo kwa wafanyakazi yawe ya kueleweka

4. Watakaokosa kazi walipwe fidia.
Very well done, haya ndio tunata kusikia
Big up
 
Obviously kuna kipengele atakuwa ameainisha kwamba atakuwa na performance nzuri kuendeleza bandari so mtaji na faida vitakuwa vimeingia.

Miaka kumi siyo michache ule wakati wa kuwapa favour watu wafanye kazi kuchuja hasara na faida hizo zama zimeisha mtu anaona kazi anaiweza afanye hawezi apewe mwengine.
Muda itategemea anawekeza kiasi gani kwa hiyo si rahisi kusema miaka kumi mpk kuona plan yake...kweli Ile ujinga wa kuwapa watu miaka mitano ya kujaribu umepitwa...ila naona siku hizi watz wamekuwa macho watu wamecharuka balaa japo na uongo nao mwingi.
 
Mimi binafsi sijui mambo ya Sheria .....

Namsubiri mwanasheria mkuu wa serikali aongee neno nami nielewe.
 
Mkataba upo wazi na utajadiliwa bungeni tarehe 10 /6
Tutege masikio na ikibidi tushiriki,kushauri na kukosoa
Lengo ni zuro ila mafisadi wanaogopa mirija kuzibwa
Kitu ambacho nina uhakika na DPWorld upigaji utaisha kwenye Bandari ya salama.
 
Yafanyiwe kazi yafuatayo;
1. Mda wa mkataba usizidi miaka 10 na iwe renewable
2. Apewe bandari moja au mbili na sio kupewa bandari zote za nchini
3. Akubali tusuluhishe mahakama za ndani kama mmojawapo akizingua
4. Kiwekwe kipengele cha kuvunja mkataba endapo itabidi
Hapo tu ati.
 
Tunaenda kuongeza mapato, na kuongeza ufanisi kwa ujumla wake
Sasa kupinga bila sababu za msingi na kukazania na uzushi tuuu hii inaleta ukakasi,

Kama ni mapungufu si tuyarekebishe tu?
Kwanini kumkataa mwarabu moja kwa moja?
Angekuwa mzungu tungepinga?
mafisadi ya ccm yameiba pesa za umma yakamaliza yameona yaanza kupora na mali asili.
 
Miaka kumi kwa biashara ya bandari naona ni michache sana yaani mtu alete mifumo ya maana ya mabillioni halafu mkataba miaka kumi...hivi anakuwa hata kasharudisha mtaji?
Ungekuwa wewe ungekubali mgogoro wako na serikali utatuliwe katika mahakama ambazo jaji anateuliwa na mkuu wa nchi na wakati Kuna mahakama za kimtaifa za utatuzi wa migogoro ya kibiashara.
Halafu nimeona kama ni partnership kwa hiyo Kuna role Kila mmoja atafanya.
Mengine nakuunga mkono...mkataba gani usiovunjwa ila viongizi wetu utadhani hawakufika darasani.
Yaap kama kutakuwa na kesi naungana nawe, kwamba zitumike Mahakama za kimataifa na sio za bongo zenye majaji wateule wa Rais....
 
Kiusalama haiko poa kubinafsisha bandari , tatizo letu lipo kwenye role inforcement, Hao mnaowaita mafisadi wangekuwa wanakula shaba tu na Kunyongwa mnona bandari ingefikia huo ufanisi tena hata zaidi ya hizo 233+.

Mnaweka rehani nchi kisa Fisadi wa Kutoka kijiji furani ataiba/kaiba, zimwi likujualo halikuli kukumaliza, hawa tungedili nao tu humu humu ndani kuliko huu upuuzi wa Milele.
 
Miaka kumi kwa biashara ya bandari naona ni michache sana yaani mtu alete mifumo ya maana ya mabillioni halafu mkataba miaka kumi...hivi anakuwa hata kasharudisha mtaji?
Ungekuwa wewe ungekubali mgogoro wako na serikali utatuliwe katika mahakama ambazo jaji anateuliwa na mkuu wa nchi na wakati Kuna mahakama za kimtaifa za utatuzi wa migogoro ya kibiashara.
Halafu nimeona kama ni partnership kwa hiyo Kuna role Kila mmoja atafanya.
Mengine nakuunga mkono...mkataba gani usiovunjwa ila viongizi wetu utadhani hawakufika darasani.
Mbona unamsemea huyo mwekezaji?
Yeye mwenyewe ataongea akiona haitoshi!
Ni issue ya negotiation tu!
Ila serikali yetu iweke offer ya miaka 10
 
Mimi sipingi Bandari kukodishwa na Dubai ports World wasi wasi wangu ni mkataba huenda ukawa ni ilie ile mikataba mibovu ambayo Serkali ya CCM huingia miaka yote.

Mikataba ya akina Mangungo na Mkoloni.
Yaani huna uhakika,unapayuka kwa kitu usokijua!!..wabongo bana!!
 
Back
Top Bottom