Wanaoponda kutoa sadaka kwa watumishi wakumbuke kila mtu hutoa sadaka, tofauti ni unatoa wapi

Wanaoponda kutoa sadaka kwa watumishi wakumbuke kila mtu hutoa sadaka, tofauti ni unatoa wapi

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Kitendo cha kutoa sadaka kimefungamanishwa na uhai wa binadamu kiasi kwamba huwezi kuishi bila kutoa sadaka. Ukizuia kutoa ili uujenge ufalme wa Mungu utatafuta pa kuipeleka. Ila lazima utatoa hata kama utaitungia jina tofauti.

Tendo la kwanza mwanadamu wa kwanza kuzaliwa (Kaini na Habiri) walilofanya ilikuwa ni kutoa sadaka.

Kama hutatoa sadaka kwa mtumishi ili kazi za Mungu zisikwame, au kanisani au kwa masikini na wahitaji, utatoa kwenye ngono, Michezo na burudani, pombe au kwa waganga.

Anza kupitia upya uone sadaka zako huwa zinaelekea wapi? Kujaza account au kibubu chako cha mbinguni au kupalilia kifo chako cha milele.

Heri kutoa kuliko kupokea.

Ni hayo tu.
 
Wakristo hutoa sadaka
Wayahudi (Judaism) hutoa sadaka
Wabudha hutoa sadaka
Wahindu huota sadaka
Mababu zetu walitoa sadaka
Freemasonry hutoa sadaka
Atheists wasiamini Mungu hutoa sadaka

Swala sio mimi sitoi sadaka ninanufaisha watu, kila mtu hutoa sadaka, usiseme sitoi sema nimebadilisha matumizi.
 
Acha fujo wewe, hicho kifungashio kilicho tumika kufungamanisha na uhai wangu na sadaka kiko wapi km siyo njama zenu za kuwaogofya waoga?
 
Usipotoa sadaka kanisani basi utatoa kwa waganga lakini utatoa...

Sadaka sio pesa tu hata wanyama, kuku unaoenda kutambika huko kwenu ni sadaka...

NB: Sadaka ni Ile inayompendeza Mungu, tusimuibie...
Aminaa
 
Sahihi kabisa Mimi naamini nikimbless mwamba aliyekosa chamula hio ni sadaka
Hiyo ni sadaka bora sana. Sadaka ya kumpa mtu chakula ni kubwa sana. Mungu huwa anajibu haraka kuliko ukimpa pesa akale. Jitahidi kumnunulia au kumpa chakula (physical) sio pesa ya kula. Anaweza kubadili kusudi la matoleo yako.
 
Back
Top Bottom