Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Sijaona kama una hoja nyingine zaidi ya hii. Kifupi ni kuwa padri wala mchungaji HANA NA HATAKUWA NA UWEZO WA KUMWONDOLEA MTU DHAMBI. Ni Mungu pekee anafanya hilo. Sema binadamu wanahiaji utukufu waweze pata sababu ya kupewa sadaka na kicho. Sijui hata kama unaweza elewa kiswahili hiki chepes hivi.

Usisome Biblia kwa kurukaruka....
 
Sijaona kama una hoja nyingine zaidi ya hii.
Ipi hiyo ..?? Hoja kuu na majibu yote yapo kwenye uzi..

Kifupi ni kuwa padri wala mchungaji HANA NA HATAKUWA NA UWEZO WA KUMWONDOLEA MTU DHAMBI.
Kwanini iwe kifupi...? Kwanini unaifunga akili yako kuizuia kujifunza zaidi na zaidi....

Inamaana unaenda kinnyume na maneno ya Yesu alipowaachia Mitume uwezo huo wa Kuondolea zambi...??

Ni Mungu pekee anafanya hilo.
Ni kweli kabisa.....ila ni kwa kupitia Mapadre....

adamu wanahiaji utukufu waweze pata sababu ya kupewa sadaka na kicho. Sijui hata kama unaweza elewa kiswahili hiki chepes hivi.
Na kuelewa sana....kudhihirisha kuwa nakuelewa jibu maswali niliyokuuliza
 
Msiabishe hizo elimu mlizopata japo kidato cha nne..

Umeshindwa kung'amua lugha mbili za kigiriki na Kilatini
Lugha si hoja, Biblia ninayosoma mimi hakuna sehemu iliyoandikwa Yesu kristu sasa sijui natumia biblia yenye lugha ya kilatini au kigiriki. Umeshawahi kujiuliza kwa nini wakatoliki hawatumii neno kristo wanatumia kristu kama makanisa mengine hata kama neno hilo lina maana moja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una uhakika na hiki ulichoandika...??


Ni sawa kabisa....Mungu abasamehe kupitia kwa Padre

Wakati wa agano la kale waisraeli walikua wakikosea wanaenda kwa nabii kumweleza awaombee msamaha kwa Mungu. Elewa sio nabii anayewaondolea dhambi bali alikua anawaombea msamaha lakini pia ukumbuke haikua sheria kwamba ni lazima uje kwa nabii akuombee usamehewe, walikua wanaangalia nani yupo karibu na Mungu ndio waombee msamaha kwa sababu wao walikua wanajiona wakosefu.

Wakati wa agano jipya baada ya ujio wa Yesu toba na kila kitu wanaomba watu wenyewe na Yesu lekee ndiye anayesamehe dhambi. Ili andiko liende kwa udhibitisho onyesha sehemu Yesu alipotoa maagizo kwamba watu waende kuungama dhambi zao kwa mitume ili wasamehewe. Onyesha mfano ni wapi mtume petro au paulo au yoyote yule walisamehe mtu dhambi? Agano jipya mchungaji anakuongoza sala ya toba na unakiri kwa kinywa chako mwenye ila jukumu la kusamehe dhambi sio lake.
 
Umeshawahi kujiuliza kwa nini wakatoliki hawatumii neno kristo wanatumia kristu kama makanisa mengine hata kama neno hilo lina maana moja?
Mimi ni mkatoliki...Na maneno yote hayo yanatumika sana tuu....


Sasa sijui waongelea wakatoliki gani..???

Muwe mnatendea haki elimu zanu...mambo mengine mnavyoandika ni mpaka aibu yani...

Mnatia aibu....
 
Hamuelewi maana ya mtu kupewa mamlaka. Mamlaka ya kusamehe dhambi hayafutwi na dhambi ya mhusika.

Padre anapokuwa katika dhambi hiyo inabakia yeye na nafsi yake lakini wewe unayekwenda kwake unapata neema ile ile ya kimamlaka.

Mfano mzuri ni Rais wa nchi, akifumaniwa akizini hakuondoi mamlaka yake ya kuamuru jeshi kuingia vitani au amri yoyote ya kisheria.

Kama Mapadre wangekuwa wanafanya hayo kwa mamlaka yao basi tungeweza kwanza kuhesabu maovu yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaiyo mkuu unavyosema ata padri akiwa ni mtenda dhambi wewe ukienda kutubu unasamehewa bila kujali matendo ya padri sasa nikuulize swali unaweza kuchota maji masafi kwenye ndoo chafu na ukapata maji masafi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
padri ndo nani kwenye wokovu wa mwanadamu
Ni kuhani...ndiye aliyepewa mamlaka ya kufundisha neno la Mungu ili watu waupate uzima wa milele...

