Mutha007
Senior Member
- May 27, 2018
- 166
- 345
we jamaa, Yesu sio binadamu.1. Kwa hiyo umeambiwa Binadamu hawezi kuondoa dhambi? Kajisomee
Zaidi ya Yote, Marko 2:5-10. Baadhi ya watu walipotilia shaka suala la Yesu katika ubinadamu kuwaondolea watu wengine dhambi, Yesu aliwathibitishia kuwa mwana wa mtu anao uwezo huo wa kuondoa dhambi za walimwengu:
“5Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza,“Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.” 6 Baadhi ya waalimu wa sheria waliokuwa wameketi hapo wakawaza mioyoni mwao, 7 “Anathubutuje kusema hivyo? Anamkufuru Mungu! Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake.” 8 Yesu alitambua mara mawazo yao, akawaambia, “Mbona mnawaza hivyo mioyoni mwenu? 9 Ni lipi lililo rahisi zaidi: Kumwambia mtu huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kumwambia, ‘Inuka! Chukua mkeka wako utembee?’ 10 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anayo mamlaka ya kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, 11 “Nakuambia simama; chukua mkeka wako uende nyumbani!”
2. Vile vile, kupitia Luka 5:24, tunaelezwa pia kwamba katika suala la uwezo wa Yesu kuwaondolea watu dhambi alifanya hivyo katika ubinadamu wake na sio kwa ule Umungu wake.
3. Mwinjili Matayo tena katika sura ile ya 18:15-20, anatudokeza jinsi Yesu kabla ya kuwapatia Mitume rasmi uwezo wa kuondolea watu dhambi, alipata kuwadokeza jambo hilo.Uwezo wa kufunga na kufungua ndio kule kuwaondolea watu adhabu za muda mfupi, zitokanazo na dhambi:
“15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.18 Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”
unazingua shekhe
Sent using Jamii Forums mobile app