Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Status
Not open for further replies.
Assume wewe ni muislam na una wake watatu na watoto 5:4:3 yaani 12 jumla kwa wake watatu..umefariki

Kwa sheria za ndoa ya 1971; ugawaji wa urithi huo hauwezekani japo muislam huyu aliruhusiwa kuoa kiislam

Kwanini mali yake isigawanywe kiislam?? tunataka kadhi wawasaidie hao wanawake, watoto kuhusu mgawanyiko wa mali ya muumini huyu.. siyo voluntarily iwe sheria kabisa na hukumu itolewe na mahakama..ok

Ndio maana tunataka mahakama ya Kadhi..

NB: Naomba wale wenye hasira na uislam na waislamu watuache kwanza tuseme kwanini tunataka mahakama ya kadhi ili mtuelewe
Kwanza hiyo nyekundu, hapa hatuzungumzi kwa ajili ya nani ana hasirana nani bali mantiki ya hichi kinachozungumzwa.
Wewe mwenyewe kama ni mwislamu, unaijua dini yako na katika familia yako mnaitekeleza, utaelewa kuwa pamoja na kuwepo kwa Sheria ya Ndoa ya 1971 uliyoitaja, bado waislamu wanapotaka kuwagana mirathi, wanagawana wenyewe kwa mujibu wa sheria zao za mirathi na sina kumbukumbu za mirathi hiyo kutenguliwa mahakamani. Inawezekana zipo kesi zilizofikishwa mahakamani kwa mmoja wa mwanafamiliakuhisi ana haki ya fungu kubwa zaidi.

Kwa kuwa hapa umetaja Mahakama ya Kadhi kwa ajili ya Mirathi tu, binafsi nahisi Sheria za Mirathi za Kiiislamu ni kandamizi. Mfano, ikiwa katika famillia kuna watoto hao uliowataja 5:4:3, kati ya hao 12 mwanamume ni mmoja tu wa kiume, tena wa mwisho kabisa, basi sheria inampa fungu kubwa zaidi huyu mwanamume kushinda dada zake 11. Ninaheshimu lakini hapa hainiingiii akilini. Je mnataka sheria ili kuwakandamiza wanawake?

Jengine ni kuwa Serikali haipaswi kuunda Mahakama na kuigharimia kwa pesa za walipa kodi wote. Nafikiri unaelewa kuwa katika jamii ya waislamu wana kitgno chao cha Wakfu na huko ndio humalizana. Ikiwa ni kwa ajiliya mirathi, mahkama ya kadhi ni ya nini?
 
Najaribu kufuata majadiliano.Pamoja na mimi kuwa ndani ya imani inayodai mahakama ya Kadhi, mwenzenu sioni kama tuko wengi tunaoona faida yake kwa sababu hatufuati hata hizo sharia zenyewe zinavyotaka.Mi staki nikose uhuru wa kuchagua nataka kutumia utaratibu gani kuamua mambo yangu.Niliona ndugu yangu alivyonyanyaswa na hao hao viongozi wetu pale mumewe alipompa talaka 2 za kumkomoa kusudi tu asiolewe tena.Ilibidi tumwekee lawyer, akapeleka kesi mahakamani na huko akapata haki yake.Ndoa ikavunjwa kiserikali.Akawa huru kuishi maisha yake.Spati picha kama ndo Kadhi kaamua na uamuzi ukawa mwisho.Angeliaje?
 
Nimependa hizo sehemu nilizo bold.

Mungu ni Imani ya mtu.Wapo wanaoamini, wapo wasioamini.Serikali ya Tanzania haina dini.Kwa msingi huo, serikali isiyo na dini, haiwezi kuwasaidia watu kufuata "amri za Mungu wao, au dini zao".

Kiserikali, kila mtu anao uhuru kuabudu atakacho na atakavyo.Ukiamua kuabudu Ng'ombe kama wanavyofanya baadhi ya watu ruksa! Ukiamua kuabudu nature, ruksa! Ukiamua kumuabudu Mungu wako unayemuamini wewe, ni wewe na Mungu wako.Haiwezi kuwa ni wewe, Mungu wako na serikali! Na hapa ndipo tunaposhindania ( bone of contention).Ni jukumu la kila mwenye dini yake kuabudu humohumo kwenye dini yake bila kuhusisha serikali isiyo na dini.

Kwa wakristo wakatoliki kwa mfano, kwenye masuala ya ndoa - wao wana sheria ya mke mmoja, na hakuna talaka hadi kifo kiwatenganishe! Hapo hapo, sheria za nchi zinaruhusu talaka.Wapo wakatoliki chungu mzima ambao wameenda mahakamani kudai talaka na hii ni kinyume kabisa na sheria za kikatoliki za ndoa. Kinachofanyika kwa mtu kama huyu, ni kwamba kanisa halitambui hiyo, na pia hawezi tena kufunga ndoa kanisani. Hatujawahi kusikia hata mara moja, wakatoliki wakiidai serikali ianzishe mahakama za kanisa ndani ya mfumo wa serikali.Wenyewe wanao utaratibu wao wa kufuata katika maswala yao, na hata kesi kama hizi, wanafuata hizo taratibu kivyao bila kuingiza dini nyingine maana kwa kufanya hivyo itakuwa kuingilia uhuru wa imani za wengine na hii ni kinyume na uhuru wa mtu binafsi chini ya katiba.Mara ngapi tunasikia pingamizi kanisani kwa mtu anayetaka kufunga ndoa na huku pale ambapo ametenda kinyume na matakwa ya sheria za kikristo katoliki? Ndio utaratibu, na wasioridhika wamepeleka rufaa hadi Vatican - MAKAO MAKUU YA KANISA KATOLIKI..Hii yote ni nje ya mfumo wa utoaji haki wa Serikali. mfumo unaotegemezwa na walipa kodi wote - wakristo, waislam na hata wasio na dini..Pale mhusika anapokaidi/kukiuka, basi hutengwa na kanisa.

Natamani Tropical aijibu hii hoja kiintelekcho na si kurukr ruka
 
Najaribu kufuata majadiliano.Pamoja na mimi kuwa ndani ya imani inayodai mahakama ya Kadhi, mwenzenu sioni kama tuko wengi tunaoona faida yake kwa sababu hatufuati hata hizo sharia zenyewe zinavyotaka.Mi staki nikose uhuru wa kuchagua nataka kutumia utaratibu gani kuamua mambo yangu.Niliona ndugu yangu alivyonyanyaswa na hao hao viongozi wetu pale mumewe alipompa talaka 2 za kumkomoa kusudi tu asiolewe tena.Ilibidi tumwekee lawyer, akapeleka kesi mahakamani na huko akapata haki yake.Ndoa ikavunjwa kiserikali.Akawa huru kuishi maisha yake.Spati picha kama ndo Kadhi kaamua na uamuzi ukawa mwisho.Angeliaje?

Hili nalo neno!
Inawakandamizeni, uongo?
 
Ninachosema mimi ni kwamba mambo ya ibada inabidi yabaki kuwa ...!
Hapana, sicho ulichosema. Ulidai kwamba madhehebu mengine ya dini yanaweza ku enforce sheria zao bila kusaidiwa na serikali. Ukaulizwa, how?

Wataliki wa ndoa wakigombania mali, kwa mfano, mahakama ya kanisa au ya msikiti ikiamuru mali za ex-husband ziwe seized apewe ex-wife na watoto, kanisa lita enforce vipi hiyo amri? Unaweza kujibu hicho kitu au ulijitamkia tamkia tu?

Ni kwanini waislamu hawawezi ku enforce laws zao wenyewe za kiibada kwenye mahakama zao mpaka wasaidiwe na serikali lakini madhehebu mengine ya dini yanaweza?
 
Umekasirika na umeandika kwa hasira..sijaona unataka kusema nini?? please andika tena ukiwa umetulia ..just intellectual arguments..

Nimeandika kwa hasira au umesoma kwa hasira kiasi umeshindwa kupata kitu? Wewe huna jeuri ya kuniudhi mimi kwa kuwa mimi ni mjuvi wa kucheza na minds za watu wenye mawazo finyu. Kilichokufanya ushindwe kuelewa nilichokiandika ni itikadi yako ya ubishi wa kijahidina. Badala ya kuzama kwenye nini nimeandika, wewe umesoma haraka haraka ili uwahi kubisha.

Rudia kusoma bila hasira utaona tu unaelewa. You are possessed by what you want. Kwa kifupi huna sera zaidi ya ubishi, unaandika huku machozi yanakulenga lenga sababu ya kuamini upo sahihi kumbe unachekesha
 
Hapana, sicho ulichosema. Ulidai kwamba madhehebu mengine ya dini yanaweza ku enforce sheria zao bila kusaidiwa na serikali. Ukaulizwa, how?

Wataliki wa ndoa wakigombania mali, kwa mfano, mahakama ya kanisa au ya msikiti ikiamuru mali za ex-husband ziwe seized apewe ex-wife na watoto, kanisa lita enforce vipi hiyo amri? Unaweza kujibu hicho kitu au ulijitamkia tamkia tu?

Enforcement ya jambo la imani ni kwa misingi ya imani. Unajua shida yenu ni kwamba kuna tabaka la wanaume wasiopenda kufanya kazi ambao wanatafuta namna ya kudhulumu wajane (wake za kaka zao) na ndio mnachopigia kelele hapa.

Mimi naamini kwamba, kama ni jambo la ibada basi na muongeze mahubiri ktk hilo ili waumini waielewe vyema concept ya kugawana mali. Ikiwa ibada zenu ni kulazimishana, kuna haja gani ya kuorodhesha mawili tu ya ndoa na mirathi?

Semeni hivi: Tunataka mahakama ya Kadhi ili tuweze kutoa hukumu kwa:-
1. Wanaokwepa kulipa dhaka
2. Wasiochangia watoto yatima
3. Wanaolewa ilhali wao ni waislamu
4. Wanaotafuna kitimoto wkt wanajua allah kakataza
5. Wanaogawa mirathi bila kufuata uislamu na kadhalika.

Yawezekana usinielewe hapa sbb ya hasira, lkn nachojaribu kukwambia ni kuwa, kama mirathi na ndoa ni ibada basi fanyeni kama ibada nyingine hakuna haja haja ya kupelekana mahakamani. Mwenye kuamini uislamu na atagawa mali kiislamu, period. Kwani mja akigoma kufunga ramadhani huwa mnamshitaki kwenye mahakama gani?
 
Msome vizuri Woman of substance ...utaelewa!
Mantiki yangu ilikuwa ni ...huwezi ku enforce mambo ya kiibada kama mtu mwenyewe hataki. Wapo wakatoliki wenye kufuata sheria za kikatoliki za ndoa na wapo wasiofuata... Kama mtu hafuati hizo sheria automatically anakuwa amejitoa kwenye kanisa na Kanisa linampa adhabu inayostahili ndiyo maana hautakuja kusikia hata siku moja Kanisa likiiomba serikali ku enforce sheria zake lenyewe unless kuwe na uvunjifu wa amani. Mambo ya kanisa tunamalizana kanisani period...!Sasa jiulize mtu mwenye uhuru wa kuabudu kitu chochote au kutoabudu kikatiba asipofuata sheria ya dini yake ndiyo chombo cha serikali kimlazimishe afuate sheria za dini yake?
Consigliere alizungumza vizuri...cha muhimu ni kuzingatia mafundisho na miongozo ya ya dini zetu. Kama mtu aki deviate na mahakama ya Kadhi(mnayoiendesha wenyewe) ikashindwa kumrudisha kwenye mstari basi hakuna jinsi ...ndiyo mwisho wa mchezo kwa sababu serikali yetu haina dini!
 
Enforcement ya jambo la imani ni kwa misingi ya imani. Unajua shida yenu ni kwamba kuna tabaka la wanaume wasiopenda kufanya kazi ambao wanatafuta namna ya kudhulumu wajane (wake za kaka zao) na ndio mnachopigia kelele hapa.

Mimi naamini kwamba, kama ni jambo la ibada basi na muongeze mahubiri ktk hilo ili waumini waielewe vyema concept ya kugawana mali. Ikiwa ibada zenu ni kulazimishana, kuna haja gani ya kuorodhesha mawili tu ya ndoa na mirathi?

Semeni hivi: Tunataka mahakama ya Kadhi ili tuweze kutoa hukumu kwa:-
1. Wanaokwepa kulipa dhaka
2. Wasiochangia watoto yatima
3. Wanaolewa ilhali wao ni waislamu
4. Wanaotafuna kitimoto wkt wanajua allah kakataza
5. Wanaogawa mirathi bila kufuata uislamu na kadhalika.

Yawezekana usinielewe hapa sbb ya hasira, lkn nachojaribu kukwambia ni kuwa, kama mirathi na ndoa ni ibada basi fanyeni kama ibada nyingine hakuna haja haja ya kupelekana mahakamani. Mwenye kuamini uislamu na atagawa mali kiislamu, period. Kwani mja akigoma kufunga ramadhani huwa mnamshitaki kwenye mahakama gani?
Mkuu hawa jamaa sijui wanaelewa ila hawataki tu kukubali au sijui ni nini...! Tanzania bado tuna kazi kubwa sana!
 
Hapana, sicho ulichosema. Ulidai kwamba madhehebu mengine ya dini yanaweza ku enforce sheria zao bila kusaidiwa na serikali. Ukaulizwa, how?

Wataliki wa ndoa wakigombania mali, kwa mfano, mahakama ya kanisa au ya msikiti ikiamuru mali za ex-husband ziwe seized apewe ex-wife na watoto, kanisa lita enforce vipi hiyo amri? Unaweza kujibu hicho kitu au ulijitamkia tamkia tu?

Mkuu, hili swali limeenda shule! Hebu niseme hivi, Wana imani budi waelimishane ili maamuzi yote ya imani wayaheshimu! Wakishindwa hilo ndipo waumini wanatafuta njia mbadala. Hivyo basi sio vyema kwa wakuu wa imani kuomba serkali kumlazimisha mwana imani kuwa muumini safi wa imani husika. Mbona hawamuigi kibwetere kuwaaminisha waumini hadi waliamini upuuzi? Alipewa msaada wa ffu na serkali? Au!
 
Msome vizuri Woman of substance ...utaelewa!
Mantiki yangu ilikuwa ni ...huwezi ku enforce mambo ya kiibada kama mtu mwenyewe hataki. Wapo wakatoliki wenye kufuata sheria za kikatoliki za ndoa na wapo wasiofuata... Kama mtu hafuati hizo sheria automatically anakuwa amejitoa kwenye kanisa na Kanisa linampa adhabu inayostahili ndiyo maana hautakuja kusikia hata siku moja Kanisa likiiomba serikali ku enforce sheria zake unless labda kuwe na uvunjifu wa amani. Mambo ya kanisa tunamalizana kanisani period...!Sasa jiulize mtu mwenye uhuru wa kuabudu kitu chochote au kutoabudu kikatiba asipofuata sheria ya dini yake ndiyo chombo cha serikali kimlazimishe afuate sheria za dini yake?
Consigliere alizungumza vizuri...cha muhimu ni kuzingatia mafundisho na miongozo ya ya dini zetu. Kama mtu aki deviate na mahakama ya Kadhi(mnayoiendesha wenyewe) ikashindwa kumrudisha kwenye mstari basi hakuna jinsi ...ndiyo mwisho wa mchezo kwa sababu serikali yetu haina dini!

Acha niliseme hili japo hawatalipenda. Nafikiri huu ni mpango wa watu wachache wenye nia ya kuwaonea wenzao. Nachokiona ni kuwa huu ugawaji wa mali sio reasonable na ndio maana wanajihami. Ni mpango tu wa vidume visivyofanya kazi kuandaa mazingira ya kuwadhulumu wanawake wajane mali za waume zao wanapofariki. Nasema hivi kwa kuwa, kama mtu hataki utaratibu fulani basi imani yake ktk hilo jambo ni zero. Na cha kushangaza, FUNGA (Ramadhan) ni moja ya NGUZO KUU 5 ZA UISLAMU lkn sijaona wakiomba law inforcement kwenye hilo. Kuna nini kwenye mirathi? Kwani mtu akipungukiwa imani anamkosea Mungu au mwanadamu? Imekuwa kazi ya serikali kumsaidia Allah kuwahukumu watu wake kwa kosa la kutofuata mafundisho ya Allah?
 
Mkuu, hilo nalo Neno!
 
nazani unahitaji kuipitia vzuri probate and administration of estate Act,2002 utapata majibu ya swali lako la mirathi n mengineyo km wakfu nk
 
Mimi ni Mkristo ninayeheshimu sana utaratibu wa Ibada katika Dini ya Kiislamu na Sera zake! Kwangu mimi sioni Kukataliwa juu ya Mahakama ya Kadhi endapo utaratibu Serikali utafuatwa! Bado waislamu watabaki kuwa Ndugu zetu na kamwe hakuna wakututenganisha nao Maana ni Baba zetu Mama zetu Wajomba na Mashangazi na Ni Kaka na Dada zetu!

Umaana wa Mahakama ya Kadhi upo kwa Waislamu na si Wengine! Maumivu ya Kukosa Mahakama ya Kadhi yapo kwa Waislamu, Hivyo ni Haki ya Kimsingi kwa Waislamu na Wakristo! Kama jamii ya Kipagani inavyoona!

Iko Dhana ya Udini na Mfumo wa Kidini unaosumbua vichwa vya Watanzania wengi ambao bado wanakuna vichwa na kutaka kujua ni Lini hasa Wanasiasa wataacha Dini zitumie Mfumo wa Kistaraabu katika Maamuzi yao!

Kadhi kuingia ndani ya Serikali ni Hatari kama ilivyo Katoliki kuingia Ndani ya Serikali hivyo basi ni wakati wetu sote kuacha Mawazo ya Watu yapewe nafasi zaidi katika Mahakama ya Kadhi.

Sisi ni Watanzania na tutabaki kuwa Watanzania! Maana Waarabu wameleta Uislamu huku Wazungu wakileta Ukristo! Swali la Kujiuliza je Wazee wetu walikuwa Hawana Ustraabu walikuwa wanatumia kabla!

Bado Mahakama ya Kadhi ni Muhimu na pia Si Muhimu endapo Ustraabu utatumika!.
 
Msome vizuri Woman of substance ...utaelewa!
Well, alichosema WoS ndio kituko kikubwa zaidi. Kasema enforcement ya hukumu ni kutengwa na kanisa. I mean, I can't help it but this is totally preposterous.

WoS, tumepelekana kwenye kesi ya talaka mahakama ya kanisa, ikaamuliwa wewe upewe custody ya watoto na nikulipe mahela, nikakaidi, mnanihukumu kutengwa na kanisa! Kwanza after all that melodrama kanisani kwenyewe I don't wanna see your face or your big belly, ukinifukuza kanisani umeninyima kunde. Kwa hiyo wataniruhusu niondoke na custody ya watoto na however many thousands or milions nilizohukumiwa nimlipe ex-wife. Naenda usharika mwingine huku naimba Bwana Asifiwe! I mean this is amazingly ridiculous. hahahahahaahaha.... Mahakama gani haiwezi ku enforce maamuzi yake?

na wasioridhika wamepeleka rufaa hadi Vatican - MAKAO MAKUU YA KANISA KATOLIKI....Pale mhusika anapokaidi/kukiuka, basi hutengwa na kanisa.
 
Mwanakijiji
a. Wakristo wenyewe watataka mahakama sasa kwa vile waislamu wameomba?? au wanataka sidhani kama itakuwa ni mahitaji yao kwakuwa kutofauta hiyo hukumu za kikristo ni dhambi kwa wakristo..kama ni dhambi then wanaogopa nini kuomba kuanzishwa siku zote?? wala hatujaona huo mfano kwa nchi nyingi za kikristo duniani mbona sijaona hiyo sheria na hukumu zikitumika? kadhi courts ambazo zipo hata kwa nchi za kikristo kwa ajili ya waislamu kwasababu ni ibada...kwa hiyo hoja yako ni uwongo au uchoyo na chuki tu kwa waislam wa Tanzania

Nadhani hujanisoma vizuri; nimesema Kanisa Katoliki limekuwa na mahakama zake kwa mamia ya miaka; na Tanzania kanisa lina Mahakama zake (zinaitwa canonical courts). Wakatoliki hawahitaji kuomba serikali kuwatungia au kuwaanzishia mahakama kwani tayari mahakama hizo zipo na zinafanya kazi katika majimbo yote Katoliki. Makanisa mengine nayo yana taratibu zao za kujiamulia mambo yao yanayohusiana na ibada na taratibu zao (nadhani hata Waanglikani nao wanazo mahakama kama hizo). Kama zilivyo mahakama za Kadhi, Mahakama za Kanisa zinahusiana na ibada na maisha ya kiimani ya waumini na haki zao. HIvyo, zinaamua mambo ya sadaka, ndoa na hata utendaji wa kanisa. Padre akivuruga sakrament hapelekwi mahakamani; akiacha kufundisha mafundisho rasmi ya kanisa hashtakiwi Kisutu! Anapelekwa kwenye mahakama ya Kanisa na kanisa likimvua upadre hakuna mahakama Kuu ya nchi inayoweza kuingilia kati.

Hapa ndio hoja ilipo - kwanini Waislamu nao wasianzishe mahakama zao? Jibu ni rahiisi - kwa sababu hawana chombo kimoja cha kusimamia maslahi yao. Hakuna chombo kinachoweza kusema kinawakilisha "maslahi ya Waislamu wote". Na kutokana na hilo wanataka kutumia serikali kama mahali pa kusimamia. Kama wangekuwa na chombo kimoja wangeweza kuanzisha mahakama zao. Sasa kushindwa kwao kuwa na umoja si kosa la serikali au Wakristu; ni kosa la viongozi wa Kiislamu kuweza kuunda chombo kimoja.

b. Waislamu wa Tanzania wanalipa kodi kama wananchi wengine kuna kuwa na shida gani kuhudumia na pesa za serikali kwakuwa hata sasa kuna kesi za kiislamu katika mahakama za kawaida ambapo hakimu analipwa lakini anahukumu kesi ambazo hana ujuzi nayo??..kazi ya serikali ni kuhudumia wananchi wote kwahiyo hawa waislamu wanaotaka mahakama ya kadhi pesa zao zinatakuwa hizo hizo zinazoenda katika mahakama zetu ..ndio maana nikasema serikali inatakiwa kupeleka kwenye kadhi funds pesa equivalent na kesi ambazo zingeenda mahakama za sasa not otherwise..

Wewe sasa hivi wanafanyiwa hivyo kwa sababu sheria hizo mbalimbali zimeingizwa katika sheria za nchi na ni sehemu ya sheria za nchi na mahakamu wetu wanafuata sheria hizo za nchi. Kusema kuwa hawana ujuzi nao si kweli wapo watu wanajifunza mambo hayo na wanafuata mashauri mbalimbali ya Waislamu. Sasa mkiamua kuwa hawataki ziwe sehemu ya sheria za nchi kama ilivyo sasa ni sawa na kuamua kuwa wanataka wawe na za kwao.. well.. hawawezi kula keki na kutaka kubaki nayo!

Kwanini Waislamu wasiunde chombo chao cha kuunda mahakama ya kadhi na wale wanaotaka kukatwa mishahara yao kuchangia hilo; hawawezi kutaka kulipiwa na kodi ya Watanznaia wote halafu mahakama ziwahudumie wao peke yao.

Sijaona mantiki ya waislamu kulipia huduma ambayo serikali inatakiwa kutoa kwa wananchi wake..

Ooh no, serikali haitakiwi kutoa ibada kwa wananchi wote na mahakama ya kadhi ni ibada! Ndio maana kanisa halihudumii mahakama za kanisa kwani haziwahusu Watu wengine. Wakatoliki wanahudumia mahakama zao kama sehemu ya ibada na dini yao kwanini kwa Waislamu iwe tofauti?
 
Well, alichosema WoS
ndio kituko kikubwa zaidi.

THATSWHATSUP!

Kasema enforcement ya hukumu ni kutengwa na kanisa.

"enforcement" wewe unaielewaje maana huenda uelewa unatofautiana.'Hukumu' unamaanisha nini maana sikutumia neno hilo popote kwa sababu najua uzito wake.

WoS, tumepelekana kwenye kesi ya talaka mahakama ya kanisa, ikaamuliwa wewe upewe custody ya watoto na nikulipe mahela, nikakaidi, mnanihukumu kutengwa na kanisa!
Nijuavyo mimi, kanisa halibehave namna hiyo, haliendeshi mambo yake kwa kutoa maamuzi kama unavyoweka hapa! Kutengwa utatengwa maana umejitenga mwenyewe baada ya kutokufuata sheria za kanisani.

Kwanza after all that melodrama kanisani kwenyewe I don't wanna see your face or your big belly,

Neither do they want to see you im sure kwa sababu kama una arrogance namna hiyo mbele ya viongozi wako wa kiroho hadi unadiriki kuwatukana, sidhani watakuwa na muda na wewe.Fahamu kanisa haliwafanyii waumini wake kama zifanyavyo mahakama za kawaida - ambazo the likes of you who are so full of themselves believe they can buy justice na kukanyaga kila mtu kichwani.

ukinifukuza kanisani umeninyima kunde.
OH REALLY?

Kwa hiyo wataniruhusu niondoke na custody ya watoto na however many thousands or milions nilizohukumiwa nimlipe ex-wife.
Kama una millions kiasi hicho na unakataa hata kuwapa walio na stahili, hufai hata kuhangaisha vichwa vya wateule wa Mungu.Kumbe ulitaka wakufunge kamba usiondoke?!Thats not how the church operates na hapa siyo mahali pake kujadili.Kumbuka hii siyo mada ya "mahakama za kikristo - katoliki bali ni mahakama za kadhi

Naenda usharika mwingine huku naimba Bwana Asifiwe! I mean this is amazingly ridiculous. hahahahahaahaha.... Mahakama gani haiwezi ku enforce maamuzi yake?

Like seriously? You want an answer to this one? Nitakushauri kama una nafasi, basi nenda tembelea mahakama ziwe za mwanzo au wilaya, uone kesi nyingi zilizokwisha na uone kama hizo orders "zimekuwa enforced' ukishakamilisha utafiti huo mdogo ndio uje hapa tujadili hii hoja ya enforceability.Ridiculous is what it is!
 
Well, alichosema WoS ndio kituko kikubwa zaidi. Kasema enforcement ya hukumu ni kutengwa na kanisa. I mean, I can't help it but this is totally preposterous.

WoS, tumepelekana kwenye kesi ya talaka mahakama ya kanisa, ikaamuliwa wewe upewe custody ya watoto na nikulipe mahela, nikakaidi, mnanihukumu kutengwa na kanisa! Kwanza after all that melodrama kanisani kwenyewe I don't wanna see your face or your big belly, ukinifukuza kanisani umeninyima kunde. Kwa hiyo wataniruhusu niondoke na custody ya watoto na however many thousands or milions nilizohukumiwa nimlipe ex-wife. Naenda usharika mwingine huku naimba Bwana Asifiwe! I mean this is amazingly ridiculous. hahahahahaahaha.... Mahakama gani haiwezi ku enforce maamuzi yake?

nadhani unapata shida kuelewa jambo jepesi sana; mahakama za kanisa zinakubalika na sheria ya sasa. Serikali inatekeleza maamuzi ya mahakama za kanisa au vyombo vya kidini. Ndio maana ndoa inapofungishwa na shehe inatambulika na serikali. Na talaka ikitolewa kiislamu talaka hiyo inatambulika na serikali. Ni uhuru wa dini. Sasa, serikali inaheshimu dini na maamuzi ya kidini bila kuyatungia sheria nyingine.

Sasa, uamuzi wa mahakama ya kanisa kwa mfano - ukisema kuwa ndoa x siyo ndoa na hivyo kutangaza annulment - uamuzi huo unapelekwa tu kwenye vyombo vya serikali (civil authority) kuregister na kutoka hapo mambo mengine yanafuatia. Mtu ataweza kwenda kwenye mahakama ya kawaida sasa kuonesha kuwa uamuzi wa kanisa au dini umeshafanyika. Sasa hilo tayari linatokea sasa hivi. Serikali tayari ina enforce maamuzi ya taasisi za kidini ikitambua uhuru wa vyombo hivyo kusimamia dini hizo. Serikali haiendeshi harusi za Kiislamu wala za Kikristu; haiwalipi mapadre wanapofungisha ndoa wala Mashehe wanapofungisha ndoa! Inatambua tu mambo hayo once perfromed na kuyaregister.

Hivyo, mahakama ya kadhi haiitaji sheria au upendeleo mwingine wowote. Waislamu wanahitaji kukutana:

a. Kuunda chombo chao cha umoja na kuangalia madhehebu yao mbalimbali
b. Chombo kitakachosimamia uendeshwaji wa mahakama ya kadhi kwa Waislamu wote (ukumbuke hata watu wanaposema 'mahakama ya kadhi' si kwamba wanazungumzia madhehebu yote ya Waislamu. Katika TAnzania yawezekana watu wa madhehebu ya Sunni watakuwa na haki zaidi na labda ni sheria ambazo wao wanazikubali ndio zitatumika; itakuwaje kwa Shia na Ahmadiya?
c. Wakubaliane jinsi ya kufinance mahakama hiyo
d. Wafikishe uamuzi wao kwa serikali ili utambulike rasmi kuwa ni wa chombo cha Kiislamu. Serikali itafuatilia tu maamuzi hayo.
e. Tatizo la mahakama ya kadhi ni kuwa nani ataizuia isihukumu mambo mengine ambayo Sheria ya Kiislamu inayo? Maana kama mahakama ya kadhi inahusika na mirathi na talaka, tunajua kuwa inatumika pia kuweza kuhukumu uhalifu - well kwanini Waislamu wasitake mahakama ya kadhi kamili yenye kuhumu mambo yote ya maisha ya Waislamu? Kwanini watake kuhukumiwa kwenye mambo ya ndoa na mirathi lakini siyo kwenye uhalifu? au hiyo si sehemu ya Ibada?
 
Hapa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, hawa watu wamezoea kukariri hivyo basi hata ueleze vipi hawataelewa zaidi ya walivyokariri

Wimbo ukizoeleka baada ya kurudiwa rudiwa basi huenda itagusa hisia zinazosema " hapa kuna kitu, nisogee au nitulie"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom