Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Status
Not open for further replies.
Kwanza hiyo nyekundu, hapa hatuzungumzi kwa ajili ya nani ana hasirana nani bali mantiki ya hichi kinachozungumzwa.
Wewe mwenyewe kama ni mwislamu, unaijua dini yako na katika familia yako mnaitekeleza, utaelewa kuwa pamoja na kuwepo kwa Sheria ya Ndoa ya 1971 uliyoitaja, bado waislamu wanapotaka kuwagana mirathi, wanagawana wenyewe kwa mujibu wa sheria zao za mirathi na sina kumbukumbu za mirathi hiyo kutenguliwa mahakamani. Inawezekana zipo kesi zilizofikishwa mahakamani kwa mmoja wa mwanafamiliakuhisi ana haki ya fungu kubwa zaidi.

Kwa kuwa hapa umetaja Mahakama ya Kadhi kwa ajili ya Mirathi tu, binafsi nahisi Sheria za Mirathi za Kiiislamu ni kandamizi. Mfano, ikiwa katika famillia kuna watoto hao uliowataja 5:4:3, kati ya hao 12 mwanamume ni mmoja tu wa kiume, tena wa mwisho kabisa, basi sheria inampa fungu kubwa zaidi huyu mwanamume kushinda dada zake 11. Ninaheshimu lakini hapa hainiingiii akilini. Je mnataka sheria ili kuwakandamiza wanawake?

Jengine ni kuwa Serikali haipaswi kuunda Mahakama na kuigharimia kwa pesa za walipa kodi wote. Nafikiri unaelewa kuwa katika jamii ya waislamu wana kitgno chao cha Wakfu na huko ndio humalizana. Ikiwa ni kwa ajiliya mirathi, mahkama ya kadhi ni ya nini?
 
Najaribu kufuata majadiliano.Pamoja na mimi kuwa ndani ya imani inayodai mahakama ya Kadhi, mwenzenu sioni kama tuko wengi tunaoona faida yake kwa sababu hatufuati hata hizo sharia zenyewe zinavyotaka.Mi staki nikose uhuru wa kuchagua nataka kutumia utaratibu gani kuamua mambo yangu.Niliona ndugu yangu alivyonyanyaswa na hao hao viongozi wetu pale mumewe alipompa talaka 2 za kumkomoa kusudi tu asiolewe tena.Ilibidi tumwekee lawyer, akapeleka kesi mahakamani na huko akapata haki yake.Ndoa ikavunjwa kiserikali.Akawa huru kuishi maisha yake.Spati picha kama ndo Kadhi kaamua na uamuzi ukawa mwisho.Angeliaje?
 

Natamani Tropical aijibu hii hoja kiintelekcho na si kurukr ruka
 

Hili nalo neno!
Inawakandamizeni, uongo?
 
Ninachosema mimi ni kwamba mambo ya ibada inabidi yabaki kuwa ...!
Hapana, sicho ulichosema. Ulidai kwamba madhehebu mengine ya dini yanaweza ku enforce sheria zao bila kusaidiwa na serikali. Ukaulizwa, how?

Wataliki wa ndoa wakigombania mali, kwa mfano, mahakama ya kanisa au ya msikiti ikiamuru mali za ex-husband ziwe seized apewe ex-wife na watoto, kanisa lita enforce vipi hiyo amri? Unaweza kujibu hicho kitu au ulijitamkia tamkia tu?

Ni kwanini waislamu hawawezi ku enforce laws zao wenyewe za kiibada kwenye mahakama zao mpaka wasaidiwe na serikali lakini madhehebu mengine ya dini yanaweza?
 
Umekasirika na umeandika kwa hasira..sijaona unataka kusema nini?? please andika tena ukiwa umetulia ..just intellectual arguments..

Nimeandika kwa hasira au umesoma kwa hasira kiasi umeshindwa kupata kitu? Wewe huna jeuri ya kuniudhi mimi kwa kuwa mimi ni mjuvi wa kucheza na minds za watu wenye mawazo finyu. Kilichokufanya ushindwe kuelewa nilichokiandika ni itikadi yako ya ubishi wa kijahidina. Badala ya kuzama kwenye nini nimeandika, wewe umesoma haraka haraka ili uwahi kubisha.

Rudia kusoma bila hasira utaona tu unaelewa. You are possessed by what you want. Kwa kifupi huna sera zaidi ya ubishi, unaandika huku machozi yanakulenga lenga sababu ya kuamini upo sahihi kumbe unachekesha
 

Enforcement ya jambo la imani ni kwa misingi ya imani. Unajua shida yenu ni kwamba kuna tabaka la wanaume wasiopenda kufanya kazi ambao wanatafuta namna ya kudhulumu wajane (wake za kaka zao) na ndio mnachopigia kelele hapa.

Mimi naamini kwamba, kama ni jambo la ibada basi na muongeze mahubiri ktk hilo ili waumini waielewe vyema concept ya kugawana mali. Ikiwa ibada zenu ni kulazimishana, kuna haja gani ya kuorodhesha mawili tu ya ndoa na mirathi?

Semeni hivi: Tunataka mahakama ya Kadhi ili tuweze kutoa hukumu kwa:-
1. Wanaokwepa kulipa dhaka
2. Wasiochangia watoto yatima
3. Wanaolewa ilhali wao ni waislamu
4. Wanaotafuna kitimoto wkt wanajua allah kakataza
5. Wanaogawa mirathi bila kufuata uislamu na kadhalika.

Yawezekana usinielewe hapa sbb ya hasira, lkn nachojaribu kukwambia ni kuwa, kama mirathi na ndoa ni ibada basi fanyeni kama ibada nyingine hakuna haja haja ya kupelekana mahakamani. Mwenye kuamini uislamu na atagawa mali kiislamu, period. Kwani mja akigoma kufunga ramadhani huwa mnamshitaki kwenye mahakama gani?
 
Msome vizuri Woman of substance ...utaelewa!
Mantiki yangu ilikuwa ni ...huwezi ku enforce mambo ya kiibada kama mtu mwenyewe hataki. Wapo wakatoliki wenye kufuata sheria za kikatoliki za ndoa na wapo wasiofuata... Kama mtu hafuati hizo sheria automatically anakuwa amejitoa kwenye kanisa na Kanisa linampa adhabu inayostahili ndiyo maana hautakuja kusikia hata siku moja Kanisa likiiomba serikali ku enforce sheria zake lenyewe unless kuwe na uvunjifu wa amani. Mambo ya kanisa tunamalizana kanisani period...!Sasa jiulize mtu mwenye uhuru wa kuabudu kitu chochote au kutoabudu kikatiba asipofuata sheria ya dini yake ndiyo chombo cha serikali kimlazimishe afuate sheria za dini yake?
Consigliere alizungumza vizuri...cha muhimu ni kuzingatia mafundisho na miongozo ya ya dini zetu. Kama mtu aki deviate na mahakama ya Kadhi(mnayoiendesha wenyewe) ikashindwa kumrudisha kwenye mstari basi hakuna jinsi ...ndiyo mwisho wa mchezo kwa sababu serikali yetu haina dini!
 
Mkuu hawa jamaa sijui wanaelewa ila hawataki tu kukubali au sijui ni nini...! Tanzania bado tuna kazi kubwa sana!
 

Mkuu, hili swali limeenda shule! Hebu niseme hivi, Wana imani budi waelimishane ili maamuzi yote ya imani wayaheshimu! Wakishindwa hilo ndipo waumini wanatafuta njia mbadala. Hivyo basi sio vyema kwa wakuu wa imani kuomba serkali kumlazimisha mwana imani kuwa muumini safi wa imani husika. Mbona hawamuigi kibwetere kuwaaminisha waumini hadi waliamini upuuzi? Alipewa msaada wa ffu na serkali? Au!
 

Acha niliseme hili japo hawatalipenda. Nafikiri huu ni mpango wa watu wachache wenye nia ya kuwaonea wenzao. Nachokiona ni kuwa huu ugawaji wa mali sio reasonable na ndio maana wanajihami. Ni mpango tu wa vidume visivyofanya kazi kuandaa mazingira ya kuwadhulumu wanawake wajane mali za waume zao wanapofariki. Nasema hivi kwa kuwa, kama mtu hataki utaratibu fulani basi imani yake ktk hilo jambo ni zero. Na cha kushangaza, FUNGA (Ramadhan) ni moja ya NGUZO KUU 5 ZA UISLAMU lkn sijaona wakiomba law inforcement kwenye hilo. Kuna nini kwenye mirathi? Kwani mtu akipungukiwa imani anamkosea Mungu au mwanadamu? Imekuwa kazi ya serikali kumsaidia Allah kuwahukumu watu wake kwa kosa la kutofuata mafundisho ya Allah?
 

Mkuu, hilo nalo Neno!
 
nazani unahitaji kuipitia vzuri probate and administration of estate Act,2002 utapata majibu ya swali lako la mirathi n mengineyo km wakfu nk
 
Mimi ni Mkristo ninayeheshimu sana utaratibu wa Ibada katika Dini ya Kiislamu na Sera zake! Kwangu mimi sioni Kukataliwa juu ya Mahakama ya Kadhi endapo utaratibu Serikali utafuatwa! Bado waislamu watabaki kuwa Ndugu zetu na kamwe hakuna wakututenganisha nao Maana ni Baba zetu Mama zetu Wajomba na Mashangazi na Ni Kaka na Dada zetu!

Umaana wa Mahakama ya Kadhi upo kwa Waislamu na si Wengine! Maumivu ya Kukosa Mahakama ya Kadhi yapo kwa Waislamu, Hivyo ni Haki ya Kimsingi kwa Waislamu na Wakristo! Kama jamii ya Kipagani inavyoona!

Iko Dhana ya Udini na Mfumo wa Kidini unaosumbua vichwa vya Watanzania wengi ambao bado wanakuna vichwa na kutaka kujua ni Lini hasa Wanasiasa wataacha Dini zitumie Mfumo wa Kistaraabu katika Maamuzi yao!

Kadhi kuingia ndani ya Serikali ni Hatari kama ilivyo Katoliki kuingia Ndani ya Serikali hivyo basi ni wakati wetu sote kuacha Mawazo ya Watu yapewe nafasi zaidi katika Mahakama ya Kadhi.

Sisi ni Watanzania na tutabaki kuwa Watanzania! Maana Waarabu wameleta Uislamu huku Wazungu wakileta Ukristo! Swali la Kujiuliza je Wazee wetu walikuwa Hawana Ustraabu walikuwa wanatumia kabla!

Bado Mahakama ya Kadhi ni Muhimu na pia Si Muhimu endapo Ustraabu utatumika!.
 
Msome vizuri Woman of substance ...utaelewa!
Well, alichosema WoS ndio kituko kikubwa zaidi. Kasema enforcement ya hukumu ni kutengwa na kanisa. I mean, I can't help it but this is totally preposterous.

WoS, tumepelekana kwenye kesi ya talaka mahakama ya kanisa, ikaamuliwa wewe upewe custody ya watoto na nikulipe mahela, nikakaidi, mnanihukumu kutengwa na kanisa! Kwanza after all that melodrama kanisani kwenyewe I don't wanna see your face or your big belly, ukinifukuza kanisani umeninyima kunde. Kwa hiyo wataniruhusu niondoke na custody ya watoto na however many thousands or milions nilizohukumiwa nimlipe ex-wife. Naenda usharika mwingine huku naimba Bwana Asifiwe! I mean this is amazingly ridiculous. hahahahahaahaha.... Mahakama gani haiwezi ku enforce maamuzi yake?


na wasioridhika wamepeleka rufaa hadi Vatican - MAKAO MAKUU YA KANISA KATOLIKI....Pale mhusika anapokaidi/kukiuka, basi hutengwa na kanisa.
 

Nadhani hujanisoma vizuri; nimesema Kanisa Katoliki limekuwa na mahakama zake kwa mamia ya miaka; na Tanzania kanisa lina Mahakama zake (zinaitwa canonical courts). Wakatoliki hawahitaji kuomba serikali kuwatungia au kuwaanzishia mahakama kwani tayari mahakama hizo zipo na zinafanya kazi katika majimbo yote Katoliki. Makanisa mengine nayo yana taratibu zao za kujiamulia mambo yao yanayohusiana na ibada na taratibu zao (nadhani hata Waanglikani nao wanazo mahakama kama hizo). Kama zilivyo mahakama za Kadhi, Mahakama za Kanisa zinahusiana na ibada na maisha ya kiimani ya waumini na haki zao. HIvyo, zinaamua mambo ya sadaka, ndoa na hata utendaji wa kanisa. Padre akivuruga sakrament hapelekwi mahakamani; akiacha kufundisha mafundisho rasmi ya kanisa hashtakiwi Kisutu! Anapelekwa kwenye mahakama ya Kanisa na kanisa likimvua upadre hakuna mahakama Kuu ya nchi inayoweza kuingilia kati.

Hapa ndio hoja ilipo - kwanini Waislamu nao wasianzishe mahakama zao? Jibu ni rahiisi - kwa sababu hawana chombo kimoja cha kusimamia maslahi yao. Hakuna chombo kinachoweza kusema kinawakilisha "maslahi ya Waislamu wote". Na kutokana na hilo wanataka kutumia serikali kama mahali pa kusimamia. Kama wangekuwa na chombo kimoja wangeweza kuanzisha mahakama zao. Sasa kushindwa kwao kuwa na umoja si kosa la serikali au Wakristu; ni kosa la viongozi wa Kiislamu kuweza kuunda chombo kimoja.



Wewe sasa hivi wanafanyiwa hivyo kwa sababu sheria hizo mbalimbali zimeingizwa katika sheria za nchi na ni sehemu ya sheria za nchi na mahakamu wetu wanafuata sheria hizo za nchi. Kusema kuwa hawana ujuzi nao si kweli wapo watu wanajifunza mambo hayo na wanafuata mashauri mbalimbali ya Waislamu. Sasa mkiamua kuwa hawataki ziwe sehemu ya sheria za nchi kama ilivyo sasa ni sawa na kuamua kuwa wanataka wawe na za kwao.. well.. hawawezi kula keki na kutaka kubaki nayo!

Kwanini Waislamu wasiunde chombo chao cha kuunda mahakama ya kadhi na wale wanaotaka kukatwa mishahara yao kuchangia hilo; hawawezi kutaka kulipiwa na kodi ya Watanznaia wote halafu mahakama ziwahudumie wao peke yao.

Sijaona mantiki ya waislamu kulipia huduma ambayo serikali inatakiwa kutoa kwa wananchi wake..

Ooh no, serikali haitakiwi kutoa ibada kwa wananchi wote na mahakama ya kadhi ni ibada! Ndio maana kanisa halihudumii mahakama za kanisa kwani haziwahusu Watu wengine. Wakatoliki wanahudumia mahakama zao kama sehemu ya ibada na dini yao kwanini kwa Waislamu iwe tofauti?
 
 

nadhani unapata shida kuelewa jambo jepesi sana; mahakama za kanisa zinakubalika na sheria ya sasa. Serikali inatekeleza maamuzi ya mahakama za kanisa au vyombo vya kidini. Ndio maana ndoa inapofungishwa na shehe inatambulika na serikali. Na talaka ikitolewa kiislamu talaka hiyo inatambulika na serikali. Ni uhuru wa dini. Sasa, serikali inaheshimu dini na maamuzi ya kidini bila kuyatungia sheria nyingine.

Sasa, uamuzi wa mahakama ya kanisa kwa mfano - ukisema kuwa ndoa x siyo ndoa na hivyo kutangaza annulment - uamuzi huo unapelekwa tu kwenye vyombo vya serikali (civil authority) kuregister na kutoka hapo mambo mengine yanafuatia. Mtu ataweza kwenda kwenye mahakama ya kawaida sasa kuonesha kuwa uamuzi wa kanisa au dini umeshafanyika. Sasa hilo tayari linatokea sasa hivi. Serikali tayari ina enforce maamuzi ya taasisi za kidini ikitambua uhuru wa vyombo hivyo kusimamia dini hizo. Serikali haiendeshi harusi za Kiislamu wala za Kikristu; haiwalipi mapadre wanapofungisha ndoa wala Mashehe wanapofungisha ndoa! Inatambua tu mambo hayo once perfromed na kuyaregister.

Hivyo, mahakama ya kadhi haiitaji sheria au upendeleo mwingine wowote. Waislamu wanahitaji kukutana:

a. Kuunda chombo chao cha umoja na kuangalia madhehebu yao mbalimbali
b. Chombo kitakachosimamia uendeshwaji wa mahakama ya kadhi kwa Waislamu wote (ukumbuke hata watu wanaposema 'mahakama ya kadhi' si kwamba wanazungumzia madhehebu yote ya Waislamu. Katika TAnzania yawezekana watu wa madhehebu ya Sunni watakuwa na haki zaidi na labda ni sheria ambazo wao wanazikubali ndio zitatumika; itakuwaje kwa Shia na Ahmadiya?
c. Wakubaliane jinsi ya kufinance mahakama hiyo
d. Wafikishe uamuzi wao kwa serikali ili utambulike rasmi kuwa ni wa chombo cha Kiislamu. Serikali itafuatilia tu maamuzi hayo.
e. Tatizo la mahakama ya kadhi ni kuwa nani ataizuia isihukumu mambo mengine ambayo Sheria ya Kiislamu inayo? Maana kama mahakama ya kadhi inahusika na mirathi na talaka, tunajua kuwa inatumika pia kuweza kuhukumu uhalifu - well kwanini Waislamu wasitake mahakama ya kadhi kamili yenye kuhumu mambo yote ya maisha ya Waislamu? Kwanini watake kuhukumiwa kwenye mambo ya ndoa na mirathi lakini siyo kwenye uhalifu? au hiyo si sehemu ya Ibada?
 
Hapa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, hawa watu wamezoea kukariri hivyo basi hata ueleze vipi hawataelewa zaidi ya walivyokariri


Wimbo ukizoeleka baada ya kurudiwa rudiwa basi huenda itagusa hisia zinazosema " hapa kuna kitu, nisogee au nitulie"
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…