Pia ndiye aliyepewa mamlaka ya Kusamehe dhambi kupitia kwa Yesu Kristo
 
Mimi sio mkatoliki na hata ningekuwa mkatoliki kamwe nisingekwenda kwa binadamu/Padri mwenye mwili wa nyama kama wangu kuungama dhambi.
 
Nitaipinga hoja yako mkuu kupitia kipengele chako cha mada chenye maneno "Historia ya maungamo ya dhambi katika agano la kale"

Nianze kwa kukupa history kidogo. Mara baada ya anguko la Adamu na Hawa pale Eden Mungu alikuwa ameshaanda mpango wa wokovu wa Mwanadamu ndiyo maana utaona kuna mnyama alichinjwa pale ili wapate nguo za kuficha uchi wao lkn halikuwa lengo hasa Ila alichinjwa ili awe mbadala wao kwa dhambi walizotenda ndiyo maana hawakufa kama sheria isemavyo ya mshahara wa dhambi ni mauti.

Kutokea hapo utaona ibada za kafara kupitia wanyama zikianza kwa kila aliyekuwa akitenda dhambi na hata habari ya ukuhani pia baadaye hema ya kukutania ilipoanzishwa katika kitabu cha kutoka 25 agizo la ujenzi wa hema hiyo lilipotolewa.

Katika ujenzi ule Mungu anamwambia musa kuwa hema ile itakuwa mfano wa ile ya mbinguni kwa hiyo note hata mbinguni kuna huduma ya upatanisho kupitia kuhani

Turudi kwa mada hema ya kukutania Ilikuwa na sehemu kuu tatu uwa wa nje, patakatifu na patakatifu pa patakatifu ambapo ktk uwa wa nje ndiyo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa ambapo mdhambi alitwaa kondoo kama mbadala wake na kwenda naye kwa kuhani ambaye aliact kama mpatanishi baina ya mwanadamu mdhambi na Mungu ambapo aliungama dhambi zake kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha kondoo kama namna ya kuhamisha dhambi kutoka kwake kwenda kwa kondoo kisha alimchinja na kuhani kukinga damu na kuingia nayo kwenye chumba cha pili cha patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho wakati kondoo akiteketezwa katika ua wa nje huu ndiyo ulikuwa utaratibu wa wokovu ulioandaliwa na Mungu kabla ya Kristo kuja duniani

Baada ya Kristo na kufa kama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu yohana 1:29 na kufa pale msalabani habari za kwenda kuungama kwa kuhani zilikoma au huduma za kikuhani na utoaji kafara ulikwisha maana huduma ile ilikuwa kivuli kumuwakilisha Kristo na sasa Kristo ameshakuja hakuna haja tena kwenda kwa mwanadamu kuungama wakati Kristo yupo

Kwa hiyo hoja yako ya kuungama kwa padri ni kutaka kuturudisha kwa huduma ya kikuhani ya mwanadamu ambayo ni hatari sana maana unapinga kwamba Kristo bado hajafa kwa ajili ya dhambi na wewe unageuka kuwa mpinga Kristo

Leo hatuna haja ya kuungama kwa mwanadamu tena maana tunaye Kristo mwombezi wetu kuhani asiyepatikana na mauti anayehudumu ktk hekalu lisilofanywa kwa mikono ya mwanadamu huyo pekee astahili kutuombea msamaha kwa Mungu Baba na si mwingine yoyote
Umemjibu vema mleta uzi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kuhani...ndiye aliyepewa mamlaka ya kufundisha neno la Mungu ili watu waupate uzima wa milele...

Pia ndiye aliyepewa mamlaka ya Kusamehe dhambi kupitia kwa Yesu Kristo

acha kukalili nioneshe wapi alipo pewa hayo mamlaka ya kufundisha na kusamehe na uo ukuhani
 
1. Ndio kule kule tunakokusema kwamba waprotestanti wanasoma maandiko Matakatifu kwa kurukaruka na ni wapinga Kristo.

2. Mtu anakataa nyama ya Nguruwe ikiwa imekaangwa lakini anakubali ikiwa katika mfumo wa Unga kwenye kopo.Au mtu anakataa Pombe kwenye Chupa ya Serengeti lakini anakubali kuwekewa kwenye mwili wake na daktari akiwa anachukuliwa damu au baada ya. Au mtu anaikataa Pombe lakini anaikubali awekewe ndugu marehemu wake Mochwari ili mwili wake usioze. Kama Padri hana uwezo wa kuwaondolea dhambi kwa sababu sio Mungu basi, vile vile hana uwezo uwezo wa kuwaondolea dhambi kwa njia ya ubatizo. Na kuanzia sasa wapange foleni wamusubirie Mungu awabatize au wawe wanajibatiza wenyewe vyumbani kwao.
Umeandika nin? Nakushauri soma biblia ndugu uelewe kwa msaada wa Roho Mtakatifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom