MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,607
Kwanza hiyo nyekundu, hapa hatuzungumzi kwa ajili ya nani ana hasirana nani bali mantiki ya hichi kinachozungumzwa.Assume wewe ni muislam na una wake watatu na watoto 5:4:3 yaani 12 jumla kwa wake watatu..umefariki
Kwa sheria za ndoa ya 1971; ugawaji wa urithi huo hauwezekani japo muislam huyu aliruhusiwa kuoa kiislam
Kwanini mali yake isigawanywe kiislam?? tunataka kadhi wawasaidie hao wanawake, watoto kuhusu mgawanyiko wa mali ya muumini huyu.. siyo voluntarily iwe sheria kabisa na hukumu itolewe na mahakama..ok
Ndio maana tunataka mahakama ya Kadhi..
NB: Naomba wale wenye hasira na uislam na waislamu watuache kwanza tuseme kwanini tunataka mahakama ya kadhi ili mtuelewe
Wewe mwenyewe kama ni mwislamu, unaijua dini yako na katika familia yako mnaitekeleza, utaelewa kuwa pamoja na kuwepo kwa Sheria ya Ndoa ya 1971 uliyoitaja, bado waislamu wanapotaka kuwagana mirathi, wanagawana wenyewe kwa mujibu wa sheria zao za mirathi na sina kumbukumbu za mirathi hiyo kutenguliwa mahakamani. Inawezekana zipo kesi zilizofikishwa mahakamani kwa mmoja wa mwanafamiliakuhisi ana haki ya fungu kubwa zaidi.
Kwa kuwa hapa umetaja Mahakama ya Kadhi kwa ajili ya Mirathi tu, binafsi nahisi Sheria za Mirathi za Kiiislamu ni kandamizi. Mfano, ikiwa katika famillia kuna watoto hao uliowataja 5:4:3, kati ya hao 12 mwanamume ni mmoja tu wa kiume, tena wa mwisho kabisa, basi sheria inampa fungu kubwa zaidi huyu mwanamume kushinda dada zake 11. Ninaheshimu lakini hapa hainiingiii akilini. Je mnataka sheria ili kuwakandamiza wanawake?
Jengine ni kuwa Serikali haipaswi kuunda Mahakama na kuigharimia kwa pesa za walipa kodi wote. Nafikiri unaelewa kuwa katika jamii ya waislamu wana kitgno chao cha Wakfu na huko ndio humalizana. Ikiwa ni kwa ajiliya mirathi, mahkama ya kadhi ni ya nini?